Huyu binti anahitaji msaada, badala watu wampe ushauri wa kumsaidia mnakuja na dhihaka, ni nini sasa? Mnakua kama watu msiojitambua.
Hivi nawaza kama unaenda kituo cha huduma unakutana na majibu ya ovyo kama haya unajisikiaje?
Ngono ameshafanya, iwe salama au si salama. Alichotakiwa ni kuambiwa kwa namna ya kuelimishwa, hivi umejaribu kuwaza upande wa pili? Kama ni mwanao anakuomba ushauri unamjibu hivi basi ndio unamtuma akashauriwe na makundi rika.
Hii inaonesha hatuna utamaduni wa kuongea na vijana wetu kuhusu elimu ya afya ya uzazi. Na hata wanapokua wamepotea njia hatuwapi msaada wa kuwarudisha mstarini. Tunaropoka kama wahuni wa stand.
Malezi ni jukumu la wote, yeye kafikiria mazingira salama na ya usiri kwa upande wake akakimbilia huku, huku anakutana na majibu ya ovyo, atakimbilia wapi tena?
Mnapoamua kumjibu mtu hasa ukizingatia umri wake jitahidi kuwa muungwana, jaribu kuvaa uhusika wake, hakuna aliyekamilika.
Hapa tunamsema tu ila hawa hawa waliomsema kuhusu umri na ndoa karibia wote walianza katika mazingira kama yake tu.
Nyinyi ndio wale wahudumu mnaosababisha mtu akipata tatizo aogope kwenda kituo cha afya kwa kuogopa mineno yenu, matokeo yake wanajitibia tiba zisizo sahihi.