National language ya Uganda ni ipi?

National language ya Uganda ni ipi?

Yeah kweli. Chakushangaza waganda japo wanaongea kiswahili ukweli baadhi ya watu wanakichukia mno!
 
Wala si ajabu ina sababu zake na hasa wakati wa utawala wa Nduli. Wale askari wake walikuwa wanajua kiswahili sasa zile henya henya za kama " fungua mlango", "toka", "k*** nyoko", "kuja hapa" ziliwafanya siyo tu kuuchukia utawala wa Nduli mpaka na kiswahili. Hiki kiswahili kilidharaulika na kuonekana lugha ya watu ambao hawajaenda shule na si ajabu ukakuta kiswahili kinatumika sana sehemu za masoko na zingine zinazofanana na hiyo. Kukabalika kwake itachukua muda na hasa kwa generation inayokua sasa hivi na ijayo lakini siyo ile iliyoshuhudia unyama wa Nduli.
 
Official language ndo English and Luganda but national language ni Kiswahili and English!!
 
yaonekana wengi mnatumia kuhisia tu, ukweli ni kuwa Lugha ya Taifa ni ENGLISH na Lugha ya biashara ni LUGANDA, Huo ni ukweli
 
Wala si ajabu ina sababu zake na hasa wakati wa utawala wa Nduli. Wale askari wake walikuwa wanajua kiswahili sasa zile henya henya za kama " fungua mlango", "toka", "k*** nyoko", "kuja hapa" ziliwafanya siyo tu kuuchukia utawala wa Nduli mpaka na kiswahili. Hiki kiswahili kilidharaulika na kuonekana lugha ya watu ambao hawajaenda shule na si ajabu ukakuta kiswahili kinatumika sana sehemu za masoko na zingine zinazofanana na hiyo. Kukabalika kwake itachukua muda na hasa kwa generation inayokua sasa hivi na ijayo lakini siyo ile iliyoshuhudia unyama wa Nduli.
Haswa kabisa. Nimesikia hii stori toka waganda wengi.
 
Lugha yanayotumia bungeni ndio lugha ya Taifa
 
Hili ni sio uganda yote , ni kutoka baadhi tu ya maeneo, kwa mfano maeneo ya central uganda(Buganda region) hii ndo eneo ukiongea kiswahili wengi wanafikilia either wewe ni mwanajeshi au sio laia, ila ukienda maeneo ya north and west nile mbona wanatumia sana kiswahli
 
Lugha rasmi ni English. Luganda inazungumzwa tu central lkn si rasmi.
Ofisi zote za serikali lugha ni english

Lakini bado hawaijui hiyo english yenyewe, nimefika ndani ndani kuna sehemu inaitwa Mbale, huko bila lugha ya huko hakuelewi mtu, Kiingereza hakuna anayeongea, kwa kifupi nchi ambayo inaweza kuiita Taifa hapa Afrika (Kusini mwa Sahara) ni sisi tu na TanZania yetu, wengine wote ni makundi tu ya watu wanaojaribu kuishi pamoja lkn wala hawawezi kuwasiliana kwa maana hawana lugha ya Taifa au wanayo lkn hawawezi kuitumia!
 
Official language ni Kingereza.

Niliwahi kumsikia M7 akisema anataka Taifa la Uganda lijifunze kuzungumza kiswahili ili baadae kitumike kama lugha ya Taifa, sina shaka kabila la Kiganda aliwezi kukubaliana na pendekezo hilo ni wabishi sana.

Kinacho shangaza zaidi utakuta karibu makabila yote ya Uganda wanajua kuzungumza Luganda, hata M7 yuko fluent kwa lugha ya Luganda ingawa yeye ni Munyankole!
 
Wakubali tu kiswahili kitawasaidia kuondoa matabaka huko kwao na kwa intergrated vizuri in east africa
 
Back
Top Bottom