National Intelligence and State Intelligence

Spetnaz ni neno la kirusi lenye maana ya kikosi maalumu. Spetnaz zipo nyingi. Labdi ulikuwa unaongelea GRU- Spetnaz na vikosi vyake viwili Zapad na Vostok
 
Hapo kwenye SAD nahisi kama umetulisha tango pori. Review makala yako tena.
 
I think people need to STOP trying to read something into everything and quit making mountains out of mole hills!
am sorry didn't know you gon' get offended, am gon' delete my previous post
 
Andiko zuri sana. Ila ili tu kwa ajili ya wasomaji ni kuwa, Kuhusu kitengo cha "KIDON" cha Israel hakifanyi kazi yake nje ya sheria za nchi{ Kiusalama}.

Maana KIDON ni TAWI maalumu la shirika la ujasusi la Israel Mossad. Ambalo lilianzishwa rasmi mwaka wa 1949 kama kitengo maalumu cha kulilinda taifa la Israeli dhidi ya MAADUI wa NJE ya nchi na SI wa NDANI ya nchi.

Masuala ya ndani yanasimamiwa na kitengo kingine kiitwacho Shin Bet.{ ISA} nacho HAKIUI raia waliona mtazamao tofauti na serikali ya
Kikosi cha KIDON HAKIUI RAIA wa nchi ya Israel hata kama wana maoni tofauti na Waziri mkuu na serikali yake.

Nakubaliana nawe kuwa ni cha siri sana.

Na Mara nyingi WANAOJIUNGA ni LAZIMA wawe wamepitia jeshini na si jeshi tu {IDF} bali ni wale waliopitia mafunzo maalumu ya SPECIAL FORCES unit. Na WAKASTAFU AMA KUTOKA Huo ndo utaratibu wao ulivyo.

Kwa kifupi KIDON HAIUI raia wanoipinga SERIKALI.Waziri mkuu anaweza kushitakiwa haraka sana.Maana si kikosi chake binafsi. Kinatambulika KISHERIA.

Kazi yao n kwenda NJE ya nchi kuwafuata maadui wa taifa na hasa hutumika tu katika HIGH VALUE TARGETS/Kazi maalumu ambayo ni lazima imalizwe kwa ajili ya kulinda taifa lao kwa Usalama wa Israeli.
Na hata KNESSET amabalo nibunge laowanajua ni sheriaya Mosssad.Na silazimawajue kila SIRI.

Kumbuka Israel ni nchi inayofuata sheria sana.Hata WAZIRI MKUU anaweza kushitakiwa hata akiwa madarakani akifanya
mambo kienyeji, UFISADI nk.
Nimefurahishwa na kujifunza mengi. Kudos sir.
 
Nzuri sana naomba kitabu chako nisome nadhani ntaelewa zaidi?
 
Kakuambia hakufundishi kuelewa anakufudisha kufikiri, kama uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo siyo kosa lake na kama huwezi ku 'relate' mifano ya Marekani na ya Tanzania pole.

Ushauri wangu, penda kujisomea vitabu mbalimbali uongeze maarifa kusoma vitabu vya wazungu sio utumwa, after all vitabu vingi tunavyotumia mashuleni hata ulivyotumia wewe vimeandikwa na wazungu, hata hiyo computer au smartphone unayotumia imetengenezwa na wazungu kwahiyo na wewe ni mtumwa wa wazungu?
 
 

NCHI YETU HAINA MAMA NITILIE NA WAKULIMA WA KOROSHO TU....KUNA WENGINE WENYE UWEZO NA LEVEL YA JUU AMBAO WANAWEZA KUCHANGANUA HAYO YALIYOANDIKWA NA KUWAELIMISHA WENGINE. HAYO MAWAZO YA KUWA KILA MMOJA ANATAKIWA NA LAZIMA AJUE KITU FULANI YAMEPITWA NA WAKATI, HATA HUKO CHINA KWENYE UKOMUNISTI HAYAPO. TATIZO LA NCHI YETU BADO TUNAENDELEA KUWA NA "HANGOVER YA UJAMAA" WENYE MAWAZO KAMA YAKO WANAJIDANGANYA KUWA UKIANDIKA KITU LAZIMA KIELEWEKE KWA AUDIENCE YOTE (WAKULIMA WA KARANGA, MIHOGO NA MAMA/BABA NITILIE) PLEASE THINK OUT OF THE BOX. KAMA UKIWA NA MAWAZO HAYO BASI KUNA HAJA GANI YA KUWA NA VYUO VIKUU? KWA SABABU CHEMISTRY/ENGINEERING AU MAMBO MENGINE MAZITO MKULIMA NA MAMA/BABA NITILIE WATAELEWAJE? LAZIMA TUWE NA MAWAZO TOFAUTI NA TUKUBALIANE MAMBO MENGINE YA JUU YA UWEZO WA WATU WENGINE, WAO WATAELEWA YALE TU YA LEVEL YAO NA SIYO KILA KITU KITA-FIT JAMII NZIMA. NDIYO MAANA KUNA "THINK TANK"MIFANO ULIYOTUMIA SIYO "VALID"
YERICKO AMEELEZA VIZURI WENYE KUELEWA WATAELEWA....WASIOELEWA WATAOMBA MSAADA WA KUELEWESHWA KAMA WATAHITAJI, SIYO LAZIMA KILA MTU AJUE KILA KITU. WATANZANIA BADO TUNA KASUMBA KWA SABABU BADO TUMELALA.
 
