Naumia sana Mtu wangu wa karibu akifanikiwa, inanidhoofisha mwili

Wivu ni kawaida, ila badilisha wivu wako uwe katika positive side, mfurahie aliyefanikiwa huku ukiamini kuna kitu utajifunza kutoka kwake ambacho kitakuvusha hapo ulipo, badilisha attitude...waza vitu vizuri, Waza kufanikiwa, wawazie rafiki zako vitu vizuri huku ukiamini mafanikio yao, yatakuwa daraja kwako kwa namna moja au nyingine...
Life is too short!! Ujaze moyo wako furaha.
 
Nenda kwa wanasaikolojia wa kutibu ilo tatizo. Uenda kukosa kwako kazi na kutofanikiwa kwako kunatokana na hiyo tabia yako. Marafiki wana msaada mkubwa sana kwenye ku-network kama ukiishi nao vizuri. Duniani tunategemeana uwezi toba ukiwa peke yako au ukiwa na roho uliyo nayo.

Utakosa msaada kwa roho yako mbaya, utakosa pa kukimbilia wakati wa shida kwa roho yako. Wenzako tunakesha tukiomba watu wa karibu wafanikiwe ili tuweze kupata michongo ya kufanikiwa kupitia wao.

Unaona wale kina Polepole wanateuliwa kuwa wabunge au watu wanateuliwa kuwa mawaziri ile ni kwa kuwa Rais anawajua so amepata nafasi ya kuwa Rais nae anawateua ili afanye nao kazi. Sasa wewe kama rafiki yako akiwa Rais badala ufurahi unaweza kupewa nafasi unaanza kukonda mwisho wa siku kwa kuwa chuki haijifichi unaachwa. Nimekupa mfano wa Rais lakini unaweza kujiweka katika level yako
 
Habari za asubuhi hii wakuu, poleni na majukumu ya hapa na pale.

Nina shida kidogo inanikabili ndugu zangu, tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15 kuna hali ndani yangu ambayo sio ya kawaida, iliyonipelekea kuwa na kama ugonjwa wa kudhoofika mwili wangu na akili.

Nina umri wa miaka 38, nina elimu nzuri tu ya degree ya kwanza katika mambo ya utawala. Kwa sasa napitia katika hali ngumu sana ya kiuchumi, tangu nimalize chuo sijawai kupata kazi katika maisha yangu.

Tangu nikiwa na umri wa miaka 15 ikitokea mwenzangu akifanikiwa roho inaniuma sana. Yaani roho inaniuma mpaka kuna muda nashindwa kula kabisa, ile hali inapelekea kuona kwanini nisifanikiwe mimi kwanini awe huyo mtu?

Ndugu zangu tangu miaka 15 mpaka sasaivi 38 iyo hali inaniumiza sana, nimepoteza marafiki wengi sana. Nikiona amefanikiwa tu halafu mimi bado nipo hapa hapa nilipo leo basi na namba yake ya simu nafuta na sitaki tena urafiki maana roho inakuwa inanifukuta na kuona mbona mimi nafaa kukaa katika hiyo nafasi, kwanini huyo ndio akae hapo?

Mfano rafiki yangu anaweza kuja kunieleza jambo lake ambalo lipo katika njia ya kufanikiwa, najikuta naumia ndani kwa ndani huku nikimuomba mungu jambo ilo lifeli (lisifanikiwe) kabisa kwa huyo mtu, na ikitokea amefanikiwa basi nakuwa sipo katika hali nzuri.

Rafiki yangu akija kunieleza jambo lake ambalo ni la shida au amepata matatizo fulani kazini au sehemu nyingine, basi roho yangu huwa kama na furaha na ahueni tena nikimuona mtu huyo nimemzidi hata mavazi nakuwa na furaha sana.

Juzi tulienda kufanya mitihani ya utumishi pale DUCE mimi na rafiki yangu mmoja hivi, sasa kwa bahati mbaya mimi sikufanikiwa na yule rafiki yangu akapata nafasi ya ile kazi. Akaja kuniambia malengo yake baada ya hiyo kazi, akasema anataka kwanza avute usafiri wa kutembelea nikajikuta naishiwa nguvu kabisa huku mapigo ya moyo yakienda kasi na kuhisi napoteza fahamu kabisa. Roho iliniuma sana sana sana, nikatamani niende ofisini kwake nikawaambie huyo mtu mliyemchagua hafai kabisa, mfukuzeni.

Kuna rafiki yangu fulani aliniambia kuwa ana mpango wa kuacha kazi afanye biashara, akaniomba nimpe wazo la biashara, nikamuambia anipe muda kidogo. Nikaanza kufanya utafiti kuhusu biashara ambayo ni mbaya sana ambayo mtu akiingia tu huko basi afilisike kabisaaa na achakae vibaya mnooo. Nikapata wazo la biashara ya network marketing basi nikamuunganisha uko, akaingia akaanza izo biashara pamoja na forex, akaanza uza vitu vyake ili awekeze uko, akaanza kufilisika kidogokidogo, mpaka akaja kufukuzwa kwenye nyumba aliyekuwa anakaa, hali ilikuwa mbaya sana kwake, mimi moyo wangu ulikuwa na amani tele.

