Naumia sana Mtu wangu wa karibu akifanikiwa, inanidhoofisha mwili

Daa we ni jamaa yangu sana na jana umekuja kunitembelea baafa ya miaka kadhaa ingawa wote tupo Dar hapahapa. Nisingeumwa usingekuja mkuu?
 
Hongera sana,ni Afadhali wewe umefunguka ningekuwa na kazi ningekupa na kukulipa mshahara unaotaka Ila kuna wale ambao hawaongei lakini wapo zaidi yako hao ndio hatari kuliko wewe wale mara nyingi wanakuwa wachawi sana tena. Ila kuna kitu nimejifunza kupitia wewe.
 
Nilidhani ni mimi tu mwenye tatizo hilo😂😂😂 mimi mara nyingi hii tabia inanitokea pindi napouona mkeka ambao sijaufata unataka kuwin, huwa nauombea uchanike
 
Kuna Rafiki yangu mmefanana roho mbaya.
Wewe ni wa kike au? Ukiwa wa kiume nitashangaa maana wanawake ndio wengi wana roho za husda
 
Nilikuwa Nasikia kuna shetani... Leo ndio nimeona shetan kaandika Uzi jamii forum....

We jamaa ni LUCIFER mwenyewe!
 
Learn to Learn from them !! Throw away all the negativity !! This is the way to go, and the bottom line is, you're going to stop them from prospering and moving forward !!
 
Habari za asubuhi hii wakuu, poleni na majukumu ya hapa na pale.

Nina shida kidogo inanikabili ndugu zangu, tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15 kuna hali ndani yangu ambayo sio ya kawaida, iliyonipelekea kuwa na kama ugonjwa wa kudhoofika mwili wangu na akili.

Nina umri wa miaka 38, nina elimu nzuri tu ya degree ya kwanza katika mambo ya utawala. Kwa sasa napitia katika hali ngumu sana ya kiuchumi, tangu nimalize chuo sijawahi kupata kazi katika maisha yangu.

Tangu nikiwa na umri wa miaka 15 ikitokea mwenzangu akifanikiwa roho inaniuma sana. Yaani roho inaniuma mpaka kuna muda nashindwa kula kabisa, ile hali inapelekea kuona kwanini nisifanikiwe mimi kwanini awe huyo mtu?

Ndugu zangu tangu miaka 15 mpaka sasahivi 38 hiyo hali inaniumiza sana, nimepoteza marafiki wengi sana. Nikiona amefanikiwa tu halafu mimi bado nipo hapa hapa nilipo leo basi na namba yake ya simu nafuta na sitaki tena urafiki maana roho inakuwa inanifukuta na kuona mbona mimi nafaa kukaa katika hiyo nafasi, kwanini huyo ndio akae hapo?

Mfano rafiki yangu anaweza kuja kunieleza jambo lake ambalo lipo katika njia ya kufanikiwa, najikuta naumia ndani kwa ndani huku nikimuomba Mungu jambo hilo lifeli (lisifanikiwe) kabisa kwa huyo mtu na ikitokea amefanikiwa basi nakuwa sipo katika hali nzuri.

Rafiki yangu akija kunieleza jambo lake ambalo ni la shida au amepata matatizo fulani kazini au sehemu nyingine, basi roho yangu huwa kama na furaha na ahueni tena nikimuona mtu huyo nimemzidi hata mavazi nakuwa na furaha sana.

Juzi tulienda kufanya mitihani ya utumishi pale DUCE mimi na rafiki yangu mmoja hivi, sasa kwa bahati mbaya mimi sikufanikiwa na yule rafiki yangu akapata nafasi ya ile kazi. Akaja kuniambia malengo yake baada ya hiyo kazi, akasema anataka kwanza avute usafiri wa kutembelea nikajikuta naishiwa nguvu kabisa huku mapigo ya moyo yakienda kasi na kuhisi napoteza fahamu kabisa. Roho iliniuma sana sana sana, nikatamani niende ofisini kwake nikawaambie huyo mtu mliyemchagua hafai kabisa, mfukuzeni.

