Mhakiki
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,385
- 2,101
Rudi kwa mkeo kimya kimya.Mimi ni Baba wa watoto watatu, nimeoa ndoa yenye miaka 12 sasa. Kuna sehemu niko nafanya kazi mke wangu naye ni mfanyakazi na ni ngumu kuhama basi tunahisi tofauti.
Hapa ofisini kuna dada nimeanza naye mahusiano ni mwaka 4 sasa, ni kama nimehamia kwake nilipokuwa nimepanga mimi naweza kukaa hata miezi 6 siendi huko, kila mtu anafahamu kuwa huyu ni mke wangu hata ofisini kila kitu tunafanya pamoja wanajua nishaachana na mke wangu.
Wakati nakutana naye nilimuambia kuwa nimeoa na kipindi hicho mke wangu alikua anakuja huku bila shida ila baadaye nilimkataza kwakua ndiyo mimi naenda tu.
Kashanitambulisha kwao na mimi kwetu kuna baadhi ya ndugu wanamfahamu. Anaamini nitamuoa na kweli kuna kipindi mimi na mke wangu mahusiano yaliyumba tukaenda mpaka mahakamani kufuatilia talaka lakini mke aligoma hivyo niliacha mambo ya kufuatilia.
Sababu ya kuja kwako ni hivi, nimemchoka huyu dada na kweli sasa hivi nataka kurudi kwenye ndoa yangu. Naona kama nampotezea mdua ana miaka 33 hana mahusiano mengine ni kama anasubiria mimi kauchana na mke wangu, naona ashaanza kisirani ananichunga kama mke kitu amabcho sitaki!
Shida inakuja kwamba kuna vitu vingi vya maendeleo nimefanya naye, tumejenga nyumba mbili, tuna gari na biashara ambayo kila kitu kina majina yangu lakini yeye alichangia kwani alichukua mpaka mikopo akiamini mimi ni mume wake kwakua tu sina mawasiliano mazuri na mke wangu.
Hofu yangu ni kwamba nikitaka kumuacha atadai mali kitu ambacho siko tayari kumpa. Kuna watu wananishauri kubadilisha hizi mali kuandika majina ya wanangu, nauliza je ana haki yoyote.
Mimi nayeye hatuna mtoto nimekua makini sana kuhakikisha simpi mimba ila yeye ana mtoto alizaa na mwanaume mwingine na tunaishi naye, nimechoka nataka kurudi kwenye familia yangu, je namuondoaje huyu Bibie bila kumpa chochote.
Nimejaribu kuhangaika ili ahamishwe mkoa lakini imekua ngumu, kila nikihangaika anabana. Kwakweli nimechoka haya maisha ya kuishi na mchepuko, nataka kwenda kumchukua mke wangu tuishi pamoja kwani huu umbali mke wangu naye asije kuchepuka, nisaidie nafanya nini?
Ila punguza UJINGA kwa kuacha mbachao kwa msala upitao. Ujinga mwingine ni kujimwaga kwa mchepuko KUHUSU habari zako na mkeo jambo hili ni baya hata kwenye kikao chetu wanaume Huwa tunalikemea kwa nguvu zote.
KUHUSU mali mwachie kwa roho nyeupe.