BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Kituo cha Bajaj Ferry hapa Dar es Salaam, zile Bajaj zinazoelekea Kibada, Kisiwani n.k. wahusika wamekuwa na kawaida ya upandishaji holela wa nauli.
Nauli inajulikana ni shilingi mia saba lakini wiki kadhaa zilizopita ilipanda ghafla na kuwa Shilingi 1,000 mpaka 1,500 kwa abiria wanaoelekea Kisiwani.
Tulipowauliza madereva kulikoni? Wakidai kuna matengenezo ya barabara kutoka Kituo cha Stivin mpaka Round About, lakini lakini cha kushangaza zaidi matengenezo hayo yamekamilika wiki mbili zilizopita lakini nauli zimeendlea kutoeleweka kila dereva amekuwa na bei zake.
Tunaomba mamlaka inayohusika Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) itusaidie katika hili ili ikiwezekana isimamie kuratibu hixo bei, hata kama inatambulisha Bajaj ni usafiri wa kukodisha lakini kama bei haziwezi kudhibitiwa kila mmoja atajiamua bei yake na mwisho wake inakuwa vurugu mechi.