Haijallishi ata kama amaeanza miezi 3 nyuma na amefanikiwa kupata Adsense ni hongera kwake kuliko kukaa mtaani tu bure na kwenda kumchangia mhindi au mchina(kubeti).
Wengi ambao hawajui wanasema ni utapelibila Adsense sio utapeli mnavyomuona Millard Ayo anazunguka Dunia ni kwasababu ya ujeur wa Adsense.
Mwananchi, ITV huwa hawamalizii habari wakitaka uende ukasome kwenye Blog or ukatizame video kwenye Channel zao ilimradi tu wapate kipato kupitia Adsense.
Wengine tulifanya Blogging kipind cha nyuma sana na tukafanikiwa kujenga vibanda vyetu kabla ya kukutana na Rungu la GOOGLE ya self click (wakongwe wanaelewa).
Nachotaka kumshaur jamaa hapo ni kuwa:
1.Jitahidi sana kukomaa na contenta za nje mfano contents ambazo ata mtu wa SouthAfrica, kenya ikibd ata USA aweze kuwa mtembeleaji wako utapata CPC kubwa sana.
2.Ongeza nguvu na akili yako kwenye SEO ili uachane na kufanya sharing ya kwenye magroup. Najua vijana weng tu wanapata $100+ kwa kufanya sharing hasa Blog za Ajira ila ni kazi ngumu sana na muda wowote Whatsap wanaweza kuBan number yako.
SEO kama sio mtaalam na msomaji mzur itakuchukua muda mwing sana kujua coz contents nying zipo Technical sana, soma sana vitabu usibase kwenye video.
3. Tengeneza Group/channel ya Telegram ili uwe unapost na kuwa na visitors wako wa uhakika na uwe na uhakika kuwa utawapa madini ya maana ili wasitoke kwenye group lako. Telegram inachukua members weng sana na ukiwa serious utakuja unishukuru.
4.Kuwa na accounts za twitter na facebook ambazo zitakuwa na jina la blog yako na kule uwe ubatoa taarifa kama intro.. wakitaka habar kamili waje kwenye blog yako. Hizi account ukifanya vizur zitakuja kukulipa kwa sponsored Ads.
5. Usitegemee tu Adsense kama njia pekee ya kupata income jaribu njia tofauti tofauti ila hapo uhakikishe blog yako ina visitors wa nje (Tier One countrie), ukiweka Links za Affiliates utakuwa unapata commision ndogo ndogo kwa kuanza.
6. Usiwe mBAHILI sana kutoa hela ili utengeneze pesa, Mfano kuna tools za premium ukinunua ili ikusaidie na pia kwenye kufanya Promo pia usiwe na mkono wa birika ukumbuke hapa Duniani Nothing is free.
Nikupongeze sana kijana kwa hatua hiyo najua ni kazi ngumu sana ila mbeleni utakuja upate Tulizo na wengi watakukatisha tamaa maana weng wao hawajui haya mambo na wanaojua wanakula PESA kimya kimya hawasemagi WABONGO tunajijua tabia zetu.
Hela unazopata jaribu kuwekeza kwenye Fixed Assets na kufanya biashara tofauti tofauti maana bloggers wengi nawajua ikifika tu tarehe 22 Google akishafanya yake wao ni BATA mpaka inaisha hela yote.