Kuna rafiki yangu fulani aliniambia kuwa ana mpango wa kuacha kazi afanye biashara, akaniomba nimpe wazo la biashara, nikamuambia anipe muda kidogo. Nikaanza kufanya utafiti kuhusu biashara ambayo ni mbaya sana ambayo mtu akiingia tu huko basi afilisike kabisaaa na achakae vibaya mnooo. Nikapata wazo la biashara ya network marketing basi nikamuunganisha uko, akaingia akaanza hizo biashara pamoja na forex, akaanza uza vitu vyake ili awekeze huko, akaanza kufilisika kidogokidogo, mpaka akaja kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anakaa, hali ilikuwa mbaya sana kwake, mimi moyo wangu ulikuwa na amani tele.

Wakuu hii hali inanitesa sana, mpaka nimeamua kuleta hapa inaniumiza sana, mwezi uliopita nilipata kazi sehemu flani ambayo sio fani niliosomea mshahara ulikuwa ni wa kawaida sana nilisaini mkataba wa malipo, sasa week ya kwanza kazini kuna mfanyakazi moja wakati tunapiga story za hapa na pale akaniambia "kaka unajua nafanya kazi ila mshahara naona hautoshi kabisa", nikamuuliza kwani unalipwa sh ngapi akaniambia analipwa pesa ndogo tu, kumbe analipwa kubwa zaidi ya kwangu, mimi nilisaini mkataba wa laki 4 na nusu, yeye analipwa milion 1 na laki 2, nilijikuta roho imeniuma vibaya mnoo nikajikaza tu, nikaanza kumshawishi kama ana akiba afanye biashara aachane na sifa zote ulizoeleza hapo ni wasifu wa Mchawi ile kazi huku roho ikiniambia aondoke ili mimi nikamate ile nafasi pale kazini.

Nilijaribu sana kumsisitiza aache ile kazi akafanye biashara ya kulima tangawizi, niamuambia tangazawizi na vitunguu vinalipa sana. Kiukweli kabisa mwisho wa siku yule kaka alianza kuhisi nafanya jitihada aache kazi, maana nilikuwa naongea na boss namuambia utakaaje na mfanyakazi haridhiki na mshahara wa milion 1.2, boss akaenda kumuambia yule jamaa akaniona mimi mmbea na mnafiki, basi nahisi waanza kuniwekea fitina za kunitoa kazini, yule boss siku iyo kaniita akasema anaona kama sifai kuendelea na mkataba katika kampuni yao kwahiyo anihitaji tena, nilidumu kwenye ile ofisi siku 19 tu (week 2 na siku 5) nikafukuzwa, mpaka naleta hapa kwenu nimepitia mengi san

Kwa kifupi nikiona mtu wangu wa karibu kafanikiwa iwe ni ndugu, jamaa au rafiki basi roho yangu huwa kama inataka kutoka hivi kwa maumivu makali sana.

Ndio hali inayonikabili ndugu zangu, sijui nafanyaje niache, ushauri wenu wakuu.

Habari za asubuhi hii wakuu, poleni na majukumu ya hapa na pale.

Nina shida kidogo inanikabili ndugu zangu, tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15 kuna hali ndani yangu ambayo sio ya kawaida, iliyonipelekea kuwa na kama ugonjwa wa kudhoofika mwili wangu na akili.

Nina umri wa miaka 38, nina elimu nzuri tu ya degree ya kwanza katika mambo ya utawala. Kwa sasa napitia katika hali ngumu sana ya kiuchumi, tangu nimalize chuo sijawahi kupata kazi katika maisha yangu.

Tangu nikiwa na umri wa miaka 15 ikitokea mwenzangu akifanikiwa roho inaniuma sana. Yaani roho inaniuma mpaka kuna muda nashindwa kula kabisa, ile hali inapelekea kuona kwanini nisifanikiwe mimi kwanini awe huyo mtu?

Ndugu zangu tangu miaka 15 mpaka sasahivi 38 hiyo hali inaniumiza sana, nimepoteza marafiki wengi sana. Nikiona amefanikiwa tu halafu mimi bado nipo hapa hapa nilipo leo basi na namba yake ya simu nafuta na sitaki tena urafiki maana roho inakuwa inanifukuta na kuona mbona mimi nafaa kukaa katika hiyo nafasi, kwanini huyo ndio akae hapo?

