National Alliance for Mass Advancement(NEMA), chama kilichonyimwa usajili kwa kuogopwa wanachama wake

National Alliance for Mass Advancement(NEMA), chama kilichonyimwa usajili kwa kuogopwa wanachama wake

Historia ni jambo linalovutia.
 
Hii Nchi ina historia tamu sana hasa namna Watawala wa mwanzo walivyoifinyanga ili kuondoa au kuzuia chokochoko za wachache waliotaka kutugawa.

Ilianza na chama cha NRA akiwemo na Kighoma Malima, kulikuwa na harufu kali sana ya 'dini'. Wazalendo kitengoni wakawa wanawafuatilia kwa makini humohumo ndani kwao na hatimaye kikafa bila kuleta athari yeyote ya mgawanyiko. Akaja Mtikila na kelele zake, wakamwangalia na kumuacha wakijua mbio za sakafuni zinaishia ukingoni. Hatimaye Mtikila kaondoka Duniani akiwa na wanachama wasiojaa hata kwenye basi la mkoani.

Wakatokea wachache wakataka kuifanya CUF kama chama cha mlengo flani, lakini matokeo yake kikajitahidi kujijenga Kitaifa na hatimaye leo kimekuwa historia.

Ila nilichojifunza Nchi hii ni kuwa, Watu wengi hawapendi harufu za migawanyiko, ndiyo maana wanapogundua kuna hila flani huwa wanajitenga na hata hawakuambii, kimyakimya.

Mimi nilikuwa msomaji mkubwa wa gazeti la Annur, kwa waliokuwa wanalisoma wakati huo watakubaliana na mimi kuna makala zilikuwa kali sana na zinazochochea mgawanyiko au kuonyesha sisi na wao, na likinunuliwa sana na baadhi ya Ndugu zetu Waislam, lakini nini kilitokea? Sasa lipo hoi bin taabani. 'Wazalendo wangeweza hata kulifungia kama walivyokuwa wanafungia magazeti mengine, lakini wakaliacha wakijua kwa yakini kabisa, wanaonunua watalichoka tu kwa sababu linawapeleka kwenye utamaduni usiokuwa wa kwetu.
Editorial Panel ya hilo gazeti (Annur) sidhani kama Mzee wetu atakosekana!
 
Kwenye ulimwengu huu wa Sasa, Kama bado Kuna mtu anazungumza udini huyo atakuwa ni mtu duni sana kifikra
 
Plato...
Mimi si mtu wa kuandika mambo hayo ya suti nk.

Mimi naandika mambo ambayo mtu akiona post yangu atasimama kusoma kwa kuwa kipo atakachojifunza.

Kupokelewa kwa Nyerere Dar es Salaam ni muhimu sana katika historia yake kwani vinginevyo vipi angeweza kukubalika?

Pugu si Dar es Salaam mjini Mtaa wa Stanley na Sikukuu nyumbani kwa Abdul Sykes, Act. President na Secretary wa TAA.

Pugu si Kariakoo Market ambako Abdul Sykes alikuwa Market Master.

Hapo kulikuwa na watu maarufu na wanachama wa TANU kama Mzee Mshume Kiyate na Shariff Abdallah Attas.

Watu wengi walimfahamu Nyerere hapo na nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya kuacha kazi ya Ualimu na kuhama Pugu.

Hapa kuna historia ya kusisimua.

Nakuwekea picha ya Mwalimu Nyerere akiwa Uwanja wa Ndege safari ya kwanza UNO 1955 kasindikizwa na mke wa Shariff Attas, Bi. Chiku int Said Kisusa, Bi. Tatu bint Mzee Bi. Titi Mohamed na akina mama wengine wawili sijapata majina yao.

Hawa akina mama ndiyo waliokuwa wanaifanyia kampeni mikutano ya TANU kujaza wanawake viwanja vya Mnazi Mmoja na wakihudhuria mikutano ya ndani nyumbani kwa Abdul Sykes siku moja kabla ya mkutano kuweka mikakati.

Hapo ndipo ninaposema kama mtu haijui historia ya Mwalimu na historia ya TANU atataabika sana.

Kuna kipindi cha TV kitarushwa hivi karibuni.

Picha hiyo watayarishaji wa kipindi hicho wakiwa kazini mimi niko pembeni yao nikieleza jinsi baadhi wanachama wa TANU na baadhi ya viongozi walivyokuwa wakikusanyika ofisi ya TANU, New Street kisha pamoja kwa maandamano wakienda Mnazi Mmoja mbele umetangulia Mganda.

Picha ya mwisho hiyo ipo hapo Mnazi Mmoja watu wanasema imewekwa hapo kama kumbukumbu ya Mganda uliokuwa ukiwaleta TANU mkutanoni Mnazi Mmoja kumsikiliza Mwalimu Nyerere.

View attachment 2334806
View attachment 2334815
View attachment 2334844
Nilijua tu utaleta mpaka wapiga picha. Najua maandishi yako na kwa bahati nzuri huwa napenda consistence yako. Hata kama ni uwongo huwa unajitahidi kuurudia hata mara elfu.

Kwamba Mwalimu asiijue Dar es Salaam mpaka apokelewe!
Kwamba Kighoma Malima ndiye alienzisha mfumo wa namba kwa watahiniwa. Uwongo uliothibitishwa na Watu wengi hapa jamvini.

