National Alliance for Mass Advancement(NEMA), chama kilichonyimwa usajili kwa kuogopwa wanachama wake

Historia ni jambo linalovutia.
 
Editorial Panel ya hilo gazeti (Annur) sidhani kama Mzee wetu atakosekana!
 
Kwenye ulimwengu huu wa Sasa, Kama bado Kuna mtu anazungumza udini huyo atakuwa ni mtu duni sana kifikra
 
Nilijua tu utaleta mpaka wapiga picha. Najua maandishi yako na kwa bahati nzuri huwa napenda consistence yako. Hata kama ni uwongo huwa unajitahidi kuurudia hata mara elfu.

Kwamba Mwalimu asiijue Dar es Salaam mpaka apokelewe!
Kwamba Kighoma Malima ndiye alienzisha mfumo wa namba kwa watahiniwa. Uwongo uliothibitishwa na Watu wengi hapa jamvini.

Hakuna shida, nimeshaeleza, maadam pamoja na hizo hila siye tupo wamoja hiyo inatosha sana.

Ila andika Mzee wangu, kila Mtu na namna yake ya kuishi. Na kwa hilo sina kinyongo kabisa
 
Plato...
Mimi si nliyowaita hao watu wa media.

Wao walikuja kwangu kufanya kipindi na tulikaa nyumbani kwangu Maktaba tikafanya ''recording.''

Wakaniomba kuwa intapendeza kama tutawenda ''on site,'' ili wafanye recording nyingine ya sehemu ambazo nimezieleza.

Ninaposema kupokelewa sina maana ya mgeni kutembezwa mjini.
Ikiwa mimi nasema uongo basi hii ni nafasi yako wewe kueleza ukweli.
 
Kwenye ulimwengu huu wa Sasa, Kama bado Kuna mtu anazungumza udini huyo atakuwa ni mtu duni sana kifikra
Mzee...
Umesema kweli.

Ikiwa kutakuwa na watu ndani ya serikali wanakaa na kupanga mipango ya kuwahujumu watu wengine kwa kuwa si watu wa imani yao huu ni msiba mkubwa sana.

Soma bango hilo hapo chini:


Bango katika maandamano ya Waislam kupinga hujuma ya Baraza la Mitihani (NECTA) dhidi ya shule za Kiislam 2012. Mkurugenzi wa NECTA alikuwa Dr.Joyce Ndalichako ambae baada ya kutoka NECTA akawa Waziri wa Elimu.
 

..asante kwa historia hii.

..umenivunja mbavu hapo ulipoandika mawazo yaliyokuwa yakizunguka akilini mwako siku mliyokuwa Anartouglo Hall.
JK,
Nilikuwa naleta kumbukumbu ya mkutano wa kwanza wa TANU hapo ukumbini August 1954.

Aliyekuwa anaalika watu kuhudhuria mkutano huo alikuwa Abbas Sykes.
Alikuwa kijana mdogo wa miaka 25.

Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.



Abbas Sykes​
 
Zimekuongezea ujuha wewe. Sisi wengine zimetusaidia
Mwama...
Mara kadhaa huyu bwana amekuwa akija kwangu na lugha za dharau ya Uislam ingawa anajificha nyuma ya kuwa haamini dini yeyote.

Kwa kawaida unapoona mtu anaushambulia Uislam kwa kujificha nyuma ya upagani ukweli ni kuwa zamani alikuwa Mkristo.

Huwezi kukuta Muislam katika mambo kama haya ya kumkana Allah hata kama atakuwa asi wa kutupwa.

Mimi simjibu kwa kuamini kwanza suala la dini ni la mtu binafsi na katiba ya nchi ina heshimu na kutambua uhuru wa kuamini.

Halikadhalika Allah katika Qur'an anasema hakuna kulazimishana katika dini kwani ukweli uko wazi.

Naogopa kuwa ikiwa nitamjibu yeye atapata ukaidi na hatari anaweza akamtukana Allah.

Lakini kuwa hoja yangu hapa ni mchango wa Waislam katika kupambana na ukoloni.

Hili si suala la kama Uislam ni dini ya haki au vinginevyo.
 
Moja ya kazi nzuri inayofanywa na CCM ni kuzuia siasa za kidini. Siku ikitoka madarakani nchi itapasuka kidini. Vyama vyote vya upinzani vimeshindwa kuiga jambo hili zuri kutoka CCM.
 
Moja ya kazi nzuri inayofanywa na CCM ni kuzuia siasa za kidini. Siku ikitoka madarakani nchi itapasuka kidini. Vyama vyote vya upinzani vimeshindwa kuiga jambo hili zuri kutoka CCM.
Lycoon...
Sikiliza hiyo video ya William Lukuvi hapo chini:
 
Hii 20:80 Hata leo ipo?.
Au ni zama nyuma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…