kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
National Interest: Marekani itashindwa na China katika vita juu ya mgogoro wa Taiwan
Jarida la National Interest limewanukuu maafisa wa zamani na wa sasa wa masuala ya ulinzi nchini Marekani wakitahadharisha kwamba, Washington itashindwa na Beijing iwapo kutatokea vita juu ya eneo la Taiwan.
Mivutano baina ya Marekani na China kuhusu kisiwa cha Taiwan ambao ulichochewa na rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump kwa kutuma meli za kivita katika mlango bahari wa Taiwain na kuiuzia silaha seriikali ya kisiwa hicho, umepamba moto zaidi katika kipindi cha sasa cha utawala wa Rais Joe Biden baada ya kiongozi huyo kuahidi kwamba, atailinda Taiwan iwapo itashambuliwa na China.
Graham Allison ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Harvard ameandika katika jarida la National Interest kwamba uchambuzi wa maafisa wa ulinzi wa zamani na wa sasa nchini Marekani umetahadharisha kuwa, nchi hiyo inapaswa kukubaliana na ukweli wa mambo kwamba si nguvu kubwa tena ya kijeshi katika eneo la Magharibi mwa Oceania.
Allison ameashiria uchambuuzi na tathmini za karibuni za maafisa wa sasa na wa zamani wa ngazi za juu wa Marekani kama mkuu wa zamani wa majeshi ya Marekani, James Winfeld na mkurugenzi wa zamani wa shirika la ujasusi la CIA, Michael Morel juu ya uwezekano wa kutokea vita juu ya kisiwa cha Taiwan ambao wamesisitiza kuwa, jeshi la China linaweza kuchukua hatua dhidi ya Taiwan wakati wowote.