NATO ipo katika wakati mgumu sana kuikoa Ukraine

NATO ipo katika wakati mgumu sana kuikoa Ukraine

USSR iliamua kuwa ally na Germany baada ya kuona west wanamkataa, akaamua kusaini huo mkataba Molotov–Ribbentrop Pact ya kwamba wasivamiane kijeshi. Alitumia akili, lakini Hitler alipoavunja makubaliano ilibidi aingie nae vitani kumbuka kwamba USSR hawakutaka vita na Germany, walifahamu jeshi la Germany lina nguvu kiasi gani, hata USA hakuingia vitani mpaka pale ally wa Germany ambae ni Japan alipoivamia Pearl Harbor.
USSR iliamua kuingia makubaliano na Nazi Germany kwa sababu kuu mbili:

Mosi: Kuepusha vita ya karibu ya moja kwa moja na Nazi Germany.

Pili: Kuongeza mipaka (territorial gains) ili kujenga buffer zone ya kukabiliana na uvamizi wa baadaye kutokea magharibi mwa mipaka ya USSR. Ukitaka kujua hilo angalia jinsi ambavyo makubaliano yao yalivyokuwa yakitekelezwa mwanzoni.

Kiufupi ni kwamba, USSR ilikuwa tayari kukubaliana na kujitanua kwa Hitler upande mmoja (western/central Europe) huku Soviet Union na yenyewe ikijitanua upande mwingine (eastern Europe) bila upande mmojawapo kuingilia upande wa mwenzake, kitu ambacho "the West" ya wakati huo haikukubaliana nacho.
 
Dah basi tumesoma vitabu tofauti kwa maana west walimtenga USSR kwa sababu moja kuu, sera za kijamaa, huko kujiongezea mipaka nadhani itakua ziada.

Elewa pia Stalin alikuwa anafahamu fika Hitler si mtu wa kuamini, hivyo alikwenda kuomba kusaini mkataba wa Molotov-Ribbentrop Pact akiwa na nia ya kununua muda kujijenga kijeshi, alimfahamu vyema Hitler, rejea Hitler alipovunja makubaliano ya Munich, soma Munich Agreement.

Hitler pia alivunja Anglo-German Naval Agreement na Chamberlain 1935, akavunja 1939.

Stalin hakuwa mjinga, licha ya makubaliano apewe sehemu Czech baadae akasem anaitaka na Poland ndipo France kujikuta Super power kuingili vita kutandikwa hadi aibu.
Mara ya mwisho katika pitapita zangu, USSR ilikuwa nchi ya kikomunisti na sio ya kijamaa. Ingawa yote mawili yamekuwa yakitumika [interchangeably].

Hata hivyo, kutofautiana kwa ideologies kati ya USSR na West hakukuzuia mazungumzo au maelewano kati ya pande mbili kabla ya WW2. Kilichokwamisha maelewano ama makubaliano ya ulinzi wa pamoja (collective-security agreements) ni masharti ambayo kila upande ungepaswa kuyatekeleza (terms of agreement).

Sio sahihi kusema kwamba USSR ilitengwa na West kwenye issue ya kumkabili Hitler, bali kulikuwa na maslahi zaidi kwa Stalin kuingia makubaliano na Nazi Germany ambayo ilionesha kuendana ama kukubaliana na sera ya kujihami ya USSR (expansion) kuliko kuunda muungano wa kiulinzi na West ambayo ilishaonesha kutokukubaliana na sharti hilo.
 
Hii habari yako ni ya kuunga unga sana. Unasema Ukraine kapoteza wakati unakumbuka Kyiv ilizungukwa na jeshi la Urusi ila sasa vita vipo mpakani. Askari wengi wa Ukraine wamefariki kama walivyofariki wa Urusi. Urusi ni kubwa kwa Ukraine na sio rahisi Ukraine kushinda. Njia ya vita kuisha ni askari wa Urusi kufariki kwa winging zaidi, ikijumuisha mamluki wa India, Nepal na nchi za Central Asia.
Russia haikutaka kuipiga Ukraine itoke vipande vipande, Russia walirudi nyuma makusidi, lakini wangetaka watie ngumu hata Zelensky angekuwa marehemu hivi sasa.
Russia anaipiga Ukraine gentle, sio kama wale walevi wanaoipiga Gaza zigzag wakiua maelfu ya raia wakiwemo watoto wadogo hadi wanashtakiwa mahakama ya kimataifa kwa uhalifu wa kivita.

