Sijawai kujivunia Utanzania Wangu
Nakumbuka nyimbo za shule za kipindikile tulizokuwa tukiimba kwa furaha na bashasha,
Tukiwa tumevalia uzi mweupe na bukta za blue, tuliimba Mungu ibariki na Tazama ramani kwa bashasha kweli,,
Hakika tulikuwa n uzalendo kweli kweli,
Miaka imeenda ss tumekuwa wakubwa na ule usemi wa mama “mwanangu kuwa uyaone” ss tumejionea kwa macho.
Miaka zaid ya 60 ya uhuru wa taifa hili lakini bado maadau watatu wanaendelea kuitafuna inch tena kwa kasi ya ajabu.
Ujinga, umasikini, maradhi n wimbo wa taifa kila uchwao..
Chaajabu umasikini na maradhi hutafuna zaidi watu wa vipato vya chini, ila ujingi hili utafuna zaid viongozi wetu maana wao ndo wamepewa dhamana y usimamizi wa raslimali za Taifa hili.
Viongozi ni wachumia tumbo na wanawimbo wao sijajua mtunzi nani ila unaitwa “Chukua chako mapema”
Na sishanga kwenye hili maana Nchi yoyote ya chama kimoja ambayo imejivika kivuli cha vyama vingi, nchi yoyote isiyo heshimu uhuru wa kujieleza, uhuru wa kidemokrasia hili n jambo la kawaida kutokea..
wananchi wanateseka kwa ugumu wa maisha huku serikali sikivu ikiendelea kuwakandamiza kwa kodi zisizo na kichwa wala miguu.
Viongozi wameshindwa kutafuta vyanzo imara vya mapato na kuamua kumuangushia mzigo wote mwananchi wa kawaida anaepambana kupata mlo wake wa siku.
Kodi zimekuwa mwiba kwa wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo..
Ni kawaida kukuta kodi inazidi dhamani ya manunuzi ya bidhaa husika. Hii hupelekea wafanya biashara kushindwa ku compete kwny soko la dunia hasa linapokuja swala la kodi kuathiri uti wa mgogo wa biashara husika.
Chungulia kidogo kwny kodi za magari kuingia nchi, utaagiza gari kwa milion 10 utapaswa kulipia kodi million 13 had 15.. na gari litakughalimu milion 23 had 25 kuanza itumia, which is nonsense.
hapo hujagusia kodi ya ardhi ambayo sasa inalipwa na wapangaji na sio mwenye nyumba husika. Km umepanga chumba kimoja na umefungiwa mita, kodi hii inakuhusu.
Hapo sijaongelea gharama za vifurush vya internet na makato y kipuuzi kwa watumiaji wa mitandao ya simu..
Mifumiko ya bei za chakula isijoyali hali za walaji.
kupanda hovyo kwa bei za mafuta na gas as if hakuna mamlaka husika za kudhibiti na kusimamia mifumuko hiyo..
Ajira rasmi hakuna, wanakomaa wenyewe tuu, na yakiwapalia utasikia tangazo la ajira za muda, miezi mitatu..
Hapo wanaokoa gharama kazaa, km pesa za kujikimu, contributions za nssf, NHIF na kuingia kwny payroll za malipo ya serikali na stahiki nyingine anazohitaji km mwajiriwa..
Kipindi wanatumia ujuzi na jasho wako kufanikisha masuala ya kitaifa, linapokuja swala la ajira unawekwa kushoto..
Tabaka la wenyenacho na wasionacho ni kubwa sn sn sn, huku tunakosa mlo wa siku, kule kuna dhifa za kitaifa watu wanakula na kusaza.
Deni la taifa linakua kwa mikopo ya kila kukicha mara leo urabuni, kesho korea, keshokutwa china… tukiuliza tunaambiwa vijana mmekubukwa,
Mnaambiwa undeni vikundi vya ushirika, mara njoo na business plan nzuri ukopeshwe, kamilisha vyote.. bt trust me utazunguka inchi nzima ofisi husika inayotoa hiyo mikopo hutokaa uione.
Hatuna dira y Taifa, na km ipo ni dira jina tuu, hatuna vipaumbele vya taifa,
Limekuwa Taifa linalopenda kuona vijana wanateseka, wazazi wanaangaika na vijana wao waliomaliza vyuo wapo mitaani,
wamejaribu kujiajiri wamekutana na vikwazo vingi vya kimfumo vinavyopeleka biashara kufa
“wamerudisha mpira kwa kipa”
Kwny maharusi wanachangiana mabilions of money, wakati majimboni mwao wananchi wanakufa kwa kukosa huduma bora za afya..
Mpige kura msipige kura watatangazwa tuu washindi, wananchi hamna tena power y kuchagua nani mnamtaka n nani hamumtaki.
tht why now days hawaombi tena kura kwa wananchi,
matokeo yake wameelekeza nguvu zao kwa viongoz wakuu wa vyama, hapo ni mwendo wa kuabudu na kusujudu tuu, ni mwendo wa uchawa kwenda mbele..
Imekuwa n nchi y kula kwa urefu wa kamba, na kamba za malisho huongezwa kadili unavyomfurahisha mfungaji.
Wenzangu n mm tulioamua kusimama kwenye kweli tujiandae kukabiliana na kesi za uhujumu uchumi,
Utafungwa jela Ili jamii isipate madini kutoka kwa watu makini wenye mitazamo chanya.
Kunawakati Mungu pekee ndo ataweza kutuvusha kwny hili.
Vijana tusikate tamaa, cz hatima yetu ii mikononi mwetu, tuvuje jasho ili walau watoto wetu wasipate utapia mlo..
Cjivunii kuwa MTANZANIA