Samahani kwa kukukosoa. Naamini kuwa uongo usiporekebishwa unaweza kuonekana ukweli.

Ni rahisi sana kuwadanganya Watanzania wengi. Na sababu kuu ni wengi wao kutojihangaisha japo ku-Google vitu mbalimbali wanavyokutana navyo mitandaoni au hata katika maongezi.

Unfortunately, tuna wenzetu ambao ni mahiri sana katika kutumia udhaifu huo, ambapo huzusha habari huku wakijua bayana hakuna atakayejihangaisha ku-countercheck. Kibaya zaidi, hata mtu aki-volunteer kuweka rekodi sawa, chances are ataonekana kama hater flani.

Situation could become even worse katika zama hizi za fake news, maana hiki ni kipindi ambacho mlaji wa habari/taarifa shurti afanye jitihada za ziada kusaka ukweli, kwa vile hata baadhi taasisi za habari za rekodi nazo zaweza kujiingiza katika mkumbo wa fake news.

Back to kwako Bwana Yericko. Sijui ulidanganywa, au umeamua tu kudanganya, lakini tafsiri ya ulichokiita "national intelligence" ni mgawanyiko tu wa majukumu ya kiintelijensia ndani ya taifa husika, ilhali ulichokiita "state intelligence" ni ujumla wa intelijensia kwa taifa husika, mara nyingi kwa kulinganisha na taifa jingine. Maelezo yako kuhusu maneno hayo sio sahihi.

Umeandika "National Intelligence huwa ipo kisheria (Legal), na State Intelligence huwa haipo kisheria (illegal). Wanaweza kufanya kazi moja, mahali pamoja, nk Tofauti yao nikuwa kimoja Natinal Intelligence kinafanya kazi chini ya miiko na taratibu za kisheria kwa nchi husika, na State Intelligence hakitambuliwi na sheria yoyote zaidi ya (decree) na mara nyingi huwa hakifahamiki na wengi katika serikali, huenda katika nchi kikafahamika na watu watano au sita tu." Nani aliyekudanganya? Or rather kwanini unadanganya?

Labda kwa kukusaidia tu, ni vema ukajielimisha kuhusu tofauti/mfanano kati ya" nation" na "state" na maana ya "intelligence" kisha ulete hiyo nonexistent dichotomy kati ya "national intelligence" vs "state intelligence." Sio siri, upotoshaji wa aina hii unakera hasa ikizingatiwa kuwa haya ni masuala nyeti.

Bila aibu unaandika "Special Activites Division (SAD)... huendesha shughuli zenye maslahi ya rais, chafu, mbaya na pia dhalili zenye maslahi kwa nchi na muda mwingine kwa maslahi ya wakuu katika nchi au katika vikosi husika. Uwepo wacho hautambuliwi na katiba wala sheria yoyote." Urais Marekani ni taasisi, na tofauti na akina sie ambapo kimsingi Rais ndio mkuu" halisi" wa Idara ya Usalama wa Taifa, kwa wenzetu uhusiano kati ya Rais na taasisi za intelijensia ni wa kitaasisi kuliko matakwa binafsi.

Special Activities Division ya CIA ni moja tu ya vitengo kadhaa vya Idara hiyo ya ujasusi. Ipo kisheria na uwepo wake unafahamika. Kwa wenye uhusiano mzuri na Google, fanya kuuliza, kisha linganisha na hicho anachodai Bwana Yericko.

Kwa kifupi, Special Activities Division ni kitengo kinachohusika na "covert operations." Na kimegawanyika sehemu mbili, "Special Operations Group" (SAD/SOG) kwa ajili ya operesheni zenye ujeshi ndani yake (tactical paramilitary operations) na "Political Action Group" (SAD/PAG) kwa ajili ya operesheni za siri za kishushushu kuhusiana na siasa (covert political action). Kama ilivyo nature ya CIA, yaani taasisi ya ujasusi, shughuli hizi hulenga mataifa mengine. Special Activities Division humpatia Rais wa Marekani option mbadala pindi njia za kidiplomasia zinapoonekana hazina ufanisi.

Kwa wenye uhusiano mzuri na Google, bonyeza hapa https://www.google.co.uk/search?biw....64.mobile-gws-serp..1.0.0....248.aG24GvAxhbo

Kuhusu Kidon ya Israeli, Bwana Yericko umefanya kile Waingereza wanaita "telling tall stories," tuseme "changa la macho" kwa lugha ya mtaani. Kufupisha maelezo, Kidon ni kitengo cha Mossad kama ilivyo Special Activities Division ya CIA, kinachofanya shughuli zake (mostly mauaji) kwa usiri mkubwa kupindukia. Na hiyo "usiri mkubwa kupindukia" ni kama utani katika ushushushu, kwa sababu taaluma yenyewe nzima ni ya "usiri mkubwa kupindukia."