Russia akiamua kuipiga Ukraine iwe jivu haishindikani.
 
Sasa mbona ruhusa ya iwapo washambulie ndani ya Urusi inatakiwa kutoka kwa nato.
Ukraine imekuwa ikishambulia viwanda vya kusafisha mafuta ndani ya Urusi hata kabla ya ruhusa kutoka nchi au taasisi yoyote.

Sharti la kutoshambulia ndani ya Urusi linaweza kuwekwa na nchi zinazoipa silaha Ukraine. Hilo sharti halipo kabisa kwa silaha ambazo Ukraine imeunda yenyewe.
 
Kuna mjadala mpya nimeuibua mimi mwenyewe kuhusiana na USSR kuwa nchi ya kikomunisti ama kijamaa.

Wapo wanaosema kuwa USSR ilifuata itikadi mojawapo ama zote mbili na wapo pia wanaosema USSR haikuwahi kuwa mojawapo ama vyote viwili, bali ilikuwa kitu kingine tofauti kabisa (state-capitalist). Hivyo ni suala la muktadha zaidi.
 
Mkuu upo vizuri
Wengi history ya vita ya kwanza na ya pili wanalishwa Matango pori na west.
West kwenye propaganda wapo vizuri hata ukifuatilia hii vita ya Ukrein wanaongopa bila aibu.
Mwanaume Rusia yeye anatwanga tu kimyakimya.
Mara ooh hana silaha. Mara hana uchumi. Yeye ni mwendo wa kugonga tu
Ukichagua kutotaka kuamini hicho unachokiita "matango pori" unaweza kujikuta unaungana na wale denialists wanaosema kwamba hizo vita kubwa mbili hazikuwahi kutokea kabisa bali ni stori za kutunga tu.
 
Mara ya mwisho katika pitapita zangu, USSR ilikuwa nchi ya kikomunisti na sio ya kijamaa. Ingawa yote mawili yamekuwa yakitumika [interchangeably].

Hata hivyo, kutofautiana kwa ideologies kati ya USSR na West hakukuzuia mazungumzo au maelewano kati ya pande mbili kabla ya WW2. Kilichokwamisha maelewano ama makubaliano ya ulinzi wa pamoja (collective-security agreements) ni masharti ambayo kila upande ungepaswa kuyatekeleza (terms of agreement).

Sio sahihi kusema kwamba USSR ilitengwa na West kwenye issue ya kumkabili Hitler, bali kulikuwa na maslahi zaidi kwa Stalin kuingia makubaliano na Nazi Germany ambayo ilionesha kuendana ama kukubaliana na sera ya kujihami ya USSR (expansion) kuliko kuunda muungano wa kiulinzi na West ambayo ilishaonesha kutokukubaliana na sharti hilo.
Nimekueleza vyema tu unaweza kupitia machapisho mengi mtandaoni,

Huyu jamaa ameelezea kama nilivyoelezea hadi nimeshangaa ni mwanahistoria wa kirusi anaelezea kama nilivyokuelezea hapo, sababu ya west kumtenga Stalin, nimekuelezea pia Stalin alitambua Hitler atamgeuka muda wowote, hivyo alikua akinunua muda tu.

Screenshot 2024-06-06 101606.png

Nimesoma kitabu muda kidogo nyuma.
 
USSR iliamua kuingia makubaliano na Nazi Germany kwa sababu kuu mbili:

Mosi: Kuepusha vita ya karibu ya moja kwa moja na Nazi Germany.

Pili: Kuongeza mipaka (territorial gains) ili kujenga buffer zone ya kukabiliana na uvamizi wa baadaye kutokea magharibi mwa mipaka ya USSR. Ukitaka kujua hilo angalia jinsi ambavyo makubaliano yao yalivyokuwa yakitekelezwa mwanzoni.

Kiufupi ni kwamba, USSR ilikuwa tayari kukubaliana na kujitanua kwa Hitler upande mmoja (western/central Europe) huku Soviet Union na yenyewe ikijitanua upande mwingine (eastern Europe) bila upande mmojawapo kuingilia upande wa mwenzake, kitu ambacho "the West" ya wakati huo haikukubaliana nacho.
Sasa the west mbona wao walimuuza czechslovakia, kwenye makubaliano ya Munich, Huyo Britain na France walikubaliana na Hitler kwamba achukue eneo la Czech liitwlao Sudetenland kwa makubaliano ya kwamba Germany isiendelee kujitanua, kumbuka hapo Germany walishaichukua Austria.
Ulikuwa ni usaliti, ukweli ni kwamba Czech alikuwa ni mbuzi wa kafara, kwanza eneo la Sudetenland ndipo ambapo kulikuwa ni ngome ya muhimu kujizuia dhidi ya uvamizi.

Siku Hitler alipofika Czech kuichukua Czech, Czech ikidhani France na Britain wangempa msaada matokeo yake wakamshauri amwachie Hitler eneo kwani wao hawawezi ingia vitani kumsaidia, ikabidi Czech akubali.
Matokeo yake Hitler akachukua na maeneo yaliyobaki ya Czech.

Hakuna nchi ilikuwa tayari kuanza vita na Germany, hata USSR kuweka makubaliano na Hitler ya kutovamiana kijeshi hapaswi kulaumiwa kwani hata west walimuuza Czech kama mbuzi ya kafara ili kumpooza Hitler.

Bora hata USSR aliwaomba kuungana kumkabili Hitler mapema. Stalin alikua smart sana, isitoshe alikua na makachero hadi USA na Germany.
 
Nimekueleza vyema tu unaweza kupitia machapisho mengi mtandaoni,

Huyu jamaa ameelezea kama nilivyoelezea hadi nimeshangaa ni mwanahistoria wa kirusi anaelezea kama nilivyokuelezea hapo, sababu ya west kumtenga Stalin, nimekuelezea pia Stalin alitambua Hitler atamgeuka muda wowote, hivyo alikua akinunua muda tu.

View attachment 3010680

Nimesoma kitabu muda kidogo nyuma.
Tatizo ni kuwa, huyo mchambuzi ametaja tu "Communism" bila kueleza muktadha au namna ambavyo huo Ukomunisti wa USSR ulikwamisha au ulichelewesha mchakato wa ushirika kati ya USSR na Britain/France kabla ya Operation Barbarossa.

Again, Ukomunisti wa USSR haukuzuia engagements za mazungumzo kati ya USSR na Britain/France ili kuunda ushirika dhidi ya Hitler bali kilichokwamisha mchakato ni kutokukubaliana kwenye masuala mengi ya msingi ikiwemo sera na mikakati ya kijeshi.

Baada ya Hitler kuivamia USSR na uhusiano wao kuvunjika, ndipo USSR ilipokuwa na mkakati wa wazi kuhusu Hitler ambao ulitengeneza msingi wa pamoja (common ground) wa makubaliano ya ushirika kati ya USSR na West kufikiwa.
 
Sasa the west mbona wao walimuuza czechslovakia, kwenye makubaliano ya Munich, Huyo Britain na France walikubaliana na Hitler kwamba achukue eneo la Czech liitwlao Sudetenland kwa makubaliano ya kwamba Germany isiendelee kujitanua, kumbuka hapo Germany walishaichukua Austria.
Ulikuwa ni usaliti, ukweli ni kwamba Czech alikuwa ni mbuzi wa kafara, kwanza eneo la Sudetenland ndipo ambapo kulikuwa ni ngome ya muhimu kujizuia dhidi ya uvamizi.

Siku Hitler alipofika Czech kuichukua Czech, Czech ikidhani France na Britain wangempa msaada matokeo yake wakamshauri amwachie Hitler eneo kwani wao hawawezi ingia vitani kumsaidia, ikabidi Czech akubali.
Matokeo yake Hitler akachukua na maeneo yaliyobaki ya Czech.

Hakuna nchi ilikuwa tayari kuanza vita na Germany, hata USSR kuweka makubaliano na Hitler ya kutovamiana kijeshi hapaswi kulaumiwa kwani hata west walimuuza Czech kama mbuzi ya kafara ili kumpooza Hitler.

Bora hata USSR aliwaomba kuungana kumkabili Hitler mapema. Stalin alikua smart sana, isitoshe alikua na makachero hadi USA na Germany.
Moja ya makubaliano ya kipuuzi kuwahi kufanyika katika karne ya 20 ni hayo ya Munich a.k.a. Munich Agreement ya kina Neville Chamberlain (waziri mkuu wa zamani wa Uingereza).

Nimewahi kukosoa mara kadhaa humu kuhusiana na hilo. Na nimekuwa nikitumia huo mfano kupingana na wale wanaojaribu kuishinikiza Ukraine iingie kwenye makubaliano ya kuachia maeneo yake kwa Urusi ili kumaliza vita inayoendelea hivi sasa.

Miongoni mwa michango yangu humu jukwaani ni huu hapa:

Pamoja na hilo, hizo agreements mbili hazifanani. Makubaliano ya Munich yalikuwa na lengo la kuishawishi Nazi Germany imalizie vita yake Sudetenland na sio kuendeleza expansion upande mwingine. Terms za makubaliano kati ya Nazi Germany na USSR zilikuwa tofauti kabisa na zilihusisha expansionists wawili mezani.
 
Ukichagua kutotaka kuamini hicho unachokiita "matango pori" unaweza kujikuta unaungana na wale denialists wanaosema kwamba hizo vita kubwa mbili hazikuwahi kutokea kabisa bali ni stori za kutunga tu.
Ktk dunia hii iliyojaa uongo usipende kuamini amini hata kama ndivyo ulivyofundishwa na kukupa marks darasani.
Tafuta ukweli pande zote.
Mengi ya unayofundishwa ni ili kuku shape uwe vile wao wanavyotaka.
 
Sasa mbona ruhusa ya iwapo washambulie ndani ya Urusi inatakiwa kutoka kwa nato.
Kwa sababu wao ndio wenye kuamua silaha zao zitumike wapi maana wao ndio watoaji
 
Kuna mjadala mpya nimeuibua mimi mwenyewe kuhusiana na USSR kuwa nchi ya kikomunisti ama kijamaa.

Wapo wanaosema kuwa USSR ilifuata itikadi mojawapo ama zote mbili na wapo pia wanaosema USSR haikuwahi kuwa mojawapo ama vyote viwili, bali ilikuwa kitu kingine tofauti kabisa (state-capitalist). Hivyo ni suala la muktadha zaidi.
Usoshalisti na ukomunisti ni itikadi mbili za kisiasa na kiuchumi ambazo zina mfanano mwingi, lakini pia zina tofauti muhimu.

Usoshalisti (Socialism):
1. Umiliki wa Rasilimali: Serikali au jamii kwa ujumla inamiliki na kudhibiti rasilimali muhimu na njia za uzalishaji (kama viwanda, ardhi, na mitambo).
2. Usambazaji wa Mali: Lengo ni kuhakikisha usambazaji wa haki wa mali na huduma, kupunguza tofauti kubwa kati ya matajiri na maskini.
3. Soko: Inaweza kujumuisha vipengele vya soko huria, lakini serikali ina jukumu kubwa katika kudhibiti uchumi na kusimamia usambazaji wa rasilimali.
4. Mamlaka ya Serikali: Serikali ina jukumu kubwa katika kupanga uchumi na kutoa huduma za kijamii kama vile afya, elimu, na ustawi wa jamii.

Ukomunisti (Communism):
1. Umiliki wa Kijamii: Vyombo vyote vya uzalishaji vinamilikiwa kwa pamoja na jamii nzima, mara nyingi bila umiliki binafsi kabisa.
2. Usambazaji wa Kulingana na Mahitaji: Bidhaa na huduma zinasambazwa kwa msingi wa mahitaji ya kila mtu, kwa lengo la kufanikisha usawa kamili wa kijamii.
3. Soko: Hakuna soko huria; badala yake, uchumi unadhibitiwa kikamilifu na serikali, ambayo inapanga uzalishaji na usambazaji.
4. Mamlaka ya Serikali: Katika nadharia, serikali inapaswa kutoweka baada ya kipindi cha mpito ambapo nguvu za kidikteta za wafanyakazi zimeshika hatamu, na jamii ya ukomunisti safi inafanikishwa ambapo kila mtu hufanya kazi kwa ajili ya manufaa ya wote.

Tofauti Muhimu:
- Umiliki: Usoshalisti unaweza kuruhusu umiliki binafsi kwa kiwango fulani, lakini ukomunisti unakataa umiliki binafsi kabisa.

