daza steven
JF-Expert Member
- Aug 30, 2016
- 359
- 358
Kule Vatican katika makao makuu ya kanisa ambapo ni sehemu kuu ya kumwabudia Mungu ambako ilitarajiwa ibada ya maji matakatifu kwa waumini hasa kipindi hiki cha Kwaresma kama Mungu alivyowaagiza miaka yote kwa sasa kumefungwa. Na maelekezo ya aliyowapa Mungu kufanya ibada hizo yamesitishwa kwa sababu ya Corona.
Kule Maka nchini Saudi Arabia katika mji mtakatifu ibada takatifu za Umra na Hija kama alivyoagiza Munyaazi Mungu katika vitabu vyake kupitia Quran Tukufu na Hadith zimefutwa kwa sababu ya Corona Covid 19.
Lakini ilipofika hatua ya Wamisri kutaka kuwauwa Wana wa Israel wote bila ya huruma Mungu wa Musa alijitokeza live na kila mtu anajua na safari haikusimama na hakufa mtu hata mmoja isipokuwa wamisri ndiyo walikufa wao.
Mungu wa Elia Mtishibil wakati wake, walipokosa majibu kati ya pande mbili Eliya alimwita Mungu wake na alishuka, nenda ukasome
Gideon yeye hali ya vita ilipozidi kuwa mbaya na Mungu aliwaambia ile vita watashinda haita lala yeye alisimamisha jua, nendeni mkasome, shughuli za Mungu hazijawahi simama kwa sababu yeyote.
Nahoji:
Mashekh, Maaskofu, Maulamaa, Wachungaji, Mitume na Manabii wa kizazi hiki mnafeli wapi.
Hatusikii chochote kutoka kwao nao wanalia na Corona Covid19. Matumaini ya dunia sasa hivi yote yapo kwa wanasayansi na serikali za duniani.
Yuko wapi Mungu wa Musa, yuko wapi Mungu aliyekuwa anatembea na mitume na Manabii wa kale.
Kwanini leo watu wa dini nao wanalia na kukimbilia kwa wanasayansi, mbona sadaka tunaendelea kutoa kila kuchao.
Kwa kichwa ambacho kimeenda shule kinaweza kisilale.