Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Pamoja na kwamba soka ni ajira, soka pia ni kielelezo cha taifa. Soka huitangaza nchi yoyote iwayo; kuiheshimisha na kuiaibisha. Kwa muda mrefu sasa, timu zetu za taifa za soka za wanaume zimekuwa hazifanyi vyema ukilinganisha na zile za wanawake.
Timu zetu za soka za wanawake zimekuwa zikifanya vyema ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Kwa mfano, hivi sasa dada zetu wako Afrika ya Kusini wakishiriki mashindano ya COSSAFFA kama mabingwa watetezi wa michuno hiyo. Dada zetu wanatutetea kila wakati na kupambana kwa ajili ya Tanzania yetu.
Timu za wanaume za taifa za soka zimekuwa zikiboronga. Soka hutanguliwa na uwekezaji-gharama kubwa. Ni hasara kwetu sote kama watanzania kutumia pesa nyingi kuziandaa na kuzihudumia timu za taifa za wanaume ambazo hazifanyi vyema. Ifike wakati timu hizi zipuuzwe ili zijifunze.
Uwekezaji na uwezeshaji wa maana ufanywe kwa timu zetu za taifa za akinadada zinazotutangaza na kutuheshimisha. Akidada hawa wapambanaji waangaliwe kwa upendeleo mkubwa kuliko ilivyo sasa ambapo wanaume ndiyoo hupewa kipaumbele lakini wanatuachia uchungu mwisho wa siku. Kufungwa kupo ila lazima kupambana kuwepo.
Haiwezekani sisi tujibanze kwenye klabu za Tanzania na Ulaya ili kupata furaha zetu za kisoka. Timu za Taifa za wanawake zinazotulindia heshima yetu kama nchi zipate kinachowastahili na wanaume nao wapate kinachowastahili. TFF na mnisikie!