Naumia sana Mtu wangu wa karibu akifanikiwa, inanidhoofisha mwili

Naumia sana Mtu wangu wa karibu akifanikiwa, inanidhoofisha mwili

Mkuu maisha yanakupa tofauti na unavyo plan wewe
Inabid ujue jind ya ku control hyo hari
Kisha taratibu anza kuangalia jindi gan unajikwamua kwenye mafanikio kwakuanza kidoho kidogo
Ikiwa utashindwa kuendesha hisia hizo utaingia kwenye uharifu
 
Tatizo sio WEWE mkuu

Nina uhakika umeishi maisha yasiyokuwa na upendo ama furaha ya kweli,
umeishi maisha ya kulinganishwa na wengine ama kuoneshwa kuwa kuna vitu flani ni lazma uwe navyo ili uwe na thamani kama akili, hadhi flani, Pesa lakini hukufundishwa wewe kama binadamu una thamani gani ukiacha vitu vya kupata na kupoteza katika maisha... ndio maana

Thamani kwako inapimwa katika vitu na kama binadamu yoyote yule ungependa uthaminike zaidi hivyo, unahisi ukikosa na wengine wakipata bhasi thamani yako inashuka kama si kuondoka, kwako na kwa wengine Lakini SI KWELI

Kuna vitu kama moyo mzuri unaowapa wengine tumaini na faraja, Busara zinazowasaidia watu kufanya maamuzi sahihi, Ucheshi unaowasahaulisha watu matatizo kwa muda na vingine vingi ambavyo huwafanya watu wengi kupendwa na kuthaminiwa na watu wengi

Hivi vyote vinakupa uthamani mkubwa sana na pengine marafiki zako wanaviona kwako kwa hizo acting unazofanya ndio maana wanakuja kwako pasipo kujua ni FAKE.. BADILIKA

Jifunze kuona thamani yako au ya watu wengine kwa ubinadamu wao na si kwa vitu wanavyomiliki. Mwisho wa siku utajipenda, utajikubali na kujithamini ulivyo na automatically utafanya kwa wengine hivyo pia mkuu.. JARIBU KUBADILIKA MAANA INAWEZEKANA
 
Jitahidi kuwaunga mkono waliofanikiwa nawe mungu atakufungulia milango
 
Hapana huyu anatakiwa abakie hivyo hivyo akifanikiwa atakua ana roho mbaya mara dufu, ataumiza wanyonge, atawaona wasiofanikiwa hawana akili kiufupi atakua mnyanyasaji na katili wa ajabu,
Aendelee kukaa hapo alipo azidi kuumizwa na mafanikio ya wenzie.
Jamaa sounds like Jiwe
 
Huyu jamaa asipopona huu ugonjwa anaenda kuroga na kuua kabisa


Ana roho ya shetani rohoni kwake POLE Kazia hapo hapo mwana[emoji1787][emoji1787]
 
Tiba yako ni kufanikiwa, umiza kichwa zaidi mpaka na wewe utoboe.
Na hatofanikiwa kwa sababu badala akili yake iwazenamna Bora ya kufanya kazi anawaza Mambo mabaya kwa wenzake
Ubongo haufanyi kazi namna hyo
Akitaka kufanikiw atoe mawazo mabaya kichwani
 
Aisee kwanza pole sana wivu kila mtu anao,
Ila mwenzako akifanikiwa usifikie hatua ya kumuwazia vibaya sana unafunga riziki zako mwenyewe, hebu jaribu kwenda kanisani hii yote ni sababu unakaa mbali na Mungu..
Na watu was namna hyo wapo
Mtu anakuchekea kumbe moyoni anawaza kukumaliza
Acha aendelee kudhoofika mwili
Atakapokutana na kansa na magonjwa mengine yanayosababishwa na vinyongo atashika adabu
 
Habari za asubuhi hii wakuu, poleni na majukumu ya hapa na pale.

Nina shida kidogo inanikabili ndugu zangu, tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15 kuna hali ndani yangu ambayo sio ya kawaida, iliyonipelekea kuwa na kama ugonjwa wa kudhoofika mwili wangu na akili.

Nina umri wa miaka 38, nina elimu nzuri tu ya degree ya kwanza katika mambo ya utawala. Kwa sasa napitia katika hali ngumu sana ya kiuchumi, tangu nimalize chuo sijawahi kupata kazi katika maisha yangu.

Tangu nikiwa na umri wa miaka 15 ikitokea mwenzangu akifanikiwa roho inaniuma sana. Yaani roho inaniuma mpaka kuna muda nashindwa kula kabisa, ile hali inapelekea kuona kwanini nisifanikiwe mimi kwanini awe huyo mtu?

Ndugu zangu tangu miaka 15 mpaka sasahivi 38 hiyo hali inaniumiza sana, nimepoteza marafiki wengi sana. Nikiona amefanikiwa tu halafu mimi bado nipo hapa hapa nilipo leo basi na namba yake ya simu nafuta na sitaki tena urafiki maana roho inakuwa inanifukuta na kuona mbona mimi nafaa kukaa katika hiyo nafasi, kwanini huyo ndio akae hapo?

