incredible mimi
Senior Member
- Apr 14, 2024
- 179
- 256
Sijawahi kujivunia Utanzania Wangu
Nakumbuka nyimbo za shule za kipindi kile tulizokuwa tukiimba kwa furaha na bashasha.
Tukiwa tumevalia uzi mweupe na bukta za blue, tuliimba “Mungu ibariki Tanzania” na “Tazama ramani utaona nchi nzuri” kwakweli tuliimba kwa bashasha kweli kweli.
Na kwa utoto wetu tulikuwa so proud na taifa hili.
Miaka imeenda sasa tumekuwa wakubwa na ule usemi wa Mama “mwanangu kuwa uyaone” sasa tumejionea kwa macho.
Miaka zaidi ya 60 ya uhuru wa taifa hili lakini bado maadau watatu wanaendelea kuitafuna inch hii tena kwa kasi ya ajabu.
Ujinga, umasikini, maradhi ni wimbo wa taifa kila uchwao.
Cha ajabu umasikini na maradhi hutafuna zaidi watu wa vipato vya chini, ila ujinga hili hutafuna zaidi viongozi wetu maana wao ndo wamepewa dhamana ya usimamizi wa raslimali za Taifa hili.
Viongozi ni wachumia tumbo na wanawimbo wao sijajua mtunzi alikuwa nani ila unaitwa “Chukua chako mapema”
Na sishanga kwenye hili maana Nchi yoyote ya chama kimoja ambayo imejivika kivuli cha vyama vingi, nchi yoyote isiyoheshimu Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa Kidemokrasia hili ni jambo la kawaida kutokea.
Wananchi wanateseka kwa ugumu wa maisha huku serikali sikivu ikiendelea kuwakandamiza kwa kodi zisizo na kichwa wala miguu.
Viongozi wameshindwa kutafuta vyanzo imara vya mapato na kuamua kumuangushia mzigo wote mwananchi wa kawaida anaepambana kupata mlo wake wa siku.
Kodi zimekuwa mwiba kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Ni kawaida kukuta kodi inazidi dhamani ya manunuzi ya bidhaa husika. Hii hupelekea wafanya biashara kushindwa ku compete kwenye soko la dunia hasa linapokuja swala la kodi kuathili uti wa mgogo wa biashara husika. Refer mgomo wa wafanya biashara soko kuu na lakimataifa kariakoo..
Chungulia kidogo kwny kodi za magari kuingia nchi, utaagiza gari kwa milion 10 utapaswa kulipia kodi million 15 hadi 17 jumla gari litakughalimu milion 25 had 27 kuingia barabarani kwa matumizi, which is nonsense.
Hapo hujagusia kodi ya ardhi ambayo sasa inalipwa na wapangaji na sio mwenye nyumba husika. Kama umepanga chumba kimoja na umefungiwa mita, kodi hii inakuhusu.
Hapo sijaongelea gharama za vifurushi vya internet na makato ya kipuuzi kwa watumiaji wa mitandao ya simu.
Gharama za kupokea na kutuma pesa nikubwa kiasi kwamba hatuna pakukimbilia, sio bank wala mitandao y cm, wote n nyonya damu.
Mifumiko ya bei za chakula isijoyali hali halisi za walaji.
Kupanda hovyo kwa bei za mafuta na gas as if hakuna mamlaka husika za kudhibiti na kusimamia nishati hizo.
Ajira rasmi hakuna, wanakomaa wenyewe tuu, na yakiwapalia utasikia tangazo la ajira za muda, miezi mi3, miezi 6.
Lengo kubwa ni kupunguza gharama za matumizi ya pesa za serikali ndani ya sekretaliet husika,
Kwa vimikataba hivyo vya nusu mwezi wanaokoa pesa nyingi sn km pesa za kujikimu, contributions za NSSF, NHIF, fedha za safari, likizo za uzazi, pesa za dharula, misiba,
gharama za kuingizwa kwenye payroll za malipo ya serikali na stahiki nyingine anatazo hitaji ikiwa utaajiriwa.
Kipindi wanatumia ujuzi na jasho lako kufanikisha masuala ya kitaifa, linapokuja swala la ajira unawekwa kushoto. Hii imewakuta sn vijana wa jkt waliovuja jasho kwny shughuli mbali mbali za ujenzi wa taifa na sasa wapo nyumbani.
Tabaka la wenyenacho na wasionacho ni kubwa sn sn sn, huku tunakosa mlo wa siku, kule kuna dhifa za kitaifa watu wanakula na kusaza, suti za gharama na ujazo wa full tank by gvt pay check.
Deni la taifa linakua kwa mikopo ya kila kukicha, tukiuliza tunaambiwa vijana mmekubukwa.
Mnaambiwa undeni vikundi vya ushirika, mara njoo na business plan nzuri ukopeshwe, kamilisha vyote.. bt trust me utazunguka inchi nzima ofisi husika inayotoa hiyo mikopo hutokaa uione.
Hatuna dira ya Taifa, na kama ipo ni dira jina tuu, hatuna vipaumbele vya taifa, hasa vinavyo lenga maendeleo n ustawi wa nchi hasa vijana.
Limekuwa Taifa linalopenda kuona vijana wanateseka, wazazi wanaangaika na vijana wao waliomaliza vyuo wapo mitaani.
walio karibu kujiajiri wamekutana na vikwazo vingi vya kimfumo vinavyopeleka biashara kufa.
“wamerudisha mpira kwa kipa”
Kwenye maharusi wanachangiana mabilions of money, wakati majimboni mwao wananchi wanakufa kwa kukosa huduma bora za afya..
Mpige kura msipige kura watatangazwa tuu washindi, watapita bila kupingwa. wananchi hamna tena power y kuchagua nani mnamtaka ni nani hamumtaki.
Thats why now days hawaombi tena kura za wananchi, matokeo yake wameelekeza nguvu zao kwa viongoz wakuu wa vyama, hapo ni mwendo wa kuabudu na kusujudu tu, ni mwendo wa uchawa kwenda mbele..
Imekuwa ni nchi ya kula kwa urefu wa kamba, na kamba za malisho huongezwa kadri unavyomfurahisha mfungaji.
Vijana wasio na upeo na kuijali kesho yao huangukia kwny wimbi la kusifu n mapambio, hawa huvaa miwani za mbao hata wasione wapi wanaelekea, na km kijana upi mchango wako kwa jamii yako.
Wao ni ngonjela mwanzo mwisho wakiamini siku system itawafuta jasho.
Wenzangu ni mimi tulioamua kusimama kwenye kweli tujiandae kukabiliana na kesi za uhujumu uchumi.
Utafungwa jela Ili jamii isipate mtazamo kutoka kwa watu makini wenye mitazamo chanya.
Kunawakati Mungu pekee ndo ataweza kutuvusha kwny hili.
Vijana wenzangu tusikate tamaa, hatima yetu ipo mikononi mwetu, tuvuje jasho ili walau watoto wetu waione kesho yao ilio bora zaidi ya leo.
Sijivunii kuwa MTANZANIA. 😔