Naumia sana Mtu wangu wa karibu akifanikiwa, inanidhoofisha mwili

Naumia sana Mtu wangu wa karibu akifanikiwa, inanidhoofisha mwili

Wivu sio mbaya but unapaswa uuchukue katika positive means ukupe uchungu wa kufight nawe utoboe coz ukiuchukua katika negative hugeuka laana ya kufunga mafanikio yako ndo maana mpaka sasa huna kitu.

Kupenda mafanikio ya wengine huleta baraka ya mafanikio hivyo hujachelewa badilika.
 
Duuuh we jamaa...🤣

Tiba yako inatakiwa iwe na MULTI THERAPY APPROACHES....

1.Dini(imani)
2.Psychotherapy(ushauri)

MWANADAMU huathirika na vitu 2:
1.Nature(vinasaba)

2.Nurture(malezi)
👆👆👆
Ndio yajengayo PERSONALITY NA AFFECT....

Mwana inawezekana pia hujawahi kukaa maskani sana na masela.....

Mwana inawezekana wazazi wako/walezi)/mazingira YALIKUPA OVERCONFIDENCE na mategemeo makubwa maishani...labda walikuambia UKO BRIGHTER NA SMARTEST kwa hiyo huwezi kushindwa....kwa hiyo mazuri YOTE NI YAKO...🤣

Mwana huwenda pia una mapepo/vizuu/majini YASIYOONEKANA....

Mwana pole sana kaka....

Nitaendelea....
 
Hapana huyu anatakiwa abakie hivyo hivyo akifanikiwa atakua ana roho mbaya mara dufu, ataumiza wanyonge, atawaona wasiofanikiwa hawana akili kiufupi atakua mnyanyasaji na katili wa ajabu,
Aendelee kukaa hapo alipo azidi kuumizwa na mafanikio ya wenzie.
.....mara paaap katoboa na kuwa WAZIRI MKUU...🤣🤣🤣🤣
 
Husuda na kijicho ni ile hali ya kutaka mwenzako alichofanya na kupata KIMTOKE NA KUMUONDOKA....

Wivu ni hali ya kawaida ambayo mmoja hutamani kupata na kufanikiwa kama alivyopata mwenzake bila ya kumtakia MABAYA....

Karibu maskani TUBLEZI....
 
Unajua riziki anatoa Mungu, sasa kama umekuwa ukimpinga Mungu na kutokuwa na upendo kwa watu, kibao kinakugeukia. Waombee watu mema nawe pia ujaaliwe mema. Upendo ndio amri kuu ya Mungu kuliko amri zote.
 
Unajua riziki anatoa Mungu, sasa kama umekuwa ukimpinga Mungu, na kutokuwa na upendo kwa watu, kibao kinakugeukia. Waombee watu mema nawe pia ujaaliwe mema. Upendo ndio amri kuu ya Mungu kuliko amri zote.
....labda anataka MAFANIKIO NA MALI ZA DUNIA YOTE angepewa yeye pekee..🤣


Delusion and illusion....
 
Bro wewe ni mchawi. Kamwe huwezi kufanikiwa ukiendekeza hiyo roho yako.
🤣🤣

Ndio mana tunaambiwa tuwe tunasali na kuomba sana majumbani kabla ya kuianza siku ...kwani huenda tunapishana barabarani/MAKAZINI na mabiasharani na watu wengi SAMPULI hiyo.....🤣
 
Naomba Mungu aniondolee Husda,wivu, chuki na majivuno... Nawaombea wengine wapate nawaombea ndugu zangu wote mafanikio...Huu NI UKWELI MTUPU.

Rehma za mwenyezi Mungu humpa amtakae...
Blowing someone else's candle doesn't make yours burn brighter.

Jaribu kujikurubisha NA MUNGU wako...hiyo ndo solution.
Allahumma aamin kwetu sote aaamin.
 
Nilipoanza kusoma nimepata tabu sana kusoma hadi mwisho. Wewe huna tofauti na mchawi wa mchana na usiku. Kwa tabia hii sidhani kama una mafanikio. Kingine nakushauri jitahidi uache tabia hii maana hilo gubu ulilonalo linaweza kukupa ugonjwa wa moyo hata ufe mapema mno.

Tafuta mchungaji akuombee au shehe sio kawaida hii. Huwa najiuliza ukioa mwanamke ukigundua sio bikira si roho itakuuma sana!
 
Wakuu hii hali inanitesa sana, mpaka nimeamua kuleta hapa inaniumiza sana, mwezi uliopita nilipata kazi sehemu flani ambayo sio fani niliosomea mshahara ulikuwa ni wa kawaida sana nilisaini mkataba wa malipo, sasa week ya kwanza kazini kuna mfanyakazi moja wakati tunapiga story za hapa na pale akaniambia "kaka unajua nafanya kazi ila mshahara naona hautoshi kabisa", nikamuuliza kwani unalipwa sh ngapi akaniambia analipwa pesa ndogo tu, kumbe analipwa kubwa zaidi ya kwangu, mimi nilisaini mkataba wa laki 4 na nusu, yeye analipwa milion 1 na laki 2, nilijikuta roho imeniuma vibaya mnoo nikajikaza tu, nikaanza kumshawishi kama ana akiba afanye biashara aachane na ile kazi huku roho ikiniambia aondoke ili mimi nikamate ile nafasi pale kazini.

Nilijaribu sana kumsisitiza aache ile kazi akafanye biashara ya kulima tangawizi, niamuambia tangazawizi na vitunguu vinalipa sana. Kiukweli kabisa mwisho wa siku yule kaka alianza kuhisi nafanya jitihada aache kazi, maana nilikuwa naongea na boss namuambia utakaaje na mfanyakazi haridhiki na mshahara wa milion 1.2, boss akaenda kumuambia yule jamaa akaniona mimi mmbea na mnafiki, basi nahisi waanza kuniwekea fitina za kunitoa kazini, yule boss siku iyo kaniita akasema anaona kama sifai kuendelea na mkataba katika kampuni yao kwahiyo anihitaji tena, nilidumu kwenye ile ofisi siku 19 tu (week 2 na siku 5) nikafukuzwa, mpaka naleta hapa kwenu nimepitia mengi sana.
 
Nilipoanza kusoma nimepata tabu sana kusoma hadi mwisho.Wewe huna tofauti na mchawi wa mchana na usiku.Kwa tabia hii sidhani kama una mafanikio.Kingine nakushauri jitahidi uache tabia hii maana hilo gubu ulilonalo linaweza kukupa ugonjwa wa moyo hata ufe mapema mno.
Tafuta mchungaji akuombee au shehe sio kawaida hii.Huwa najiuliza ukioa mwanamke ukigundua sio bikira si roho itakuuma sana!
.....akigundua si "birkaa" Anaweza kulalamikia hilo mpaka anafika miaka 100🤣🤣
 
Hapana huyu anatakiwa abakie hivyo hivyo akifanikiwa atakua ana roho mbaya mara dufu, ataumiza wanyonge, atawaona wasiofanikiwa hawana akili kiufupi atakua mnyanyasaji na katili wa ajabu,
Aendelee kukaa hapo alipo azidi kuumizwa na mafanikio ya wenzie.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom