NATO ipo katika wakati mgumu sana kuikoa Ukraine

Hio ni kwa mtizamo wako ama unaweza kueleza hayo makubaliano?
Au pengine kwenda sawa inawezekana unachosema lakini hayo makubaliano hayakuendana na sera za kikomusti, hivyo unarudi pale pale.
 
Russia alipoteza askari wengi, ndio maana nimeeleza hapo juu, Stalin alisema Russia imetoa damu, USA katoa pesa, Britain katoa muda, unaelewa maana yake?
Anyway wewe kwa upeo wako unadhani Russia angeachwa apambane mwenyewe angemuweza Nazi germany?
Hapo mnajitekenya na kucheka wenyewe hapo kuna mtu alibadili upepo wa ile vita hamtaki tu kumkubali.
 
Sasa hapo si unaona wote dhumuni lao likiwa moja tu, kuepuka vita na Germany.
 
Anyway wewe kwa upeo wako unadhani Russia angeachwa apambane mwenyewe angemuweza Nazi germany?
Hapo mnajitekenya na kucheka wenyewe hapo kuna mtu alibadili upepo wa ile vita hamtaki tu kumkubali.
Hao askari zaidi ya 2.7 Million waliouawa na USSR na bado USSR ikawa ya kwanza kuingia Berlin unafikiri ni mchezo? yaani we ukitafakari, hawa waliokuwa nchi karibu 3 wao wakiwamaliza wanazi 339K na bado walichelewa kuingia Berlin.

Je? USSR kama iliwamaliza askari 2.7 million wa Hitler, wangeshindwa kuwamaliza hao 339K?
Na je kama askari 339K wanazi walipambana na west kuwasumbua kuingia Berlin vipi USSR isingekuwepo ikaacha hao askari 2.7 Million waingie west kupambana na the west.

Tafakari halafu unipe jibu, halafu ndipo utaelewa kwanini Russia huwa wana maadhimisho ya washindi wa ww2.
 
Soma hapa uone jinsi huyo jamaa yako bila kusaidiwa asingetoboa
 

Attachments

  • Screenshot_20240607-121305.png
    274.2 KB · Views: 3
  • Screenshot_20240607-121305.png
    274.2 KB · Views: 2
,πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ€πŸ™Œ
 
Soma hapa uone jinsi huyo jamaa yako bila kusaidiwa asingetoboa
The west wasingesaidiwa na USSR kuwatwanga wanazi hata USA isingetoboa, nimekupa statistics hapo,

Russia iliua askari 1,105,987 , waliopotea na wafungwa wa kivita 1,018,365 , majeruhi na waliougua 3,498,059.
Hapo ukijumlisha USSR peke yake ilipunguza askari zaidi ya 5 Million kwa ujumla.
Tazama west hapo juu, wameua 107,042, wafungwa na waliopotea 409,715, waliojeruhiwa vitani 516,757. Huo msaada walipewa nchi zaidi 40 hadi China, ndio maana tunapowaambia USSR alipigana vita vitakatifu uwe unaelewa mkuu.

Idadi ya hao askari waliodhibitiwa west haifiki hata robo ya askari ambao USSR iliwamaliza wanazi.
Wengi hamfahamu historia halisi ya ww2.

Hivi sasa North Korea, Iran na China wanaisaidia Russia silaha n.k kupambana na Ukraine, unataka kuniambia Russia haiwezi kusimama peke yake kuipiga Ukraine?

Na nikuulize kingine unaelewa engo la NATO kuanzishwa?

Kwa nini vita ya middle east kuanzia Syria, Iraq n.k USA iliungana na nchi washirika kama UK kwenda kupambana, je USA una maana angeshindwa vita angeenda peke yake?
 
Aisee!Hii dawa lazima jamaa ameze tu,itamponya.
 
πŸ™Œ Una phd ya ubishi kati ya USA na Russia nani alisaidiwa? Unajua ni nani alianza kuvamiwa na Nazi?
USA wakati Russia anahemea mipira yeye alikua bado na neutrality act ila aggression acts za German zikamfanya aje na lend-lease act. Na wote Uk, France ,soviet union pamoja na China walinufaika.

Sasa kati ya USA na soviet nani alitangulia vitani? Hapo ni nani alienda kurescue situation?

Mtu ambaye battle ground ilikuwa nchini kwake wakati USA alituma vikosi barani ulaya kuwasaidia allies.

