Natoa 50k (elfu hamsini)

Natoa 50k (elfu hamsini)

Habari wakuu
Kama title ya uzi inavyosema ninatoa 50k Tsh kwa yeyote anayeweza kunikutanisha na moja kati ya watu wafuatao.
-Meneja/Afisa masoko wa Pepsi/Coca-Cola
-Meneja/Afisa masoko wa Kilimanjaro/Castle light/Serengeti light
-Joseph Kusaga
-Majizzo
-Diamond Platnumz

Haya twende kazi 50k inakusubiri
Kuhusu Diamond nahisi Wala usipate tabu wewe mtafute Zembwela tu atakushika mkono mkono hadi sebureni kwa Mond
 
Nimeenda sana ila naishiwa kuchezewa akili na watu wa reception...nenda rudi nenda rudiii
Yaani hao mameneja masoko hawapatikani ? sasa wanafanyaje Masoko; Kama Proposal yako imesimama kwanini usiwape hao mareception 20k au anzia kwa Meneja Masoko wa Kanda au hata sehemu ulipo....
Kukutanishwa namaanisha mtu ambaye anaweza kunipeleka direct nikakutana nao nikapresent nnacho present then nampa 50k yake
Kama nilivyosema issue sio kukutana nao issue ni kukubaliana na ulicho nacho na hata ukiwapa sio mafanikio unaweza kuishia kutapeliwa Idea yako..., ushauri kama unaweza kuliko kupeleka maneno matupu kama unaweza kufanya unachofanya kwa uraisi / udogo ili upate prototype ndio uwafuate au watakufuata..., unless otherwise ni kujitafutia kukatishwa moyo (inaweza ikawa brilliant Idea ila hawa jamaa wakasema ni Upuuzi hence kukukatisha tamaa)...
 
Uhuni huu.

Mwombaji kaomba msaada kihuni,na mnaomsaidia mnafanya uhuni pia. Huwezi kugawa mawasiliano ya mtu kisa umepewa hela na mtu mwenye uhitaji,unajua shida yake nini? Vipi Kama ana Nia ya kumdhuru? Au naye akaamua kuianika namba/mawasiliano ya hao mnaogawa Kisha yakatokea ya kutokea? Alafu Kumbuka mkuu,watu Sina hiyo anayowataka siyo watu wa kuoenda usumbufu. From nowhere huwezi ukataka tu namba ya kusaga Tena kwa kuweka dau. L

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Umeongea vizuri mkuu...lakinin hata mimi sijaomba namba wala chochote, natafuta mtu ambaye anaweza kunikutanisha nao f2f...kama ni issue ya usalama naamini kabla ya kuingia ndani ya ofisi za hao watu kuna walinzi right?
All in all please mkuu acha kuwaza hivo...nnajaribu kujinasua kwenye huu ugumu wa maisha...heri kwako kama mambo yako yanaenda vizuri
 
Habari wakuu
Kama title ya uzi inavyosema ninatoa 50k Tsh kwa yeyote anayeweza kunikutanisha na moja kati ya watu wafuatao.
-Meneja/Afisa masoko wa Pepsi/Coca-Cola
-Meneja/Afisa masoko wa Kilimanjaro/Castle light/Serengeti light
-Joseph Kusaga
-Majizzo
-Diamond Platnumz

Haya twende kazi 50k inakusubiri
Weka maelezo vizuri mkuu,tukukutanishe nao au tukupe namba za simu mkutane wenyewe kwa muda wenu.
Maana ukisema tukukutanishe nao tutatumia gharama kubwa zaidi ya hiyo elfu 50.
 
Mkuu hata mimi nnajua 50k sio kitu lakini ndo nimeongea uwezo wangu ulipoishia... kwahiyo hiyo 50k sio malipo ni kama zawadi au shukurani
Subiri kutapeliwa huko pm basi.

Unaonekana Ni mtoto au mama boy!!

50k ili mtu akupe mawasiliano ya Kusaga,au majizzo,au meneja wa Nini sijui,like serious?Unastahili kutosaidiwa ili ujifunze adabu na hekima kwanza.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ungekuwa serious katika kuomba kwako msaada Kuna wadau wangekusaidia bila hata kuhitaji Senti.

Mfano Mimi Nina rafiki yangu ana connection na baadhi ya member wa WCB,ungeelezea Kama mtu aliyekomaa akili na ana shida kweli ilikuwa simple kwa mtu Kama yeye akukutanishe nae huyo unayemuhitaji,ila umeingiza utoto.

Jf ni jukwaa kubwa na kuna watu wakubwa pia humu,wakati mwingine hata mwandiko unaweza kutukutanisha au kutukimbiza mbali na bahati/connections.

You are soy man.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Ni kweli kabisa mkuu,umenena vyema... huwezi amini nimeshajaribu njia nyingi ambazo unaweza sema kwa lugha yako "za ukomavu wa akili" lakini they didn't work out....this is me grabbing whatever strategy that comes my way😔
 
Yaani hao mameneja masoko hawapatikani ? sasa wanafanyaje Masoko; Kama Proposal yako imesimama kwanini usiwape hao mareception 20k au anzia kwa Meneja Masoko wa Kanda au hata sehemu ulipo....

