National Intelligence and State Intelligence

Uongo gani ambao Yericko kausema au kusema kuna tofauti kati ya National na State Intelligence, na mbona unayemsifia kazunguka mlemle alimopita Yericko.
Sidhani kama umesoma vitu vizuri na kuvielewa. Halafu ni kushauri tu unapotaka kufanya analysis ya kitu chochote jibidiishe kujielimisha mwenyewe from other sources thn ndo uje humu utajua wapi unalishwa matango pori wp unaambiwa ukweli.

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Karai jingine lililoamua kuja na stori za alfulelaulela...unapiga stori za vikosi unavyodai ktk nchi wanaweza kuwa wanavifahamu watu wawili then unatoa maelezo as if na wewe ni miongoni mwa hao watano...Makarai acheni kutuongopea tuna akilii
 
SAD ni kitengo cha CIA,
operation nyingi za siri wanafana hawa ikiwemo mauaji,na sio lazima iwe ni amri ya rais ama rais ajue nini wamefanya,
anaweza akajua director wa CIA,
ama hata yeye anaweza asijue,
mfano boss wa kawaida ndani ya CIA anaweza ku authorise operation na hawa SAD wakafanya,na inaweza isiwe kwa maslahi ya rais au nchi,
inaweza ikawa kwa maslahi ya kikundi cha watu ndani ya CIA,ama ndani ya uongozi wa marekani,mfano senator fulani,au pengine labda foreign secretary etc,
rais wa marekani haidhinishi operation zote zinazofanywa na CIA,nyingi hupewa taarifa baada ya operation,
ama hata asipewe taarifa
 
strugo BOMBERDIER INAMSAIDIA NINI MAMA LISHE? USILAZMISHE WATU NAMNA YA KUFKIRI WAKAT HATA WEW UWEZO WAKO WA KUFKIRI NI 0.1%
 
Oii UMESEMA WATU WA SERIKALI WANGETUMWA KUUA LISU ASINGEPONA, KWA HYO KUMBE WATU WA SERIKALI HUWA WANATUMWA KTK MISHENI ZA KUUA? EBU TUPE MIFANO

MWSHO, HATMA YA ROHO YA BNADAMU ANAIJUA MUNGU, HATA DR. ULIMBOKA ALISEMA WALIOMTESA WALIJIHAKIKISHIA AMEKUFA LAKN AKAWA HAI.

MUNGU NDYE KASHKILIA UHAI WA MTU NA NDIYO MAANA WEWE UNAWEZA PGWA RISAS YA TUMBO UKAFA MWINGNE AKAPONA.
 
Uongo gani ambao Yericko kausema au kusema kuna tofauti kati ya National na State Intelligence, na mbona unayemsifia kazunguka mlemle alimopita Yericko.
tofauti ya msingi ni kuviweka hivyo vikosi katika category ya 'vizivyo kisheria'. mathalan Kidon ipo kisheria, Soma kitabu cha By way of deception au Gideon spies utajua kuhusu Mossad na matawi yake.
 
Kuna bwana mmoja ni mkimbizi anaishi ughaibuni, naamini atachangia huko mbeleni, yeye amejipa umiliki wa mambo ya aina hii, hivyo hata siku moja hawezi kukubaliana na alichoandika mwingine, atakipinga na kuja na majibu yaleyale ya aliyempinga lakini atazunguka weeee mpaka mwisho anarudi palepale....


Anyway, bwana Kulikoni Ughaibuni, maprofesa wanaposoma tasnifu za wafunzwa wao huzingatia mambo mawili tu, nayo huitwa "dhanna" na "mantiki". Kama mwanafunzi ataweza kushawishi jopo la maprofesa hawa katika mambo hayo mawili basi huyo hujihesabu kuwa ni mzamivu.

Yasome maandishi yako kisha chambua dhanna na mantiki ya andiko langu, kwahakika ungeikosa sifa ya uzamivu.

Wewe ni msomi na ninafahamu umepata Phd hapo ya siasa, kibaya zaidi kwenye andiko langu umeachana kabisa na matumizi ya uwanda wako na kujivika hasira za mkizi...


