Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
National Alliance For Mass Advancement(NEMA)
Nimeingia Maktaba na nimekuta picha ambazo nilipiga mimi mweyewe kwa mkono na jicho langu ukumbi wa Arnautoglu miaka 28 iliyopita. Ilikuwa siku ambayo msajili wa vyama anahakiki wanachama wa NEMA. Leo asubuhi naziangalia picha hizi nacheka peke yangu kama mwehu.
Nacheka kwa kuwa picha hizi zimenikumbusha mengi katika ujana wangu na mambo ambayo yalinishughulisha.
Mambo ambayo hivi sasa siwezi kuyafanya tena. Siwezi kuyafanya si kwa kuwa hayana maana, ila ile nguvu ya kwenda huku na kule haiko tena.
Nacheka na kumshukuru Allah kwa kutupa ujasiri wa kupambana na nguvu iliyokuwa na nguvu kubwa, na sisi hatuna chochote ila kule kukataa kudhulumiwa.
NEMA ilipata usajili wa muda tarehe 19 May, 1994. Siku ya usajili asubuhi na mapema wanachama wa NEMA tumeshafika ukumbi wa Arnautoglu tunawasubiri maofisa wa msajili wa vyama vya siasa afike. Ukumbi huu una historia kubwa katika siasa za Tanganyika.
Mle ndani ukumbini tulipokuwa tumekaa ndipo mwaka wa 1953 ulipofanyika uchaguzi wa mwaka wa TAA kumpata rais mpya. Uchaguzi huu ulikuwa baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere, Nyerere akachukua uongozi. Hiki ni kisa nimekieleza mara nyingi na wasomaji wangu naamini wanakijua vyema.
Fikra nyingi zikawa zinanipita kichwani najiambia, hivi wazee wetu waliounda TANU wakifufuka leo na kuja hapa Arnautoglu wakatuuliza imekuwaje mbona mnaunda chama kingine ile TANU tuliyowaundieni iko wapi, hivi tutawapa jibu gani? Majibu sasa yanafuatana na kuongozana moja baada ya lingine.
Lakini nikawa naamini kuwa hawa marehemu wazee wetu waliofufuka watakapo angalia wanachama wa NEMA watashangazwa na kitu kimoja. Wanachama wote tuliokuwa mle ndani ukumbini ni waswahili, kama walivyoanza wao katika ukumbi huu huu mwezi August 1954, TANU ilipoitisha mkutano wake wa kwanza.
Angalia picha hapo chini ya wanachama wa NEMA wakiwa ndani ya ukumbi wakisubiri kuhakikiwa. Fananisha na picha ya pili chini yake ya mkutano wa TANU wa mwaka wa 1955 uliofanyika Gandhi Hall, Hindu Mandal Dar es Salaam. Katika mkutano huo wa TANU wa mwaka wa 1955, kulikuwa na wajumbe wawili kutoka Lindi - Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjawale.
Hawa walikuja na ujumbe maalum kutoka Southern Province kwa viongozi wa TANU makao makuu, kuwaeleza kuwa TANU inapataka pingazimi kutoka kwa wamishionari wanawazuia waumini wao wasijiuge na TANU kwa kueneza propaganda, kuwa TANU ilikuwa inataka kuanzisha vita vya maji maji dhidi ya waingereza kama walivyofanya akina Abdulraufu Songea Mbano.
Bila shaka maofisa waliokuwa wanahakiki wanachama wa NEMA, hili kuwa kila anaekuja mezani na kadi ya NEMA ni Muislam liliandika alama ya kuuliza vichwani mwao, na hivi ndivyo ilivyokuwa mikoani kote walikopita. Kwa kawaida inawezekana katika vyama vingine ikawa hakuna waislam na walio wengi wakiwa wengine, lakini kwa kawaida ya siasa za Tanzania hili huonekana sawa, tatizo linakuja pale wanapokuwapo waislam wengi.
Moja katika magazeti yaliyokuwa yanachuki kubwa na waislam na uislam Shaba likaandika kuwa, NEMA ni chama cha Waislam (Shaba, 19-25 July, 1994). NEMA ikatoa taarifa kupinga hilo lakini haikusaidia kitu. Msajili wa vyama vya siasa tokea mwanzo alifanya kila juhudi kuhakikisha kuwa NEMA hakipati usajili.
NEMA iliomba usajili kamili na kwa zaidi ya mwaka msajili wa vyama vya siasa hakuchukua hatua yoyote alibakia kimya. Mwishowe NEMA ilinyimwa usajili kwa kile kilichoelezwa kushindwa kutimiza masharti ya sheria ya vyama vya siasa. Lakini ukweli ulikuwa unajulikana wazi kabisa na huu haukuwa mwisho. Wanachama wa NEMA wakahamia kwengine kwenye chama kilichokuwa kimeshapata usajili.