Mfano rafiki yangu anaweza kuja kunieleza jambo lake ambalo lipo katika njia ya kufanikiwa, najikuta naumia ndani kwa ndani huku nikimuomba Mungu jambo hilo lifeli (lisifanikiwe) kabisa kwa huyo mtu na ikitokea amefanikiwa basi nakuwa sipo katika hali nzuri.

Rafiki yangu akija kunieleza jambo lake ambalo ni la shida au amepata matatizo fulani kazini au sehemu nyingine, basi roho yangu huwa kama na furaha na ahueni tena nikimuona mtu huyo nimemzidi hata mavazi nakuwa na furaha sana.

Juzi tulienda kufanya mitihani ya utumishi pale DUCE mimi na rafiki yangu mmoja hivi, sasa kwa bahati mbaya mimi sikufanikiwa na yule rafiki yangu akapata nafasi ya ile kazi. Akaja kuniambia malengo yake baada ya hiyo kazi, akasema anataka kwanza avute usafiri wa kutembelea nikajikuta naishiwa nguvu kabisa huku mapigo ya moyo yakienda kasi na kuhisi napoteza fahamu kabisa. Roho iliniuma sana sana sana, nikatamani niende ofisini kwake nikawaambie huyo mtu mliyemchagua hafai kabisa, mfukuzeni.

Kuna rafiki yangu fulani aliniambia kuwa ana mpango wa kuacha kazi afanye biashara, akaniomba nimpe wazo la biashara, nikamuambia anipe muda kidogo. Nikaanza kufanya utafiti kuhusu biashara ambayo ni mbaya sana ambayo mtu akiingia tu huko basi afilisike kabisaaa na achakae vibaya mnooo. Nikapata wazo la biashara ya network marketing basi nikamuunganisha uko, akaingia akaanza hizo biashara pamoja na forex, akaanza uza vitu vyake ili awekeze huko, akaanza kufilisika kidogokidogo, mpaka akaja kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anakaa, hali ilikuwa mbaya sana kwake, mimi moyo wangu ulikuwa na amani tele.

Wakuu hii hali inanitesa sana, mpaka nimeamua kuleta hapa inaniumiza sana, mwezi uliopita nilipata kazi sehemu flani ambayo sio fani niliosomea mshahara ulikuwa ni wa kawaida sana nilisaini mkataba wa malipo, sasa week ya kwanza kazini kuna mfanyakazi moja wakati tunapiga story za hapa na pale akaniambia "kaka unajua nafanya kazi ila mshahara naona hautoshi kabisa", nikamuuliza kwani unalipwa sh ngapi akaniambia analipwa pesa ndogo tu, kumbe analipwa kubwa zaidi ya kwangu, mimi nilisaini mkataba wa laki 4 na nusu, yeye analipwa milion 1 na laki 2, nilijikuta roho imeniuma vibaya mnoo nikajikaza tu, nikaanza kumshawishi kama ana akiba afanye biashara aachane na ile kazi huku roho ikiniambia aondoke ili mimi nikamate ile nafasi pale kazini.

Nilijaribu sana kumsisitiza aache ile kazi akafanye biashara ya kulima tangawizi, niamuambia tangazawizi na vitunguu vinalipa sana. Kiukweli kabisa mwisho wa siku yule kaka alianza kuhisi nafanya jitihada aache kazi, maana nilikuwa naongea na boss namuambia utakaaje na mfanyakazi haridhiki na mshahara wa milion 1.2, boss akaenda kumuambia yule jamaa akaniona mimi mmbea na mnafiki, basi nahisi waanza kuniwekea fitina za kunitoa kazini, yule boss siku iyo kaniita akasema anaona kama sifai kuendelea na mkataba katika kampuni yao kwahiyo anihitaji tena, nilidumu kwenye ile ofisi siku 19 tu (week 2 na siku 5) nikafukuzwa, mpaka naleta hapa kwenu nimepitia mengi san

Kwa kifupi nikiona mtu wangu wa karibu kafanikiwa iwe ni ndugu, jamaa au rafiki basi roho yangu huwa kama inataka kutoka hivi kwa maumivu makali sana.

Ndio hali inayonikabili ndugu zangu, sijui nafanyaje niache, ushauri wenu wakuu.
Utakapoachana na huo wivu au husda, nina uhakika milango yako itafunguka.
Chukulia tangu miaka 20 iliyopita, usingefuta namba za waliofanikiwa, hivi wasingekupa mchongo wa wapi kuna ajira au kukupigia ndogo na wewe upate ajira je pengine wasingetokea wa kuweza kukukopa na wewe upate mtaji wa kuanzisha shughuli yako?
 
Aisee wewe ndie mwenyekiti wa ile kamati ya roho mbaya, hatimaye tumekufahamu.
Wakati niko O level mzee aliniombea nikakae nyumbani kwa rafiki yake, ambaye pia alikuwa na kijana wake tunasoma shule moja. Aisee mkewe alikuwa ana roho mbaya, yaani tukifanya test nikimshinda mtoto wake mama anakasirika ile mbaya, nikifeli anafurahi. Kuna kipindi ilikuwa inakaribia mitihani ya kufunga muhula nikaumwa malaria mpaka nikalazwa, huku paper zinakaribia, yaani akawa anafurahi ile mbaya, anamwambia mtoto soma sasa ili umzidi mwezio. Nilipotoka hospital baada ya siku 2 tukaanza mitihani, na majibu kutoka nimempita kwa mbaali mtoto wake, aloo alininunia wiki nzima.
 