Shukrani sana kwa mchango wako mkuu, mpaka tarehe 15 mwezi huu nitamaliza kusoma kitabu cha Shushushu kilichoandikwa na kada mtiifu wa ccm aitwaye Evarist Chahali. Ni kizuri japo kina makosa ya kimantiki na kidhanna.
 
tofauti ya msingi ni kuviweka hivyo vikosi katika category ya 'vizivyo kisheria'. mathalan Kidon ipo kisheria, Soma kitabu cha By way of deception au Gideon spies utajua kuhusu Mossad na matawi yake.
Kuna hitajika tafsiri mpya ya kiswahili ili kukubaliana na hoja, kusema kisicho cha kisheria hakuna maana kwamba anayekiongoza hayupo kisheria...

Mfano Idara ya Usalama Tanzania (TISS) tangu baada na kabla ya Uhuru haikuwa kisheria, lakini ilifanya kazi zote kama idara ya ujasusi tu. Miaka yote ilikuwa ni kitengo ndani ya Jeshi la Polisi ikiitwa Tawi Maalumu (Special Branch SB) mpaka Mzee Mkapa alipokuja kuiweka kisheria na kuiita Tanzania Intelligence and Security Service (TISS).

Sasa watu kama akina Chahali ukiwambia TISS iliendesha shughuli zake in black space yaani kiharamu, watakukatalia na kukuletea maandishi mareeeefu na milinks ya Google kujihalalishia kile wakisemacho....
 

Surprise me na kitu kipya, Bwana Yericko. Mie sintochoka kukurekebisha kila utapowalisha watu matango pori, na hata ukikimbilia kwenye kashfa au matusi, hayatozidi yale uliyotoa dhidi yangu wakati wa kampeni za mwaka 2015.

Mie japo sijasoma kitabu ukichoandika, siwezi kufanya utoto kama wako kukikebehi. Afterall, sikuandika kitabu changu kwa minajili ya kusaka sifa au kuwathibitishia watu kitu flani bali ulikuwa mchango wangu katika body of knowledge.

Kuna kijana mmoja alijipa uhuru kama wako kule Facebook. Nikamsihi kistaarabu kuwa hoja hujibiwa na hoja na si kebehi au matusi dhidi ya mtoa hoja...mie yangu macho! [emoji4]
 
Hakuna ulichosahihisha ndugu, nilichofanya nimekurejesha kwenye mstari uache kijicho na ujenge hoja za kisomi tu.......

Kwani wewe ndio yule Chahali mwandishi wa kitabu cha Shushushu? Basi tumia jina lako halisi ili tujadiliana kwa hekima na taadhima....

Kubwa zaidi Yericko hajawahi kukutukana kama unavyojitanabaisha... Kama siasa za maji taka huziwezi nakuasa usirudie tena kukaa kwenye ulingo wa siasa katika chaguzi zingine zijazo 2020, siasa ni kuchafuka hasaaa na kama una moyo wa nailoni kama wako utaungua tu....

Hahahaaa ati vijineno na vijembe vya uchaguzi 2015 bado umevikumbatia moyoni... Rudi bongo uishi tukufundishe aina ya siasa ngumu sio hizo za kwenye makaratasi hapo Uskochi...
 
Sioni tofauti kubwa ya alichoandika Yericko na alichoandika wewe, hakuna uongo bali ulichofanya ni kuliboresha andiko la Yericko au tuseme umejazia nyama kwa sababu alimopita Yericko nawewe ndimo ulimopitia.
Soma vizuri alichokiandika Yeriko ,yeriko kapotosha kuhusu hizo taasisi kuanzia muundo na namna zibavyotekeleza majukumu yake
 
Kukubali makosa sio dhambi ,maelezo uliyotoa kuhusu hizo taasisi hayakua sawa ,et inaweza kuwa na watu watano tu na wanaweza kuwa ndugu au rafiki wa kiongozi .Yeriko kwenye hilo bandiko hukuwa sahihi
 

taasis kutokuwepo kisheria maana yake haitambuliwi na sheria yoyote au haijawa attached kwenye taasis inayotambuliwa kisheria. Lakini administratively zinaundwa taasis ndani ya taasis like hzo SAD na KIDON.

Chukua mf afrika kusini wakati wa Mbeki alikua na 'baraza la mawaziri' lisilo rasmi. Hili liliundwa na watu mashuhuri na madon wa S.A na walikua na maamuz ambayo serikali iliyatekeleza.
 
Uongo gani ambao Yericko kausema au kusema kuna tofauti kati ya National na State Intelligence, na mbona unayemsifia kazunguka mlemle alimopita Yericko.
Hapo sasa!
 
Leo kuna ubatizo wa majasusi stay tuned.
 


Bila katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi hakuna jambo lolote la maana unaweza kuongea likapata mashiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…