  • Soko: Usoshalisti unaruhusu uwepo wa soko la mipango au hata mchanganyiko wa soko huria na mipango ya serikali, wakati ukomunisti hupinga kabisa uwepo wa soko huria.
  • Lengo la Mwisho: Usoshalisti mara nyingi hulenga kupunguza tofauti za kijamii na kiuchumi kupitia mipango ya serikali, wakati ukomunisti unalenga kuunda jamii isiyo na madaraja, ambapo serikali yenyewe itafutwa mwishowe.

Kwa ujumla, usoshalisti ni hatua kuelekea ukomunisti, lakini kwa vitendo, mataifa mengi yamekuwa yakitumia mifumo ya kiuchumi ambayo ni mchanganyiko wa vipengele vya kijamaa na vya kibepari. (Kwa msaada wa Chatgp)....

USSR (Union of Soviet Socialist Republics) ilikuwa inajiita nchi ya kisoshalisti, lakini kwa vitendo ililenga kufikia ukomunisti.

Usoshalisti katika USSR:
1. Umiliki wa Serikali: Serikali ya USSR ilimiliki karibu rasilimali zote na njia za uzalishaji kama viwanda, ardhi, na vyombo vya usafiri. Hakukuwa na umiliki binafsi wa mali kubwa za uzalishaji.
2. Mipango ya Uchumi: Uchumi wa USSR uliongozwa na mipango ya serikali, hususan kupitia mipango ya miaka mitano (Five-Year Plans) iliyoweka malengo ya uzalishaji kwa sekta mbalimbali.
3. Huduma za Kijamii: Serikali ilitoa huduma za kijamii kama afya, elimu, na ajira kwa raia wote, ikiwa na lengo la kusawazisha tofauti za kijamii na kiuchumi.

Lengo la Ukomunisti:
1. Hatua ya Mpito: USSR ilijiona kama taifa lililoko kwenye hatua ya mpito kuelekea ukomunisti. Katika nadharia za Kikomunisti, matumizi ya nguvu za serikali yalihitajika ili kuondoa athari za mifumo ya kibepari na kujenga jamii yenye usawa.
2. Dikteta ya Wafanyakazi: Nchi hiyo iliongozwa na chama kimoja cha Kikomunisti, ambacho kilijaribu kuwakilisha matakwa ya wafanyakazi wote. Katika nadharia ya ukomunisti, hii ilikuwa ni hatua ya muda inayolenga kufikia jamii isiyo na matabaka na serikali.

Kwa hivyo, kwa kutumia nadharia na vitendo, USSR ilikuwa inatekeleza usoshalisti kwa mtazamo wa kuufikia ukomunisti. Hata hivyo, USSR haikufanikiwa kufikia jamii ya ukomunisti kamili kama ilivyobainishwa na itikadi za Marxist-Leninist. Mfumo wao ulikuwa na vipengele vya kidikteta na mipango ya kiuchumi iliyodhibitiwa kikamilifu na serikali, lakini hakukuwa na kipindi cha "kutoweka kwa serikali" ambacho ni kipengele muhimu cha ukomunisti kamili.

(Kwa hisani ya Chatgp)
 
Hata hivi sasa unaweza kusema pasipo Iran kumpatia silaha Russia basi Russia haiwezi kushinda vita.
Russia aliwaambia mapema sana west tusipoungana kumkabili Hitler itakuwa ngumu, west walimtenga na kukataa mawazo yake kisa ana sera za kijamaa, baada ya Germany kumvamia Soviet ndipo vita ikaanza kati ya Germany na Russia.

Hapo unaona kabisa USA na wenzake walishamkataa Soviet kama ally mwenzao kumkabili Germany.

Kuhusu hio lend lease programme mnufaika mkubwa alikuwa ni Great Britain, je aliishinda Germany?

Sasa hivi NATO inamsaidia Ukraine pesa na silaha za kutosha je wamemshinda Russia?