Wengi watakushushua kama walivyofanya comment zilizopita ila..

Elewa kwamba kila mwaadamu ana Uselfish(Umimi) anatamani vitu vizuri apate yeye tu referring tukio la kaini na abel na tukio la Watoto wa Yakobo nk.
Hakuna anayefurahi akisikia mtu fulani kafanikiwa vitu hua inamuuma kwanza hafu ndio anafurahia mafanikio yako huku akipoga hesabu jinsi ya kunufaika na mafanikio yako.

By nature mwanadamu hakuumbwa kumiliki mali alitakiwa atafute apate atumie atafute tena..Tabia ya kutaka kumiliki mali ndio imechagiza zaidi watu kua wabinafsi...Watu wanatoana roho vita kila siku kugombania Mafuta,Dhahabu nk nk.

Hivyo basi mkuu kama unasikia kinyongo mtu akifanikiwa then Hali hiyo inaisha at a time basi haina shida kabisa upo sawa. Ila kama inakuHaunt kabiiisa hadi unakosa amani hivyo mental yako ipo damaged kiaisi kikubwa anza kuishughulikia. Jiambie ni kawaida mtu kupata mafanikio hata ww unaweza kupata huo ni muda wake.. potezea kabisa habari za mafanikio ya mtu.
Kila kitu kinaanzia akilini mwako (Your mind not Brain)
Wahindi au Wachaga ukienda dukani kwake kununua kitu na ikawa hana, hakuambii hana anampigia mwenzake akilete fasta na biashara inafanyika. Hivi huyu ataweza kufanya hivyo kweli?
 
Ulipsema haujawahi kupata kazi hata siku moja, halafu ukaja tena kusema ulipata kazi sehemu fulani..., nikaacha kusoma
 
Wakuu hii hali inanitesa sana, mpaka nimeamua kuleta hapa inaniumiza sana, mwezi uliopita nilipata kazi sehemu flani ambayo sio fani niliosomea mshahara ulikuwa ni wa kawaida sana nilisaini mkataba wa malipo, sasa week ya kwanza kazini kuna mfanyakazi moja wakati tunapiga story za hapa na pale akaniambia "kaka unajua nafanya kazi ila mshahara naona hautoshi kabisa", nikamuuliza kwani unalipwa sh ngapi akaniambia analipwa pesa ndogo tu, kumbe analipwa kubwa zaidi ya kwangu, mimi nilisaini mkataba wa laki 4 na nusu, yeye analipwa milion 1 na laki 2, nilijikuta roho imeniuma vibaya mnoo nikajikaza tu, nikaanza kumshawishi kama ana akiba afanye biashara aachane na ile kazi huku roho ikiniambia aondoke ili mimi nikamate ile nafasi pale kazini.

Nilijaribu sana kumsisitiza aache ile kazi akafanye biashara ya kulima tangawizi, niamuambia tangazawizi na vitunguu vinalipa sana. Kiukweli kabisa mwisho wa siku yule kaka alianza kuhisi nafanya jitihada aache kazi, maana nilikuwa naongea na boss namuambia utakaaje na mfanyakazi haridhiki na mshahara wa milion 1.2, boss akaenda kumuambia yule jamaa akaniona mimi mmbea na mnafiki, basi nahisi waanza kuniwekea fitina za kunitoa kazini, yule boss siku iyo kaniita akasema anaona kama sifai kuendelea na mkataba katika kampuni yao kwahiyo anihitaji tena, nilidumu kwenye ile ofisi siku 19 tu (week 2 na siku 5) nikafukuzwa, mpaka naleta hapa kwenu nimepitia mengi san
bwana kikoozi tuma na picha yako tukuone mkuu ili tukujuee jinsi ulivyo
 
It's our contact and experience with other people that give our life joyful, meaning and purpose.

Wewe ni mgonjwa kama wagonjwa wengine,unaumwa maradhi makubwa Sana...uanasumbuliwa na husda kitu ambacho imeharibu kabsa moyo na ubongo wako...(psychology nzima ishaharibiwa).

Polee sanaa...tafuta tiba sahihi utapona.
 
Hujawahi kumuonea wivu mkuu wa nchi au hujafkia huko [emoji2955]
 
Nenda kigoma,nenda sumbawanga,nenda tanga malizia na gamboshi kisha rudi Dar andika mganga maarufu wasfitna anapatikana hapa. Utakuwa tajiri mkuu.Nimewahi kukutana na jamaa mmoja alikuwa na roho ngumu akaniaga anaenda tanga kufundishwa uganga wa kuua.Kwa roho yako uchawi unakufaa sana, utakuwa milionea.
Atawaua mpaka wateja wake, kwa mafanikio watakayoyapata kwa kupitia yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom