100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 4,766
- 16,191
1940 May ulitokea mvutano mkubwa wa baraza la mawaziri nchini Uingereza baina ya pande mbili, upande mmoja ilikuwa wakiunga mkono kuongea amani na Germany na upande mmoja waliunga mkono kuendelea na vita.
Waziri mkuu wa kipindi hicho Bw Winston Churchill ndiye alikuwa akiongoza ule upande unaunga mkono kuendelea na vita dhidi ya Germany, huku ule upande mmoja wa waliokuwa wanaunga mkono kuongea mazungumzo ya amani na Germany ulikuwa ukiongozwa na Bw Lord Halif ambae alikuwa ni waziri wa mambo ya kigeni.
Ulikuwa ni mvutano wa kukata na shoka, mvutano ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ni kama waliingia katika ugomvi huku upande wa Bw Lord Hafix ambao walipendelea kufanya mazungumzo na Hitler walitishia kuondoa uongozi wa Winston Churchill kuwa waziri mkuu.
Mvutano huu ni baada ya viongozi hao kufahamu nguvu aliyokuwa nayo Germany ilkuwa si mchezo, hivyo wasingeweza kukabiliana na Germany, hii ilidhihirika baada ya jeshi la Uingereza na France kuzungukwa na jeshi la Germany katika fukwe na bandari ya Dunkirk ambapo jeshi la Uingereza walifika France kwa ajili ya kuisaidia France dhidi ya uvamizi wa Germany.
Askari wa Belgium, France na British walikuwa wamezungukwa pande zote na jeshi la Germany hapo fukwe na bandari za Dunkirk na sehemu pekee ya kutokea ilikuwa ni kuvuka bahari ya Atlantic kuelekea uingereza kupitia english channel.
Ndipo hapo ilifanyika operation dynamo wakiokolewa askari zaidi ya 338,000, wananchi wa Uingereza walijitolea kwenda kuokoa askari hao. Kuanzia wavuvi waliokuwa na mitumbwi, matajiri waliokuwa na yatchs na meli, watu binafsi, mashirika, meli za kivita n.k walijitoa kwenda kuokoa askari hao, tukio hilo hadi leo linafahamika kama maajabu ya Dunkirk, askari walikuwa wamekata tamaa wakisubiri muda ufike jeshi la Hitler kufika na kuwamaliza kikatili.
Kwa tukio hilo la Dunkirk lilipelekea kwa shemu kubwa baraza hilo kuvutana wakiona hawana uwezo kupambana na Germany.
Bw Lord Halifax ambae alikuwa kiongozi mpingaji wa maamuzi ya Winston Churchill kuhusu kukabiliana na vita na Germany endapo akiivamia Uingereza alipendekeza ni vyema amtumie rafiki wa karibu wa Hitler dictator Mussolini kufanya majadiliano na mazungumzo ya amani kutoingia vitani, hapo ndipo kuna ule msemo maarufu wa Winston ulichukua nafasi yake "Huwezi kujadiliana na tiger wakati kichwa chako kiko kinywani mwake".
Baada ya mvutano wa siku kadhaa walikubaliana maamuzi wanaingia vitani na Germany huku Bw Halifax akikubali mawazo ya Winston.
Kinachoendelea Ukraine ni kama inatukumbusha tukio hilo, nchi za NATO zipo katika mvutano mkubwa wakijadili wafanye nini kuikoa Ukraine toka mikononi mwa Russia, imedhihirika Ukraine hivi sasa licha ya kupewa pesa, kusaidiwa askari, silaha za kila aina ambazo ni superior kutoka west, air defenses, satellite n.k lakini bado game limekuwa gumu sana upande wa NATO.
Ukraine imepoteza pakubwa sana kuliko.
- Askari wa Ukraine wale walio na mafunzo ya hali ya juu, special forces wamekwenda na maji, wamepotezwa vitani kitu kinachoilazimu Ukraine ianze kutumia wananchi wasio na mafunzo, walevi mtaani, mateja, wazee na wagonjwa ndio wanapelekwa front tena kwa ulazima. Hii ni dalili mbaya sana, kama commandos wamelamba mchanga je hawa afya mgogoro wanaweza kukabiliana na jeshi la Russia?
- Vita hii imepoteza vijana wengi sana wadogo wenye nguvu ambao ndio wanategemewa na taifa la Uraine kama nguvu kazi, hii inaonyesha kwamba Ukraine itashuka sana kimapato, kwa sababu ndilo kundi linaloongoza kama walipa kodi wazuri, ina maana pato la taifa litapungua sehemu kubwa sana.
- Vifaa vya kivita, miundo mbinu, viwanda n.k vimeharibiwa sana kufikia point haiwezekani kwa marekebisho, hii itachukua muda mrefu sana kuja kurudisha vitu hivyo, hii ni hasara kubwa.
- Idadi ya watu kwa ujumla imeshuka tokana na madhara ya kivita.
Ndio maana hadi sasa tumeanza kuona viongozi kutoka nchi za NATO wakianza kutumia kuauli kwamba Ukraine ina haki kupiga ndani ya Russia ikitumia silaha zao, huku Russia ikijibu wasithubutu, tumeshuhudia pia Russia kutishia kutumia silaha za nuclear endapo tuusalama wake utakuwa matatani.
Pia tunazidi kusikia nchi za NATO zikidai kutuma vikosi vyao nchini Ukraine kukabiliana na Russia. Hii inaashiria kitu kimoja kwamba msaada wa silaha, pesa na vifaa hauna nafasi tena kuikoa Ukraine.
France imetangaza kupeleka askari wake Ukraine, tukumbuke pia France ndio wa kwanza kwenda kuiokoa Poland dhidi ya Germany WWII, kitu kilichopelekea France kupelekewa moto hadi Paris na Uingereza ilipoingia kati wakapelekewa moto hadi fukwe za Dunkirk walipotorokea na kutokomea kwa ngalawa kurudi nyumbani wakiwa hawaamini kama wamepona na kuiacha Germany ikiitawala France.
Lakini pia tukumbuke Russia ndio walimpelekea moto Germany kutoka mashariki hadi Berlin, huku West akiwepo USA, FRance na England wakiwa wanamkuta Russia tayari amefika ikulu Berlin.
Hii mistake ni kama France anairudia, kumbe history zinajirudia.
Je? Russia itakubali kupigwa mikwara kuacha kuendelea na mipango yake kuitandika Ukraine na kuweka kibaraka wake?
NATO watakubali kuona Ukraine walioishawishi iingie vitani na Russia ikichukuliwa na Russia huku wasifanye lolote?
NATO watakubali kudharaulika na kumponza kibaraka wao Zelensky ambae walimuahidi kuishinda Russia?
Kwa maana Russia ikiacha NATO kushinda hii vita ni kuiruhusu Ukraine kuingia kwenye muungano na NATO, na hili litatokea haraka sana, Je Russia itakubali NATO kukaa karibu na mipaka yake?
Maswali ni mengi. Na situation inaogofya. Tusubiri.