Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Sera za kijamaa.
Hata Soviet mwenyewe ujamaa uliwashinda.

Wananchi walianza kuona mateso, ukigundua kitu hunufaiki inakuwa ni serikali ndio inahusika si wewe.

Hii ilipelekea hata wanasayansi wengi wakimbie kutoka Soviet kuelekea nchi magharibi wakanufaike na kazi zao.
 
Watu wenye roho mbaya ndivyo walivyo uwa wanajijali wenyewe tu na wanapenda sifa na kuabudiwa na ndivyo hali ilivyo hivi sasa nchini mwetu,
Nyerere anaabudiwa kuliko Mwenyezi Mungu aliyetuumba,kila kitu utasikia Mwalimu alisema!
Angalia hata Muungano tulionao ulistahili kabisa muundo wake kupitiwa upya lakini ni kama vile kila kiongozi anaogopa kuchokonoa jambo hilo kwani anaona atauudhi mzimu wa Nyerere sasa labda tusubiri hadi vile vizee vyote vinavyomuabudu huyo bwana mkubwa vife vyote.
 
Miaka yote hii umekuwa mtu mzima; na sijui kama hata shule ulikwenda, bado hata akili ya kutafuta taarifa mwenyewe huna?
Unaeleza umezaliwa miaka ya 1970. Sasa wewe kama mtoto hayo mambo uliyajuaje?
Tueleze ulipata utapia mlo ndiyo maana akili yako ikadumaa kiasi hiki?

Ni waTanzania wangapi walikufa njaa wakati huo, unajuwa? Je, Ethiopia na hapo Kenya, nako Nyerere aliwanyima chakula watu wa huko waliokuwa wakifa kwa njaa?
 
Kama ulizaliwa mwaka 1970 basi by 1985 Nyerere akitoka madarakani ulikuwa na miaka 15.

Hukuwa na akili ya kujua mambo. Endelea kujuzwa na waliokuwepo ili uelimike.

Hakuna Tanzania yenye utulivu huu tulionao bila mchango mkubwa wa baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere
 
Tangu miaka ya 1970 hadi leo maisha yamekubonda unaanza kusingizia marehemu?Huu ni uvivu kamili.Hata dhambi zako utawasingizia wana TANU?Tuache uvivu wa kufanya kazi na akili mdebwedo.😂😂😂
Kweli hata ccm haisababishi umasikini wa watanzania ila INAONGOZA vizuri sana na magaidi yanashugulikiwa
 
Miaka 10 tu mtu anajitambua au wewe ulijitambua ukiwa na miaka 30 mzee
 
Hayati Mwalimu ni Siasa za Ujamaa na Kujitegemea ndio zilimshinda na alishindwa kukiri kuwa zimemshinda na KAMA KAWAIDA YA WATANZANIA WANAKUSHAURI MAMBO UNAYOPENDA KUYASIKIA HUKU WANAKUOGOPA KINAFIKI.
 
Nashindwa kukupa 'like' wewe, hasa kutokana na sifa unazo wapa CCM hii ya leo.
Mwalimu Nyerere asinge sogelea hii CCM iliyopo hii leo kama angekuwa yu hai.
 
1. Ukame
2. Njaa kubwa kuwai kutokea mpaka tukala ugali wa njano
3. Pressure kutoka nchi za maghalibi na taasisi za fedha za kimataifa
4. Vita ya Kagera shughuli zote za uzalishaji nikama zilisimama.
5. Kulipuka kwa gonjwa la ukimwi.
Hzo mbanga zilimpeleka mzee puta hakaona yeye hawezi kukubali masharti ya nchi za maghalibi ikabidi angatuke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…