Hongera sana kwa kuweka wazi na pole pia kwa hiyo changamoto mkuu, kikubwa kama Una imani nenda kanisani au msikitini.
Endapo utakuwa na hofu ya Mungu, Chuki hazitakuwa sehemu yako na utafunikwa na upendo, palipo na upendo hakuna chuki za kuombeana mabaya, Kufurahia kufeli kwa rafki yako ni kiwango cha juu sana cha roho mbaya.
Binafsi nnafanya biashara ila kuna jirani yangu amefanikiwa kuliko mimi, kwahyo kuna vitu ambavyo nnanufaika kupitia yeye, kama vile kunipa vitu ambavyo havitumii baada ya kufanya maboresho na mimi sina kinyongo nae maana kila mtu ana baraka zake, mimi siwezi kuzuia baraka zake.
Nakupongeza tena kwa Mara nyingne kwamba umeweka wazi kitu ambacho kinakusumbua, mwsho ni kwamba kama chuki ulifunza amini hata upendo unaweza kujifunza pia.