Nauliza hiviiiii..

Nauliza hiviiiii..

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Posts
12,271
Reaction score
1,052
Ni watanzania gani wanaotaka UTOAJI WA MIMBA UHALALISHWE?............maisha yatakuwaje baada ya kuhalalisha mauaji haya YA KIKATILI?
 
Kutoa mimba ni swala la hiali ya mtu azae au asizae.
Binafsi naona maisha yatakuwa bora zaidi maana watu wanaingia garama za kulea viumbe ambavyo havikustaili kuwepo duniani vinapata taabu na kutaabika kama kutupwa,kukosa malezi,kukosa chakula,kukosa elimu bora,kukosa pakulala n.k
Kwa hiyo utoaji mimba naona utatusaidia sana kupima kabla kukiacha kiumbe kitoke duniani tutaweza kikimudu na kikitunza?Kama huweni bora kuishusha tu mimba hiyo.
 
kutoa mimba ni swala la hiali ya mtu azae au asizae.
Binafsi naona maisha yatakuwa bora zaidi maana watu wanaingia garama za kulea viumbe ambavyo havikustaili kuwepo duniani vinapata taabu na kutaabika kama kutupwa,kukosa malezi,kukosa chakula,kukosa elimu bora,kukosa pakulala n.k
kwa hiyo utoaji mimba naona utatusaidia sana kupima kabla kukiacha kiumbe kitoke duniani tutaweza kikimudu na kikitunza?kama huweni bora kuishusha tu mimba hiyo.

baba kuna viumbe ambavyo havikustahili kuwa duniani?
 
Kutoa mimba=kupunguza matumizi ya kondom=kuenea kwa vvu.
Yaelekea watu wanaogopa mimba zaidi ya vvu, Kwani kama watu wangezingatia ngono salama, mimba zisingekuwepo na mjadala usingekuwepo pia
 
Kutoa mimba ni swala la hiali ya mtu azae au asizae.
Binafsi naona maisha yatakuwa bora zaidi maana watu wanaingia garama za kulea viumbe ambavyo havikustaili kuwepo duniani vinapata taabu na kutaabika kama kutupwa,kukosa malezi,kukosa chakula,kukosa elimu bora,kukosa pakulala n.k
Kwa hiyo utoaji mimba naona utatusaidia sana kupima kabla kukiacha kiumbe kitoke duniani tutaweza kikimudu na kikitunza?Kama huweni bora kuishusha tu mimba hiyo.

Hiyo hiari inakuwepo kabla hiyo mimba haijatungwa. Hayo maelezo yako kwa maana nyingine yanamaanisha "tulegalise" kuua kwa sababu sioni tofauti kwa vile tu hicho kiumbe ni kidogo hakiwezi kujitetea. Mtaani wanadanganyana ni damu tu, hapana ni kiumbe chenye roho
 
Bora tu kuhalalisha..kwani wangapi wanakufa ktk utoaji mimba kiholela tu mitaani??

Uliza madaktari bongo ni mimba ngapi inatolewa kwa siri Tz..na wangapi pia wanatolea vichochoroni..na kuharibu kizazi??

Heri itolewe kwa usalama hospitalini!
 
Duuu nadhani kutoa mimba haifai kabisa na unaweza kuharibu kizazi na mimi siwezi kusapoti hili swala kabisa la kutoa mimba maana baadae mtu unaweza kujuta...
 
hivi na sisi tushafikia katika ile sayansi ya kutumia embryonic stem cells kama wenzetu?
 
Kutoa Mimba ni kuua, sauti ya hiyo damu Itamlilia Mungu muumba wakati wote (Mwanzo 4:9-12)
 
Kutoa mimba=kupunguza matumizi ya kondom=kuenea kwa vvu.
Yaelekea watu wanaogopa mimba zaidi ya vvu, Kwani kama watu wangezingatia ngono salama, mimba zisingekuwepo na mjadala usingekuwepo pia

Hallooooooooo.
Ni ajabu sana maana kwa udadisi na ufuatiliaji wangu watu hawaogopi kupata mimba wala hawaogopi kukutana na miba inayoitwa ukimwi.
Kondom imebaki ni kama biashara tu ya matangazo na wala haijawahi kumkinga binadamu dhidi ya mimba wala miba, na uzinzi kwa kweli unakwenda mbele kama kawaida kiasi kwamba sasa inaonekana matokeo ya uzinzi si ukimwi tena bali mimba na sasa kinachotisha si ukimwi tena ni mimba na sasa serikali inampango wa kuharibu mimba maana hizo ndio tishio. Hii inatayarishiwa sheria.
Watanzania ni watu wa ajabu sana.
 
Duuu nadhani kutoa mimba haifai kabisa na unaweza kuharibu kizazi na mimi siwezi kusapoti hili swala kabisa la kutoa mimba maana baadae mtu unaweza kujuta...

Vizazi vinaharibika kwasababu utoaji unafanyika kiholela, ingekua inafanyika kitaalamu hilo tatizo lingepungua sana.
 
Back
Top Bottom