Natetemeka/Kigugumizi nikiongea Kiingereza

Natetemeka/Kigugumizi nikiongea Kiingereza

Hah..hah..hah...sham_ok naona moderator wameunganisha ID zako...teh..teh..teh... JamiiForums raha sana.
 
tah tah tah tah, mkuu umenifurahisha sana, ni wazi kwamba lugha hiyo tajwa hujaimaster vizuri,ndio maana huwa unatetemeka wakati unaongea, ushauri wangu acha kabisaa hadi hapo utakavyowaona british council maana utakuja kuaibika zaidi,tumia lugha yako unayoimudu katika kuwasiliana,over
 
Nifafanulie wameunganisha na ipi

Jamaa alikuwa ana ID mbili, moja inaitwa Secrete na nyingine ni Joshua_ok, anaanzisha thread kwa ID ya Secrete anakuja kujijibu kwa ID ya Joshua_ok ..nikaanzisha thtead ya kuwataja wote wanaotumia ID mbili kujianzishia thread na kujijibu kwa ID nyingine ..mods wakafuta thread yangu na kuunganisha ID zao. Angalia Thread zote za huyu jamaa utaona Secrete alikuwa anakuja kujibu(lakini sasa comment zote zilionekana kwa ID ya secrete zinaonekana kwa ID ya Joshua_ok baada ya mods kuziunganisha.
 
duuu tatizo langu ni lako sasa mimi hadi jasho linanitoka sasa sijui kiingereza kina jiko la gesi au vipi
Umesababisha nicheke sana!! Duuuh!

ila fanyeni mazoezi ya kuongea pekee [yako], kisha tafuta watoto wanaoweza kuongea uwe unafanya nao majaribio ya kuongea na kisha ongea na watu. Mimi nilikuwa najifunza kifaransa niko nje ya Tz nilifanya hivyo saa ivi naongea vizuri kifaransa.

Ila kunywa sijui mzinga au mbunduki au kiroba utajiaibisha sana, maana utashangaza umati hujui ulichoongelea .

Asanteni.
 
Nimecheka sana. Nilikua hivyo kipindi cha nyuma, ila sasa hivi Kidogo nina confidence ya kusimama mbele ya mkutano na kutema yai. Maana nimegundua sio wazungu wote pia wanajua hii lugha. Nchi nyingine na wao wanatema broken balaa
 
Back
Top Bottom