Kama nilivyosema issue sio kukutana nao issue ni kukubaliana na ulicho nacho na hata ukiwapa sio mafanikio unaweza kuishia kutapeliwa Idea yako..., ushauri kama unaweza kuliko kupeleka maneno matupu kama unaweza kufanya unachofanya kwa uraisi / udogo ili upate prototype ndio uwafuate au watakufuata..., unless otherwise ni kujitafutia kukatishwa moyo (inaweza ikawa brilliant Idea ila hawa jamaa wakasema ni Upuuzi hence kukukatisha tamaa)...
Mkuu nina prototype tayari pia...ila asante sana kwa hilo wazo la kuanzia kwa meneja wa kanda au sehemu nilipo... nakuahidi na kazi pia.
 
Subiri kutapeliwa huko pm basi.

Unaonekana Ni mtoto au mama boy!!

50k ili mtu akupe mawasiliano ya Kusaga,au majizzo,au meneja wa Nini sijui,like serious?Unastahili kutosaidiwa ili ujifunze adabu na hekima kwanza.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Nakuahidi mkuu kama ningekuwa na uwezo zaidi ya hapo ningefanya...niliomba kujaribu kusaidiwa watu wanasema mkono mtupu haulambwi... please usiseme watu wasinisaidie...life crazy hard out here
 
Nakupa njia mbili ambazo hutotoa hata senti kwa mtu

1. Fungua account linkedin, weka picha yako genuine na maelezo machache. Weka post mbili tatu halafu omba urafiki na watu wenye vyeo kwenye hizo kampuni.

Anza ku like na kucomment posts zao 😁😁 hapa onesha umwamba kidogo ili kukamata attention yaani mtu akuzoee. Then zama DM omba kukutana nae live huwa hawapindui kirahisi

HII NJIA USITANGAZE NJAAN 😁😁 tUmia hata maneno soft ya kujifanya una interest kujifunza kitu flani

2. Hudhuria semina na mikutano ya hizo kampuni.. Ukisikia wanakutana na wajasiriamali au wameshiriki marathon au wana event . Iwe free au ya pesa NENDA

Sasa hapa inabidi uwe umeshamjua target wako na siku ya kukutana nae, hakikisha unajua vitu viwili vitatu kuhusu yeye nah jifanye kama unamuhusudu like he is a person of your interest au unamuadmire

NENDA FRIENDLY LAKINI WEKA PROFESSION YAKO MBELE, UKITANGAZA NJAA MAPEMA UTAONEKANA DESPERATE maana wanakutana na watu kama wewe daily, hawatopokea simu ukiwatafuta,🙏🙏

Hizi njia nilizotumia at least zimenisaidia kujua watu wawili watatu na hata humu jf usishangae wapo kwa hiyo ishi na watu vizuri na usitangulize pesa mbele 😁
 
Weka maelezo vizuri mkuu,tukukutanishe nao au tukupe namba za simu mkutane wenyewe kwa muda wenu.
Maana ukisema tukukutanishe nao tutatumia gharama kubwa zaidi ya hiyo elfu 50.
Yaani Meneja Masoko wa Kampuni za Vinywaji kumkutanisha kwa hio 50K ni ndogo !!!!, Pesa yetu ya madafu haina thamani ila sio kihivyo.....

Na hawa watu tusiwapandishe chati wana- machawa kibao na watu wa karibu wala sio kazi kuwapata (ingawa kuwapata haimaanishi chochote) issue ni kukubaliwa na unachowaambia especially wabongo... (kama issue ni kubwa subiri kupigwa kama ni ndogo subiri kupokea dharau)
 
Habari wakuu
Kama title ya uzi inavyosema ninatoa 50k Tsh kwa yeyote anayeweza kunikutanisha na moja kati ya watu wafuatao.
-Meneja/Afisa masoko wa Pepsi/Coca-Cola
-Meneja/Afisa masoko wa Kilimanjaro/Castle light/Serengeti light
-Joseph Kusaga
-Majizzo
-Diamond Platnumz

Haya twende kazi 50k inakusubiri
50k haitoshi mkuu fanya angalau 5M tufanye kazi yako haraka tu
 
Ni kweli kabisa mkuu,umenena vyema... huwezi amini nimeshajaribu njia nyingi ambazo unaweza sema kwa lugha yako "za ukomavu wa akili" lakini they didn't work out....this is me grabbing whatever strategy that comes my way[emoji17]
Kuna siku nilipita mitaa anakoishi Diamond,nikakuta vijana kadhaa pale nje ya geti. Nikamuuliza mtu niliyekuwa naye "hawa wanafanya nini pale getini?" Akanijibu wale 'madogo' wanamsubiri big(Diamond) anapotoka ndani kwenda kwenye mitikasi yake waongee nae,kila mmoja na shida yake,ila most of them,Kama siyo wote wanataka kuonyesha kipaji Cha kuimba mbele yake ili wapate collaboration au wasainiwe WCB.

Nilishangaa ila ndiyo ukweli,ukipita mitaa/nyumbani anakoishi diamond kwa wanaopajua nadhani watakubaliana na Mimi kuhusu ninachosema.

Point yangu ni nini? Watu waliofanikiwa Kuna namna ya kuwapata,maana Kama shida wanaliliwa kila sik,kuanzia huko online mpaka majumbani kwao,so Wala siyo wa kwanza wewe kulalamika usaidiwe.Kupitia hii stori unaweza kubadili namna ya kuomba connection na hao watu. Siyo rahisi kuwapata Kama unavyodhani,hata ukipewa namba zao Kama unavyodanganywa uongeze dau na baadhi ya members huko juu,utaishia kulia maana utapigwa.

Unaonekana ni msomi so jaribu kuwaza upya mkuu. Huu ndiyo msaada wangu kwako.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom