"Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:
(i) Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
(ii) Kuandika katika mlango wa kuingia abiria viwango vya nauli inavyotoza katika njia anayotoa huduma ya usafiri
(iii) Kutoa tiketi kwa kila abiria ikionyesha jina la mmiliki, namba ya usajili wa basi, kituo cha mwanzo na mwisho wa safari, nauli na tarehe ya safari
(iv) Kuzingatia usafi wa mabasi na sare za wafanyakazi wao, kutotumia wapiga debe, kutotumia lugha chafu, kutokatisha njia na kutowabugudhi wanafunzi
(v) Kubeba idadi ya abiria kulingana na uwezo wa basi na kuwepo na nafasi ya kutosha na sehemu ya kushika kwa abiria wanaosimama ndani ya mabasi makubwa
(vi) Kuhakiksha basi linabeba idadi ya abiria ambao wanapaswa kubebwa kwa mujibu wa idadi iliyoidhinishwa na mtengenezaji wa basi
(vii) Kuwepo na Bima inayowalinda abiria wote wa basi husika
(viii) Abiria wanawajibika kurejesha utamaduni wa kupanga mabasi kwa mstari na mabasi nayo yanapaswa kupakia abiria kwa mstari." (kama ilivyoletwa na PAW).
Cha ajbu ni kwamba mbona,hakuna kipengele kinachowabana wenye daladala kukarabati magari yao-service na hali ya viti-kuna baadhi ya DALA2 zimebaki na vyuma tu na mara nyingi abiria wanajikuta nguo zao zinmetobolewa au kuchanika, ama muda mwingine hata kuumizwa na vyuma hivo, hili halijazungumziwa na DAR-"KOBOA"! wanajali tu maslahi yao bila kujali usalama wa wateja wao! jamani watu wa "KIJANI" mtuonee huruma cc walalahoi! au kwakuwa nyie hampandi Dala2, na mnapewa mafuta ya Bure na allowance kedekede! inasikitisha kuwa hata yule anayejinadi kuwa mtoto wa mkulima amejisahau au anatulaghai: sishangai maake ni MWONGO hodari sana!