Angalia haya yafuatayo mpendwa:
1. Inawezekana unakula muda unaokula chakula chako, hasa nyakati za usiku. Hiyo huwatokea wengi wanaopenda kula chakula zaidi ya saa 5 usiku. Muda huo na kuendelea vimeng'enyo (enzymes) vya mwili vinakua inactive na hivyo kupelekea chakula kingi kutosagwa tumboni na sehemu nyingine stahiki, hivyo hakifyozwi na mwili . Mwisho wa siku chakula hicho hutolewa nje kwa njia ya haja kubwa kama uchafu.
2. Angalia ulaji wako.je huwa unapenda kunywa maji baridi mengi katikati ya mlo wako? Kama ndiyo basi unakosea kwani chakula huwa kinasagwa vizuri na kufyozwa kwenye joto la mwili la kawaida yaani 37[SUP]0[/SUP]c. Kunywa maji mengi baridi hupelekea joto la tumbo kuwa chini ya 37[SUP]0[/SUP]C, matokeo yake tumbo na sehemu husika kwa ufonzwaji wa chakula husubiri damu itoke sehemu nyingine za mwili kwa wingi kuja kwenye tumbo kwa ajili ya kupandisho joto hilo.
Matokeo yake chakula kinashindwa kusagwa na kfyonzwa na mwili ktk muda stahiki, hivyo kupelekea kutupwa nje kwa njia ya haja kubwa kama uchafu...