Natetemeka/Kigugumizi nikiongea Kiingereza

Natetemeka/Kigugumizi nikiongea Kiingereza

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Wadau hii hali inanikuta nikitaka kutema yai sijui kwa nini tena nikiwa kwenye kadamnasi napata ubaridi zaidi. Msaada jamani naaibika mwenzenu.
** Tena nikiona mademu ndo jasho linanitoka mwili mzima, nifanyeje wadau?
 
Wadau hii hali inanikuta nikitaka kutema yai sijui kwa nini tena nikiwa kwenye kadamnasi napata ubaridi zaidi. Msaada jamani naaibika mwenzenu.

Tatizo hili huwa linakupata pia ukiongea lugha ya kabila lenu?
 
Ni tatizo la watu wengi mkuu, Mimi huwa napata kiu, njaa na usingizi kwa wakati mmoja pale ninapothubutu kuzungumza kwa hiyo lugha tunayoijadili (sitaki hata kuitaja)

Haha haaaa...ni shiiida
 
Kuna siku nilienda ofisi fulani nilikuwa na shida na marketing manager katika hiyo ofisi kubwa tu.
Baada ya kumweleza secretary kwa ufupi akaenda kuniitia bwana.
Yule jamaa alikuwa mzungu inaonesha anatokea london mjini kabisa kwa akina blair, kingereza chake kilikuwa hakieleweki yaani anacharaza kama cherehani, labda akiongea ufanye kuandika kwanza. Yaani ilikuwa aibu pale.
Ili kujinasua, nikatema yai broken mfulululizo bila kumpa nafasi ya kuongea halafu nikasema thank you, nikamwambia secretary utamwelekeza vizuri kama nilivyokwambia eeh!
Ndio maana hiyo lugha siipendagi kabisa.
 
Hakikisha unatembea na ama kuberi au mzinga wa Konyagi wa kutoa nishai
 
kujifunza kingereza Kubali kuchekwa tu ila ipo siku utazoea utaongea vizuri kwa ufasaha.
Kipindi nipo f3 nilikuwa nachukua kioo najiangalia halafu naanza kuongea kingereza na ile image yangu kwenye kioo,nikimaliza namtafuta mtu anayejua kingereza naanza kuongea nae nikikosea narekebishwa narudi tena kwenye kioo,mpka nafika f6 nilikuwa natema yai la hatari
 
Back
Top Bottom