Mfano rafiki yangu anaweza kuja kunieleza jambo lake ambalo lipo katika njia ya kufanikiwa, najikuta naumia ndani kwa ndani huku nikimuomba Mungu jambo hilo lifeli (lisifanikiwe) kabisa kwa huyo mtu na ikitokea amefanikiwa basi nakuwa sipo katika hali nzuri.

Rafiki yangu akija kunieleza jambo lake ambalo ni la shida au amepata matatizo fulani kazini au sehemu nyingine, basi roho yangu huwa kama na furaha na ahueni tena nikimuona mtu huyo nimemzidi hata mavazi nakuwa na furaha sana.

Juzi tulienda kufanya mitihani ya utumishi pale DUCE mimi na rafiki yangu mmoja hivi, sasa kwa bahati mbaya mimi sikufanikiwa na yule rafiki yangu akapata nafasi ya ile kazi. Akaja kuniambia malengo yake baada ya hiyo kazi, akasema anataka kwanza avute usafiri wa kutembelea nikajikuta naishiwa nguvu kabisa huku mapigo ya moyo yakienda kasi na kuhisi napoteza fahamu kabisa. Roho iliniuma sana sana sana, nikatamani niende ofisini kwake nikawaambie huyo mtu mliyemchagua hafai kabisa, mfukuzeni.

Kuna rafiki yangu fulani aliniambia kuwa ana mpango wa kuacha kazi afanye biashara, akaniomba nimpe wazo la biashara, nikamuambia anipe muda kidogo. Nikaanza kufanya utafiti kuhusu biashara ambayo ni mbaya sana ambayo mtu akiingia tu huko basi afilisike kabisaaa na achakae vibaya mnooo. Nikapata wazo la biashara ya network marketing basi nikamuunganisha uko, akaingia akaanza hizo biashara pamoja na forex, akaanza uza vitu vyake ili awekeze huko, akaanza kufilisika kidogokidogo, mpaka akaja kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anakaa, hali ilikuwa mbaya sana kwake, mimi moyo wangu ulikuwa na amani tele.

Wakuu hii hali inanitesa sana, mpaka nimeamua kuleta hapa inaniumiza sana, mwezi uliopita nilipata kazi sehemu flani ambayo sio fani niliosomea mshahara ulikuwa ni wa kawaida sana nilisaini mkataba wa malipo, sasa week ya kwanza kazini kuna mfanyakazi moja wakati tunapiga story za hapa na pale akaniambia "kaka unajua nafanya kazi ila mshahara naona hautoshi kabisa", nikamuuliza kwani unalipwa sh ngapi akaniambia analipwa pesa ndogo tu, kumbe analipwa kubwa zaidi ya kwangu, mimi nilisaini mkataba wa laki 4 na nusu, yeye analipwa milion 1 na laki 2, nilijikuta roho imeniuma vibaya mnoo nikajikaza tu, nikaanza kumshawishi kama ana akiba afanye biashara aachane na ile kazi huku roho ikiniambia aondoke ili mimi nikamate ile nafasi pale kazini.

Kwa ufupi tu wewe ni MCHAWI, wasifu ulioutoa hapo ndiyo sifa za MCHAWI na HUTOFANIKIWA KAMWE hadi UACHANE NA SIFA ZA ULOZI.
 
Mm pia ni kama ww mkuu lakini ww umezidi mm Huwa inaniuma sana rafiki zangu wakipata fursa za kupata Hela alaf mm nikose Huwa inaniuma sana kwann wao sio mm ila swala la kuwaombea wafilisike sijui wapoteze kazi mm hapana
 
Mkuu hyo hali unayopitia haupo peke yako,,upo pamoja na genge la wachawi na wanga nyuma yako.,

99% ya binadamu wako hivyo especially sisi waswahili.

Elewa mwenye kufurahia mafanikio yako kwa moyo wote ni,
- wazazi wako
-,, watoto na mke wako..

Wengineo wote wanakuchekea mdomoni lakini moyoni wana maumivu makali sana.
 
Back
Top Bottom