Wala si ajabu ina sababu zake na hasa wakati wa utawala wa Nduli. Wale askari wake walikuwa wanajua kiswahili sasa zile henya henya za kama " fungua mlango", "toka", "k*** nyoko", "kuja hapa" ziliwafanya siyo tu kuuchukia utawala wa Nduli mpaka na kiswahili. Hiki kiswahili kilidharaulika na kuonekana lugha ya watu ambao hawajaenda shule na si ajabu ukakuta kiswahili kinatumika sana sehemu za masoko na zingine zinazofanana na hiyo. Kukabalika kwake itachukua muda na hasa kwa generation inayokua sasa hivi na ijayo lakini siyo ile iliyoshuhudia unyama wa Nduli.