Kwa kifupi nikiona mtu wangu wa karibu kafanikiwa iwe ni ndugu, jamaa au rafiki basi roho yangu huwa kama inataka kutoka hivi kwa maumivu makali sana.

Ndio hali inayo nikabili ndugu zangu, sijui nafanyaje niache, ushauri wenu wakuu.
Ndugu kwa kuwa umelifahamu tatizo na kujitambua ni hatua nzuri. Umejieleza sana jinsi ulivyo na kuwa shetani anatawala akili na moyo wako. Ni jambo jema sana kujitambua.

Kinachokwamisha maendeleo yako ni hiyo roho mbaya. Jitahidi sana na uombe sana kwa imani yako hali hiyo itoke na utafanikiwa. Tambua tunaongozwa na roho. Ulishajiuliza roho inayofurahia mwenzako kupata matatizo ni roho ya namna gani. Bila shaka ni shetani. Sasa chukua hatua, achana na roho hiyo kisha utaona baraka zinakuja na kumiminika.

Kwa ufupi badilika na dhamiria kutenda mema ukiikataa hiyo roho chafu
 
Mkuu huwezi fanikiwa milele kwa roho ya dizain hii,
Kuwa na roho ya kutoa then mungu atakuzidishia pale unapotoa.
 
Tatizo lako ni kubwa sana by the way unafaa kuwa jambazi, serial killer, mvuvi mchimba madini ama mortuary attendant hutakiwi kukaa na watoto wadogo utakaem.uoa atakusaliti sana sababu ya attitude yako. Inequality za kuwa panya road, alishabab members.. .jitahidi usichangamane na watu WA kawaida.

Naongea very seriously huitaji kutiwa moyo Ukweli ni kuwa desire zako ziko Juu sana kwenye majeshi nyie ndio huwa WA kwanza kuuliwa sababu ya mentality ya kufanya mapinduzi na makazini huwa ni watu WA kujipendekeza sana kwa kuhisi wanafaa na kujua kila kitu kuliko hata kiongozi wako.

Desire zako ziko Juu sana ni rahisi kujidhuru.. ..Tatizo lako linaweza kuondolewa kwa kupewa Tatizo mbadala sababu ni above average of ordinary human beings hata wachawi hawako na desire ya Juu hivi ndio sababu anaweza kukuloga na akaja kukupa pole kwa kuugua.
 
Wengi watakushushua kama walivyofanya comment zilizopita ila..

Elewa kwamba kila mwaadamu ana Uselfish(Umimi) anatamani vitu vizuri apate yeye tu referring tukio la kaini na abel Watoto wa Yakobo nk.
Hakuna anayefurahi akisikia mtu fulani kafanikiwa vitu hua inamuuma kwanza hafu ndio anafurahia mafanikio yako huku akipoga hesabu jinsi ya kunufaika na mafanikio yako.

By nature mwanadamu hakuumbwa kumiliki mali alitakiwa atafute apate atumie atafute tena..Tabia ya kutaka kumiliki mali ndio imechagiza zaidi watu kua wabinafsi...Watu wanatoana roho vita kila siku kugombania Mafuta,Dhahabu nk nk.

Hivyo basi mkuu kama unasikia kinyongo mtu akifanikiwa then Hali hiyo inaisha at a time basi haina shida kabisa upo sawa. Ila kama inakuHaunt kabiiisa hadi unakosa amani hivyo mental yako ipo damaged kiaisi kikubwa anza kuishughulikia. Jiambie ni kawaida mtu kupata mafanikio hata ww unaweza kupata huo ni muda wake.. potezea kabisa habari za mafanikio ya mtu.
Kila kitu kinaanzia akilini mwako (Your mind not Brain)
Rekebisha hapo kwa Kaini na Abel mkuu, ni watoto wa Adam

Watu wa dizain ya mtoa mada wanajionaga wao ndo wana akili, wao ndo wanastahili, wao ndo wanajua kila kitu. Wanadhani maisha ya shule/darasani ndo kila kitu maishani. Wanaumia sana wanapoona wenzao wanaowaona ka vikaza wakitoboa.

Wanasahau kuwa ktk maisha kuna bahati, connection, neema ya Mungu halafu ndo uwezo binafsi.

Huyu anahitaji mwanasaikolojia amuweke sawa
 
Uzuri tayari ushajua tatizo lako; sasa ni rahisi kulikabili...tafuta ufanikiwe labda roho itatulia; la muhimu ujue ni vigumu kufanikiwa ukiwa na roho mbaya kwa watu (roho mbaya ufukuzwa na roho mzuri), tenda wema kwa watu.
 
