Nauanika ukweli: Mwaka huu wagombea wote wa CCM lazima wawe 'Timu Magufuli"

Nauanika ukweli: Mwaka huu wagombea wote wa CCM lazima wawe 'Timu Magufuli"

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kwenye siasa, ambamo nimo kwa miaka takribani arobani, timu hazikosekani. Kuanzia kwenye vyama vya siasa na hata kwenye chaguzi, ushindi hupatikana kupitia timu. Timu huratibu bila tabu; hutibu kama tabibu; hunogesha kama mkesha na hurekebisha kama maisha. Timu ndiyo kila kitu kwenye siasa na ushindi wake.

Awamu zote tano za uongozi wa Taifa hili zilitanguliwa na kuratibiwa na timu. Hayati Nyerere alikuwa na timu yake; Mzee Mwinyi alikuwa na timu yake; Mzee Mkapa alikuwa na timu yake; Mzee Kikwete alikuwa na timu yake na hata sasa Rais Magufuli ana timu yake. Timu huunda uongozi kama ngozi na kutamba hadi kutambaa. Timu hufaidi kama siku ya Eid.

Awamu zote zilizotangulia, Marais ndiyo walikuwa Wenyeviti wa CCM Taifa. Walikuwa na neno la mwisho kwenye uteuzi wa wagombea wa CCM wa ngazi zote za kichama na kiserikali. Rais anapokuwa Mwenyekiti lazima aibebe timu yake na kuipa nafasi ya kucheza kama Barcelona-mpira wa danadana kama Maradona. Timu haziepukiki.

Wanachama wote wa CCM mkae mkijua kuwa mwaka huu wagombea wote LAZIMA wawe ni Timu-Magufuli. Na si wale wa kujipendekeza kwake au wale wa kujipitisha majimboni na katani. Ni wale waliokuwa na Magufuli tangu mwanzo. Si wale wadandiaji njiani au waliojisogeza kwake kwa kumsifu Magufuli kwa kila jambo. Ni wale wa enzi na enzi.

Wapo wateule wa majimboni na katani ambao hata hawajawahi kuwepo huko. Ila watatumwa kwenda kugombea ili kuiimarisha timu hiyo ya Magufuli. Wapo watakaookota embe kwenye mnazi. Mambo ya kjipitishapitisha na kujipendekeza hayatakuwa na nafasi kwenye uchaguzi huu. Rais Magufuli anayo timu yake na ataitetea na kuipa tena nafasi.

Tuwe makini na ugonjwa wa corona!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
 
Nyie wazee simgewaachia vijana, wagombee hizo nafasi za Udiwani na ubunge....Alafu nyie mkasubilia Uteuzi wa viti maalumu au?
 
Magufuli hana timu yeyote ndani ya ccm ana watu wachumia tumbo waliomzunguka na kumsifia ili kupiga pesa za umma.

Wazalendo wote kama wakina Butiku, Warioba watajiweka pembeni uchaguzi huu, baada ya kumsifia sana 2015 na yeye ku destroy kila kitu.

Watabaki wa kusifia wapiga vinanda na magitaa kama wakina Bashiru, Polepole, Bashite kama hauna njaa huwezi kuunga mkono Magufuli.

Magufuli hana timu niwasaka tonge tu walio mzunguka na siku akiondoka ofisini wataanza kumtukana kama walivyofanya kwa Kikwete.
 
Hakuna mzalendo hapo, Butiku mwenyewe Nyerere foundation ameigeuza ni mali yake,Warioba kwny Meremeta amehusika na Shoo.

Mzalendo alikua Nyerere tu,hawa wengine wote wanapambana ni kama sisi tu.
 
Nape, January, Mwiguru, Ngereja.... Sijui itakuwaje mwaka huu? ama kweli kila zama na kitabu chake. Wako wapi Jerry Slaa, Vita Kawawa? Timu JK chaliii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni muda muafaka wa wale wenzangu mie aka wafia chama kuonja joto ya jiwe na wale timu wahamiaji ni kicheko yaani njia yao ni nyeupeee pee!!

"Corona ni janga jipya halina chama tuwe makini....tutulie majumbani..Muda muafaka ya kuyajenga kifamilia..!!"
 
Mkuu P. Kwa hiyo hata wale waliounga juhudi na wamepewa nyadhifa kubwa kwenye chama na Serikali, nao ni wadangaji?
 
Magufuli hana timu yeyote ndani ya ccm ana watu wachumia tumbo waliomzunguka na kumsifia ili kupiga pesa za umma.

Wazalendo wote kama wakina Butiku, Warioba watajiweka pembeni uchaguzi huu, baada ya kumsifia sana 2015 na yeye ku destroy kila kitu.

Watabaki wa kusifia wapiga vinanda na magitaa kama wakina Bashiru, Polepole, Bashite kama hauna njaa huwezi kuunga mkono Magufuli.

Magufuli hana timu niwasaka tonge tu walio mzunguka na siku akiondoka ofisini wataanza kumtukana kama walivyofanya kwa Kikwete.
Hujaelewa maana ya timu dogo.
 
Back
Top Bottom