Stalin alishasema Soviet imelipa damu kwenye vita, USA imelipa pesa, GB imelipa muda, nadhani umeelewa maana yake.
Soviet asingejihusisha na hio vita USA asingeweza ishinda Germany.
USA hakuwa na mpango wa kuingilia hiyo vita
Russia alishatepeta
Uingereza alikuwa anapumulia pua
France kitaaambo alishawekwa ndani
Sema tamaa na kiherehere cha Japan akamuingiza mbabe vitani
Hitler kusikia watu wameingilia sicily kwenda kwa Mussolin ikabidi asitishe kwa muda kumbaka Russia akaelekeza nguvu upande huo maana alijua kitakachofuata

Basi Russia na red army yake wakafufuka.
Yaani Kama USA asingeingilia hii vita German alishawafinya wote hao nasikia alikuwa na staili yake hiyo unapigwa Kama radi na ghafla ardhini,angani na majini
 
Russia haikutaka kuipiga Ukraine itoke vipande vipande, Russia walirudi nyuma makusidi, lakini wangetaka watie ngumu hata Zelensky angekuwa marehemu hivi sasa.
Russia anaipiga Ukraine gentle, sio kama wale walevi wanaoipiga Gaza zigzag wakiua maelfu ya raia wakiwemo watoto wadogo hadi wanashtakiwa mahakama ya kimataifa kwa uhalifu wa kivita.

Russia akiamua kuipiga Ukraine iwe jivu haishindikani.
Unaandika kama vile vita ni Indian movie.Usichojua ni kuwa mwanzoni mwa vita Ukraine alikuwa na drone, Javelin.Urusi hakuwa na drones.Hivyo misafara ya Urusi ilikutana na drones na javelin.Urusi drone kaomba Iran .Kilichomtoa Urusi Ukraine ni kipigo sio hiari.
 
Tulia tu mkuu naona hakuna unachokijua kama mimi. Kwa akili yako unadhani Urusi anataka kiuchukua Ukraine na siyo kuidhohofisha?

Nia ya Putin siyo kuimiliki Ukraine,kuingia ama kuizunguka Kyiv ni vitisho na uthibitisho kwamba hawajafunga milango bali wameweka mapazia hivyo wawe wapole.
Hii habari yako ni ya kuunga unga sana. Unasema Ukraine kapoteza wakati unakumbuka Kyiv ilizungukwa na jeshi la Urusi ila sasa vita vipo mpakani. Askari wengi wa Ukraine wamefariki kama walivyofariki wa Urusi. Urusi ni kubwa kwa Ukraine na sio rahisi Ukraine kushinda. Njia ya vita kuisha ni askari wa Urusi kufariki kwa winging zaidi, ikijumuisha mamluki wa India, Nepal na nchi za Central Asia.
 
USA hakuwa na mpango wa kuingilia hiyo vita
Russia alishatepeta
Uingereza alikuwa anapumulia pua
France kitaaambo alishawekwa ndani
Sema tamaa na kiherehere cha Japan akamuingiza mbabe vitani
Hitler kusikia watu wameingilia sicily kwenda kwa Mussolin ikabidi asitishe kwa muda kumbaka Russia akaelekeza nguvu upande huo maana alijua kitakachofuata

Basi Russia na red army yake wakafufuka.
Yaani Kama USA asingeingilia hii vita German alishawafinya wote hao nasikia alikuwa na staili yake hiyo unapigwa Kama radi na ghafla ardhini,angani na majini
Mkuu nimetoa takwimu hapo ni upande upi askari wa hitler walikufa zaidi, ipo wazi upande wa mashariki ambapo USSR alikuwa frontline ndipo walifariki zaidi.
Ukitizama hapo USSR pekee aliwaua askari zaidi 2.7 Million hatujaweka mateka.
Front walipokuwa USA, FRance na Britain ni 339,957.

Baadae walioshirikiana kuivamia Germany kwa pamoja wakaua kama 1.2 million, sasa hapo usichoelewa nini?
 
Leta na takwimu za aliyepoteza askari wengi kati ya Russia USA na washirika wengine.😭 Natanguliza shukrani
 
Unaandika kama vile vita ni Indian movie.Usichojua ni kuwa mwanzoni mwa vita Ukraine alikuwa na drone, Javelin.Urusi hakuwa na drones.Hivyo misafara ya Urusi ilikutana na drones na javelin.Urusi drone kaomba Iran .Kilichomtoa Urusi Ukraine ni kipigo sio hiari.
We acha kuongelea Russia, unazungumzia drone watu wamerusha satellite 1957, hapo ni miaka 12 tu wametoka vitani ww2.
Rocket science ilivyo ngumu watu wanarusha satellite 1957, kabla hata US hajarusha, na USSR ndio wa kwanza kukanyaga mwezini, waheshimu hao jamaa ni tofauti na mnayodanganywa na VoA ,CNN, BBC n.k, hao ni moto wa kuotea mbali.
 
Back
Top Bottom