Nauli ya treni ya kasi Kenya ni Tsh. 400,000 wakati ya Tanzania ni Tsh. 100,000. Kwa nauli hizo Gen Z wapo sahihi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Ikiwa nauli ya SGR Treni ya mwendokasi ya Kenya inayotumia diesel mwa umbali wa Nairobi-Mombasa ni Tsh. 400,000 wakati Kwa umbali huo huo wa Dar-Makutopora Kwa SGR ya umeme ya Tanzania ni Tsh. 100,000.

Hata ungekuwa wewe ni Gen Z utaacha kuandamana kweli na kusema Ruto Must go?😂😂😂😂

--
Wizara ya Uchukuzi nchini Kenya imetangaza nauli ya treni ya abiria ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Nairobi-Mombasa kwa tiketi ya daraja la juu (premium) kuwa Ksh 20,000 [TZS laki 4] kwa safari ya kwenda na kurudi.

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na viti vya umeme vinavyoweza kukunjwa na kuzunguka, sehemu za kuchaji, sehemu maalum kwa ajili ya kunyonyesha na kubadilishia watoto, vyoo na vifaa vya usaidizi kwa ajili ya wazee na walemavu.

My Take
Tanzania ni Nchi ya maziwa na asali.

View: https://youtu.be/yJ0RXPdRWtc?si=ydDR80l9i2D6HrJN
 
Ulichochanganya ni kuzibadili hizo KSh 20,000 na kuzileta huku kwenye madafu hela yao ni Ksh 20,000 hawalipi laki nne...
 
Ikiwa nauli ya SGR Treni ya mwendokasi ya Kenya inayotumia diesel mwa umbali wa Nairobi-Mombasa ni Tsh. 400,000 wakati Kwa umbali huo huo wa Dar-Makutopora Kwa SGR ya umeme ya Tanzania ni Tsh. 100,000.

Hata ungekuwa wewe ni Gen Z utaacha kuandamana? 😂😂😂😂

--
Wizara ya Uchukuzi nchini Kenya imetangaza nauli ya treni ya abiria ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Nairobi-Mombasa kwa tiketi ya daraja la juu (premium) kuwa Ksh 20,000 [TZS laki 4] kwa safari ya kwenda na kurudi.

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na viti vya umeme vinavyoweza kukunjwa na kuzunguka, sehemu za kuchaji, sehemu maalum kwa ajili ya kunyonyesha na kubadilishia watoto, vyoo na vifaa vya usaidizi kwa ajili ya wazee na walemavu.

My Take
Tanzania ni Nchi ya maziwa na asali.

Hivi SGR tanzania imefika Makutopora?
Labda nikusaidie pia kuwa; Train ya Kenya " Madaraka Express Train" ni usafiri wa bei poa sana
Bei ninayo ifaham daraja la tatu ni shs za kenya 1000 (mombasa to Nairobi)sawa na shs 20,000 za Tanzania; na Daraja la kwanza shs 3000 Mombasa to Nairobi sawa na shs 60,000 za Tanzania
Bei zao zipo kwenye mtandao hivyo usidanganyike na storI za kijiweni
 
Ikiwa nauli ya SGR Treni ya mwendokasi ya Kenya inayotumia diesel mwa umbali wa Nairobi-Mombasa ni Tsh. 400,000 wakati Kwa umbali huo huo wa Dar-Makutopora Kwa SGR ya umeme ya Tanzania ni Tsh. 100,000.

Hata ungekuwa wewe ni Gen Z utaacha kuandamana? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

--
Wizara ya Uchukuzi nchini Kenya imetangaza nauli ya treni ya abiria ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Nairobi-Mombasa kwa tiketi ya daraja la juu (premium) kuwa Ksh 20,000 [TZS laki 4] kwa safari ya kwenda na kurudi.

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na viti vya umeme vinavyoweza kukunjwa na kuzunguka, sehemu za kuchaji, sehemu maalum kwa ajili ya kunyonyesha na kubadilishia watoto, vyoo na vifaa vya usaidizi kwa ajili ya wazee na walemavu.

My Take
Tanzania ni Nchi ya maziwa na asali.
Acho uongo uongo niliipanda December mwaka jana kutoka mòmbasa hadi Nairobi ilikua 1400sholling ya kenya sawa sawa na 20,000 kwa mwaka jana kuna umbali wa 620km.
 
Bado haibadilishi maana. Thamani ni ile ile, alicho fanya yeye ni kuiweka katika thamani ya shilingi ya Tanzania. Hiyo 20k shilingi ya Kenya ukiwa huko kwao kuipata ni mtiti pia.