Hakuna shida, nimeshaeleza, maadam pamoja na hizo hila siye tupo wamoja hiyo inatosha sana.

Ila andika Mzee wangu, kila Mtu na namna yake ya kuishi. Na kwa hilo sina kinyongo kabisa
 
Nilijua tu utaleta mpaka wapiga picha. Najua maandishi yako na kwa bahati nzuri huwa napenda consistence yako. Hata kama ni uwongo huwa unajitahidi kuurudia hata mara elfu.

Kwamba Mwalimu asiijue Dar es Salaam mpaka apokelewe!
Kwamba Kighoma Malima ndiye alienzisha mfumo wa namba kwa watahiniwa. Uwongo uliothibitishwa na Watu wengi hapa jamvini.

Hakuna shida, nimeshaeleza, maadam pamoja na hizo hila siye tupo wamoja hiyo inatosha sana.

Ila andika Mzee wangu, kila Mtu na namna yake ya kuishi. Na kwa hilo sina kinyongo kabisa
Plato...
Mimi si nliyowaita hao watu wa media.

Wao walikuja kwangu kufanya kipindi na tulikaa nyumbani kwangu Maktaba tikafanya ''recording.''

Wakaniomba kuwa intapendeza kama tutawenda ''on site,'' ili wafanye recording nyingine ya sehemu ambazo nimezieleza.

Ninaposema kupokelewa sina maana ya mgeni kutembezwa mjini.
Ikiwa mimi nasema uongo basi hii ni nafasi yako wewe kueleza ukweli.
 
Hawezi kukosekana! Hahahaa
Nchi hii nzuri sana pamoja na mapungufu yake
Plato...
Hakika siwezi kukosekana.
1661457875494.png
 
Kwenye ulimwengu huu wa Sasa, Kama bado Kuna mtu anazungumza udini huyo atakuwa ni mtu duni sana kifikra
Mzee...
Umesema kweli.

Ikiwa kutakuwa na watu ndani ya serikali wanakaa na kupanga mipango ya kuwahujumu watu wengine kwa kuwa si watu wa imani yao huu ni msiba mkubwa sana.

Soma bango hilo hapo chini:

1661458254057.png

Bango katika maandamano ya Waislam kupinga hujuma ya Baraza la Mitihani (NECTA) dhidi ya shule za Kiislam 2012. Mkurugenzi wa NECTA alikuwa Dr.Joyce Ndalichako ambae baada ya kutoka NECTA akawa Waziri wa Elimu.
 

..asante kwa historia hii.

..umenivunja mbavu hapo ulipoandika mawazo yaliyokuwa yakizunguka akilini mwako siku mliyokuwa Anartouglo Hall.
JK,
Nilikuwa naleta kumbukumbu ya mkutano wa kwanza wa TANU hapo ukumbini August 1954.

Aliyekuwa anaalika watu kuhudhuria mkutano huo alikuwa Abbas Sykes.
Alikuwa kijana mdogo wa miaka 25.

Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.


1661458583559.jpeg

Abbas Sykes​
 
Zimekuongezea ujuha wewe. Sisi wengine zimetusaidia
Mwama...
Mara kadhaa huyu bwana amekuwa akija kwangu na lugha za dharau ya Uislam ingawa anajificha nyuma ya kuwa haamini dini yeyote.

Kwa kawaida unapoona mtu anaushambulia Uislam kwa kujificha nyuma ya upagani ukweli ni kuwa zamani alikuwa Mkristo.

Huwezi kukuta Muislam katika mambo kama haya ya kumkana Allah hata kama atakuwa asi wa kutupwa.

Mimi simjibu kwa kuamini kwanza suala la dini ni la mtu binafsi na katiba ya nchi ina heshimu na kutambua uhuru wa kuamini.

Halikadhalika Allah katika Qur'an anasema hakuna kulazimishana katika dini kwani ukweli uko wazi.

Naogopa kuwa ikiwa nitamjibu yeye atapata ukaidi na hatari anaweza akamtukana Allah.

Lakini kuwa hoja yangu hapa ni mchango wa Waislam katika kupambana na ukoloni.

Hili si suala la kama Uislam ni dini ya haki au vinginevyo.
 
Moja ya kazi nzuri inayofanywa na CCM ni kuzuia siasa za kidini. Siku ikitoka madarakani nchi itapasuka kidini. Vyama vyote vya upinzani vimeshindwa kuiga jambo hili zuri kutoka CCM.
 
Moja ya kazi nzuri inayofanywa na CCM ni kuzuia siasa za kidini. Siku ikitoka madarakani nchi itapasuka kidini. Vyama vyote vya upinzani vimeshindwa kuiga jambo hili zuri kutoka CCM.
Lycoon...
Sikiliza hiyo video ya William Lukuvi hapo chini:
 
Ujoka,
Ikiwa wewe fikra yako ni kuwa umoja wa kitaifa utaimarika kwa Waislam kuwa raia daraja la tatu huo moja kamwe hautapatikana.

Unajua kuwa tuko 20:80?
Huu ndiyo umoja unaokupendeza wewe?

Unatarajia hawa 20 waliokuwa mstari wa mbele kuondoa dhulma za wakoloni wanaridhika na hali hii?
Hii 20:80 Hata leo ipo?.
Au ni zama nyuma?
 
Back
Top Bottom