Halafu nenda kasome alichofanywa Russia na wajapani. Akategea USA kaanza. Kugain specific victories over japani dakika za jioooni akajiunga kuipiga Japan
 
Mzee mbona unakuwa hunielewi, we ukipewa msaada utakataa, North Korea anamzidi nini Russia? Mbona Russia napokea contennas mamia kutoka NK zenye silaha n.k, ndio maana nikakuuliza hio ina maana Russia haiwezi Ukraine hadi msaada wa NK? Mbona swali dogo tu hilo halihitaji elimu ya rocket science kujibu?

USSR haikuomba msaada kutoka west, waliomfuata Stalin ni west wao wenyewe, kipindi hiko USSR alikuwa tayari ameshafahamu anapambana peke yake, ngoja nikuwekee screenshot hapa mtu kajibu.


Hay maelezo ukisoma utagundua Britain ndio waliifuata Russia nbaada ya kichapo kikali, Churchill kutokana na kipigo akaona waache tofauti za ukoministi na waungane kupambana na adui yao, kitu ambacho Stalin alishawafuata toka mwanzoni sana, na hapo ndipo utajua USSR ilikuwa na intel ya aina gani. Moja ya kazi intel ni kutabiri mambo ya mbele.



Unakuwa unanichosha narudia kile kile tu.
 
Sasa hapo si unaona wote dhumuni lao likiwa moja tu, kuepuka vita na Germany.
Dhumuni moja, mikakati (strategies) tofauti. Soma hiyo paragraph yangu ya mwisho nimeeleza.

Munich Agreement ilifanyika ili Nazi Germany isitishe vita. Full stop!

Molotov-Ribbentrop Pact ilikuwa na protocols za kuigawa Ulaya Mashariki katika pande mbili za kiushawishi. Na ilitekelezwa kupitia sera ya kujihami ya kujitanua (expansionism).

Wakati Stalin anafanya mazungumzo na Hitler, pia kulikuwa na mazungumzo yakiendelea upande mwingine kati ya USSR na Britain/France na yaliendelea kwa siri [kulingana na machapisho mbalimbali] hata baada ya Stalin kuingia mkataba na Hitler.

Hitler alikuwa anti-Communist. Pamoja na uhasama wake na USSR, Molotov-Ribbentrop Pact ilisainiwa. Vipi kuhusu falsafa na itikadi ya Nazi Germany? Je, ilikwamisha makubaliano ya Munich (1938)?

Utagundua kuwa suala la Ukomunisti wa USSR had nothing to do with issue ya mazungumzo kwa ujumla wake bali ni kutokukubaliana kwa hoja, masharti na mikakati ya makubaliano katika meza za mazungumzo. Soma tena vizuri kuhusu Molotov-Ribbentrop Pact na protocols zake zote, utaona kile kilichosababisha Stalin akubaliane na Hitler na sio West kwa wakati huo.
 
Hio ni kwa mtizamo wako ama unaweza kueleza hayo makubaliano?
Au pengine kwenda sawa inawezekana unachosema lakini hayo makubaliano hayakuendana na sera za kikomusti, hivyo unarudi pale pale.
Ni sera zipi hizo za kikomunisti (specifically) ambazo hazikuendana na makubaliano katika meza ya mazungumzo?

Baadhi ya wachambuzi wanaishia kusema tu "Communism" lakini hawaelezi specific jinsi ambavyo huo Ukomunisti wa USSR ulichelewesha muungano dhidi ya Hitler.
 
Hivi sasa North Korea, Iran na China wanaisaidia Russia silaha n.k kupambana na Ukraine, unataka kuniambia Russia haiwezi kusimama peke yake kuipiga Ukraine?
USSR isingeweza kusimama peke yake dhidi ya Hitler bila msaada wa allies. Hayo si maneno yangu by the way, ni maneno ya Stalin na baadaye Nikita Khrushchev, viongozi waliofuatana wa USSR.

Usifananishe uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na Vita ya Pili ya Dunia ambayo USSR ilivamiwa na kupoteza zaidi ya wanajeshi milioni 8.5 na raia takribani milioni 19.
 
Ktk dunia hii iliyojaa uongo usipende kuamini amini hata kama ndivyo ulivyofundishwa na kukupa marks darasani.
Tafuta ukweli pande zote.
Mengi ya unayofundishwa ni ili kuku shape uwe vile wao wanavyotaka.
Ndio maana nimesema, ukichagua kutotaka kuamini [hata kile ulichofundishwa darasani] utajikuta unakuwa denialist kwenye kila kitu kama wale wanaoamini kuwa vita kuu mbili za dunia hazikuwahi kutokea kabisa bali ni stori za kutunga tu.
 
nini tofauti kati ya ukomunisti na ujamaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…