Kingine mleta uzi ni muongo muongo tu, hiyo nauli sio sahihi kabisa. Nimewahi kuwa huko na sikuwahi kuona hiyo nauli mpaka naondoka.
Ulichochanganya ni kuzibadili hizo KSh 20,000 na kuzileta huku kwenye madafu hela yao ni Ksh 20,000 hawalipi laki nne...
 
Ikiwa nauli ya SGR Treni ya mwendokasi ya Kenya inayotumia diesel mwa umbali wa Nairobi-Mombasa ni Tsh. 400,000 wakati Kwa umbali huo huo wa Dar-Makutopora Kwa SGR ya umeme ya Tanzania ni Tsh. 100,000.

Hata ungekuwa wewe ni Gen Z utaacha kuandamana? 😂😂😂😂

--
Wizara ya Uchukuzi nchini Kenya imetangaza nauli ya treni ya abiria ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Nairobi-Mombasa kwa tiketi ya daraja la juu (premium) kuwa Ksh 20,000 [TZS laki 4] kwa safari ya kwenda na kurudi.

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na viti vya umeme vinavyoweza kukunjwa na kuzunguka, sehemu za kuchaji, sehemu maalum kwa ajili ya kunyonyesha na kubadilishia watoto, vyoo na vifaa vya usaidizi kwa ajili ya wazee na walemavu.

My Take
Tanzania ni Nchi ya maziwa na asali.
Halafu mwendo wake wa masaa 6 kwa umbali huohuo ambao sisi tutatembea masaa matatu.
 
Hivi SGR tanzania imefika Makutopora?
Labda nikusaidie pia kuwa; Train ya Kenya " Madaraka Express Train" ni usafiri wa bei poa sana
Mwaka jana walikuwa wanachaji daraja la tatu shs za kenya 1000 (mombasa to Nairobi)sawa na shs 20,000 za Tanzania; na Daraja la kwanza shs 3000 Mombasa to Nairobi sawa na shs 60,000 za Tanzania
Bei zao zipo kwenye mtandao hivyo usidanganyike na storI za kijiweni
Wametangaza wenyewe hizo bei unakataa nini we jamaa!?
Aya tulinganishe na Tanzania.
Daraja la tatu Tanzania itakua 24000 mpaka Dodoma na la kati itakua 37000 mpaka Makutupora Dodoma.
Na VIP 100k ilahli wao 20k ambayo sawa na 400k ya kitanzania.
Tena ukitizama yetu ina ufanisi kuliko yao.
Aya hapo bado hujaona kuwa wamewaminya sana!?
Au hesabu hujui mzee!?
 
Acho uongo uongo niliipanda December mwaka jana kutoka mòmbasa hadi Nairobi ilikua 1400sholling ya kenya sawa sawa na 20,000 kwa mwaka jana kuna umbali wa 620km.
Kilometa 620 zimetokea wapi kutoka Nairobi to Mombasa!?
Embu piga hesabu vizuri.
 
Ulichochanganya ni kuzibadili hizo KSh 20,000 na kuzileta huku kwenye madafu hela yao ni Ksh 20,000 hawalipi laki nne...
Hela ya nani Ina Nguvu hapo? Huoni Lakini yetu unayoita ya madafu inakupa Huduma Bora zaidi kushinda ya Kundustan?
 
Kilometa 620 zimetokea wapi kutoka Nairobi to Mombasa!?
Embu piga hesabu vizuri.
Ni 480 ukitumia barabara ya rami ila kwa Sgr kuna sehemu inaxunguka zinaongezeka mpaka 600km
 
Acho uongo uongo niliipanda December mwaka jana kutoka mòmbasa hadi Nairobi ilikua 1400sholling ya kenya sawa sawa na 20,000 kwa mwaka jana kuna umbali wa 620km.
Ulipanda kajamba nani ambayo sawa na 28,000 Kwa hela ya Tsh.
 
unasahau labda kenya wana kipato kikubwa klk tanzania, kenya kuna middle class kubwa zaidi kwa mbali sana tu kulinganisha na tanzania, uki factor in hiyo utaona labda tofauti wala siyo kubwa kiivyo …
 
Ni 480 ukitumia barabara ya rami ila kwa Sgr kuna sehemu inaxunguka zinaongezeka mpaka 600km
Kwa SGR ni kilometa 472 ama 293 miles.
Sijasema mimi bali vyombo vyao vya KR hata ukiingia katika blog yao ya KR wanakwambia journey takes 6 hours in a distance coverage of 472 kms.
We hizi km 600 umetoa wapi!?
Kaka dunia hii ya utandawazi still unadanganya!?
 
unasahau labda kenya wana kipato kikubwa klk tanzania, kenya kuna middle class kubwa zaidi kwa mbali sana kulinganisha na tanzania …
Jidanganye mzee.
Kenya ina masikini ambao kila uchwao wanalalamika upandaji bei wa vyakula na tozo zisizo na maana.
 
Back
Top Bottom