Nauliza hizo pesa wanatoaga wapi ukifa na je ndugu zako watachukua muda gani kugawana Mali zako

Nauliza hizo pesa wanatoaga wapi ukifa na je ndugu zako watachukua muda gani kugawana Mali zako

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Ukiumwa ndugu zako hawata kuchangia wala kukupa msaada wakidai hawana kitu, ila ukifa watasafiri kutoka mbali kuja kukuzika tena wakiwa na vitu kwaajili ya kumaliza kilio chako

hizo pesa za usafiri sijui wanatoaga wapi, hii inanikumbusha ule usemi wa kwamba unaweza ukafa Kwa njaa alafu siku ya msiba wako wakapika pilau nyingi watu wakala na kusaza na wengine wakilalamika kuwa pilau haina nyama
 
Tafuta pesa, kata bima, ule vizuri, kunywa maji mengi, usivute sigara na shisha,


Habari za kuumwa kutembeza bakuli sio nzuri kabisaaaa
 
Jamaa anataka iwe kazi ya watu wengine kumtibu,

Kujitibu ni jukumu lako aiseee
hawa ndo wale wazazi wa generation Z ,WAJAMAA sana. Nyerere aliwadekeza na vitu vya bure
bure hakuna
na suala la kusaidiana kama hamjalijenga kifamilia inakuwa ngumu
 
Waafrica hauwajui vizuri mkuu wewe?.

Ni vizuri Kama Unafanya kazi ujitunze na ujiwekee akiba

Kula vizuri
Lala mapema
Usinywe pombe Sana
Sigara bangi acha
Uzinzi acha.
Kujichua acha

Fanya maombi Sana .

Kata bima ya afya
Bima ya chakula
Bima ya nyumba na biashara.
 
Nadhani sababu kubwa ni ujinga, mashaka na ubinafsi.

Mtu anapoumwa wengi hujidanganya wakidhani huenda tatizo siyo serious kiasi cha kumpeleka mgonjwa kaburini.

Mgonjwa anapowatoweka ndipo akili zinawarudi na kujaribu sasa kufidia ile hatia ya uzembe wao ambao pengine ndio ulipelekea umauti.

Si ajabu misiba mingi iliyotokana na upuuzaji wa namna hii ndiyo hasa inahudhuriwa na wengi sana na michango huwa minono mno.

Kuna wengine wanachanga tu kwa lengo la kutunisha mfuko wao wa umaarufu.

Au ni wapi pengine pa kujichukulia pointi tatu za bure kama si kwenye halaiki ya waombolezaji wenye huzuni?

Yote kwa yote, michango misibani ni jambo jema (kama ilivyo kwenye shughuli yoyote halali ya kijamii) - ila ifanyike tu kwa unyofu wa moyo na wala si mikogo na majionesho ya ukwasi.

Kama alivyosema Bwana Yesu Kristu akiwaonya waandishi na Mafarisayo: hayo imewapasa kufanya bila kusahau yale mengine (Mathayo 23).
 
Ukiwa unaishi na watu jitahidi ujue utamaduni wao vizuri.


Waafrica wanapenda matukio social events , ndo maana hujazana katika harusi na misiba.

Waafrica huwa sio watu wakujali MTU
Waafrica ni self -centered (wabinafsi)

Waafrica huwa hawafikirii kesho sio ajabu MTU kupata mshahara leo na ukaisha Leo Leo .

So ukifa utachangiwa Sana na kuzikwa maana hiyo ni social event ambayo mwafrica anaipenda sana.

Hata ukitaka kuoa ni social events watachanga Sana Ila waambie wakupe Ada tu ya VETA haupati.


So endelea kujifunza
 
Waafrica hauwajui vizuri mkuu wewe?.

Ni vizuri Kama Unafanya kazi ujitunze na ujiwekee akiba

Kula vizuri
Lala mapema
Usinywe pombe Sana
Sigara bangi acha
Uzinzi acha.
Kujichua acha

Fanya maombi Sana .

Kata bima ya afya
Bima ya chakula
Bima ya nyumba na biashara.
Sasa mzee amna sex kabisa?
 
Back
Top Bottom