Natumiwa sana na ndugu zangu kwenye shida zao. Zikiisha wanapotea

Sasa unataka wakutafute bila sababu ya msingi ??

Yani mtu akusumbue kukupigia simu halafu akwambie tu "nilikuwa nakusalimia" si ndio hivyo unavyotaka au?
 
Usiwe legelege... jikite na familia yako!! Assess kama wao wanakusaidia..! Kama hawakusaidii au hawana hata ukaribu nawe wa kuongea na kubadilishana tu mawazo bila kuomba msaada achana nao. Hawa ndio watu wale baadae mambo yako yakibuma wanakusema kuwa ulipata fursa ila uliichezea wakati kiuhalisia kiasi ulikua ukiwasaidia...
 
Binafsi nimekua mhanga wa hilo kwa miaka.
Siku moja nikajitafakariiiiiii nikajifunza kusema Sina/Hapana.
Tangu hapo nimepoteza wengi na kununiwa wengine wamekua maadui kabisa kunisema vibaya kwa watu lakini haijanidhuru maana nimepunguza mzigo wa watu na nina aammani
 
Yawezekana ndipo dunia ilipotufikisha hapa maana mimi nimefikia mahala nataka kujifunza kuwa na roho ngumu nisisaidie tena mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…