Kidon hufahamika kama "Mossad ndani ya Mossad" kwani ipo "compartmentalised" kwa kiwango cha juu kiasi kwamba hata ofisi zake hazipo katika makao makuu ya Mossad. Na ni nadra kwa maafisa wa Kidon, wanaojulikana kama "The Team" kwenda katika ofisi za Mossad. I hope Bwana Yericko utawaeleza "raia" maana ya "compartmentalisation."

Kidon - neno la Kiyahudi lenye maana ya singe (bayonet) - imebobea katika "infiltration" (kujipenyeza) katika nchi mahasimu wa Israel kwa lengo la kuuwa bila kuacha alama.

Moja ya faida kubwa kwa Mossad ni asili ya uhamiaji wa Waisraeli, kwa maana kwamba wengi wao wana asili pia ya nchi mbalimbali duniani, na hiyo inawapa faida moja muhimu majasusi wa nchi hiyo: uwezo wa hali ya juu kumudu lugha na tamaduni za nchi nyingine. Na maafisa wa Kidon ni wanufaika wa faida hiyo.

Again, kwa mwenye muda, au mwenye kiu ya kujua zaidi kuhusu Kidon, link ya kusaka taarifa zao mbalimbali ni hii https://www.google.co.uk/search?q=k...j0l2.2964j0j4&sourceid=chrome-mobile&ie=UTF-8

Kuhusu Spetsnaz, Bwana Yericko umeongopa kwamba "Nchini Urusi nako ikulu ya Kremlin chini ya Vladimir Vladimirovich Putin ina kikosi ndani ya jeshi kitwacho Spetsnaz ambacho kazi yake kubwa ni kudhibiti wapinzani wa kisiasa na wanaharakati nchini Urusi, kikosi hiki kipo ndani ya shirika la Ujasusi la nchi hiyo la FSB japo kinaundwa zaidi na wanajeshi wa Red Army na hakitambuliwi kwa sheria yoyote ndani na nje ya Urusi." Uzuri wako Bwana Yericko ni kwamba unajua kuupamba uongo hadi unaonekana kama ukweli.

Kwa kifupi, tofauti na "tall story" yako Bwana Yericko, neno "spetsnaz" ni neno la jumla (umbrella term) lenye maana ya "special forces" kwa Kirusi, na linatumika sio Russia pekee bali pia katika mataifa mengine ya Ulaya Mashariki hasa yale ambayo zamani yalikuwa sehemu ya USSR.

Tofauti na porojo zako Bwana Yericko kwamba "spetsnaz" (special force) ipo chini ya FSB, ukweli ni kwamba ipo chini ya GRU na hujulikana kama "Spetsnaz GRU." Kwa ufafanuzi, GRU ni idara ya intelijensia ya kijeshi (military intelligence) na FSB ni Idara ya intelijensia ya ndani ya Russia, ilhali Idara ya ujasusi ya nchi hiyo ni SVR.

Again, mengi kuhusu Spestnaz, kiungo hiki hapa www.google.co.uk/search?q=spetsnaz&oq=sp&aqs=chrome.0.69i59l2j69i57j69i61j0j69i61.2434j0j9&sourceid=chrome-mobile&ie=UTF-8

Kuhusu Zanzibar, anachoongelea Bwana Yericko ni matumizi fyongo ya Idara ya Usalama wa Taifa, na wala si uwepo wa "Idara ya Usalama wa taifa ya Zanzibar." Modern equivalent ni hicho kinachosemekana kuongozwa na Bashite hivi sasa.

Kwanini Bwana Yericko unamuua kupotosha umma makusudi? Jibu unalo mwenyewe. Nakuheshimu kama mtu unayejibidiisha sana kusaka uelewa, lakini huwa nashindwa kuelewa kwanini at times anaamua kuhatarisha reputation yake kwa "tall stories." Yatendee haki maeneo usioyaelewa.

Nikusaidie kwa ufahamu huu wa traits tatu za very intelligent people
Jaribu kuzingatia hiyo ya tatu

Samahani Bwana Yericko kama nitakuwa nimekukwaza lakini ni vema kuweka rekodi sawia, maana uongo usipopingwa waweza kuwa ukweli. Otherwise, hongera kwa mapenzi yako kwenye taaluma ya intelijensia.
 
Watu wengine wanastaajabisha sana. Wanataka kumshurutisha mtu aandike kile watakacho wao vinginevyo KOSA!

 
Kitengo kina fani mbalimbali na kila mtu ni specialist,
Huwez fanya kwenye hiyo idara bila kuwa mtaalam wa jambo fulani

Mfano;Kama lissu angeletwa muhimbil wataalam wangemalizia phase 2

Mbowe aliwaza vema
Tambua fika, wauaji wa serikali wangepewa kazi ya kumuua Lisu, asingelikuwa hai sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…