Habari za asubuhi hii wakuu, poleni na majukumu ya hapa na pale.

Nina shida kidogo inanikabili ndugu zangu, tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15 kuna hali ndani yangu ambayo sio ya kawaida, iliyonipelekea kuwa na kama ugonjwa wa kudhoofika mwili wangu na akili.

Nina umri wa miaka 38, nina elimu nzuri tu ya degree ya kwanza katika mambo ya utawala. Kwa sasa napitia katika hali ngumu sana ya kiuchumi, tangu nimalize chuo sijawai kupata kazi katika maisha yangu.

Tangu nikiwa na umri wa miaka 15 ikitokea mwenzangu akifanikiwa roho inaniuma sana. Yaani roho inaniuma mpaka kuna muda nashindwa kula kabisa, ile hali inapelekea kuona kwanini nisifanikiwe mimi kwanini awe huyo mtu?

Ndugu zangu tangu miaka 15 mpaka sasaivi 38 iyo hali inaniumiza sana, nimepoteza marafiki wengi sana. Nikiona amefanikiwa tu halafu mimi bado nipo hapa hapa nilipo leo basi na namba yake ya simu nafuta na sitaki tena urafiki maana roho inakuwa inanifukuta na kuona mbona mimi nafaa kukaa katika hiyo nafasi, kwanini huyo ndio akae hapo?

Mfano rafiki yangu anaweza kuja kunieleza jambo lake ambalo lipo katika njia ya kufanikiwa, najikuta naumia ndani kwa ndani huku nikimuomba mungu jambo ilo lifeli (lisifanikiwe) kabisa kwa huyo mtu, na ikitokea amefanikiwa basi nakuwa sipo katika hali nzuri.

Rafiki yangu akija kunieleza jambo lake ambalo ni la shida au amepata matatizo fulani kazini au sehemu nyingine, basi roho yangu huwa kama na furaha na ahueni tena nikimuona mtu huyo nimemzidi hata mavazi nakuwa na furaha sana.

Juzi tulienda kufanya mitihani ya utumishi pale DUCE mimi na rafiki yangu mmoja hivi, sasa kwa bahati mbaya mimi sikufanikiwa na yule rafiki yangu akapata nafasi ya ile kazi. Akaja kuniambia malengo yake baada ya hiyo kazi, akasema anataka kwanza avute usafiri wa kutembelea nikajikuta naishiwa nguvu kabisa huku mapigo ya moyo yakienda kasi na kuhisi napoteza fahamu kabisa. Roho iliniuma sana sana sana, nikatamani niende ofisini kwake nikawaambie huyo mtu mliyemchagua hafai kabisa, mfukuzeni.

Kuna rafiki yangu fulani aliniambia kuwa ana mpango wa kuacha kazi afanye biashara, akaniomba nimpe wazo la biashara, nikamuambia anipe muda kidogo. Nikaanza kufanya utafiti kuhusu biashara ambayo ni mbaya sana ambayo mtu akiingia tu huko basi afilisike kabisaaa na achakae vibaya mnooo. Nikapata wazo la biashara ya network marketing basi nikamuunganisha uko, akaingia akaanza izo biashara pamoja na forex, akaanza uza vitu vyake ili awekeze uko, akaanza kufilisika kidogokidogo, mpaka akaja kufukuzwa kwenye nyumba aliyekuwa anakaa, hali ilikuwa mbaya sana kwake, mimi moyo wangu ulikuwa na amani tele.

Kwa kifupi nikiona mtu wangu wa karibu kafanikiwa iwe ni ndugu, jamaa au rafiki basi roho yangu huwa kama inataka kutoka hivi kwa maumivu makali sana.

Ndio hali inayo nikabili ndugu zangu, sijui nafanyaje niache, ushauri wenu wakuu.
Duuh pole Sana kwa hali uloyona nayo ya kuhitaji kumuomba Sana mungu akuepushe na hali hiyo,

Kwan hiyo hali inaweza kukupelekea usifanikiwe kamwe , kwani SAA nyingine ili ufanikiwe inakubidi uwe na mahusiano mzuri na waliofanikiwa kabla yako,

Naamini hata ukiajiriwa utakua mtu fulani hivi mnoko mnoko ambaye hupendi kuona uliowakuta wanakuzidi , utatamani uwe hata boss zaidi ya boss wako aliyekuajiri ,

Kingine ww ni mbinafsi omba tu mungu usije kushika uchawi unaweza ukaua watu wengi Sana .

Muombe mungu akuepushe na hali hiyo
 
Kama hutatubu kwa Mungu jiandae kupata ugonjwa wa moyo na pressure.
 
Unapo muombea mwenzako mabaya ndo unazidi mpa baraka na unapomwombea mwenzako mema Mungu pia hukupa mema.Si ajabu hufanikiwi sababu ya roho mbaya,jitahidi kubadilika itakusaidia
 
Habari za asubuhi hii wakuu, poleni na majukumu ya hapa na pale.

Nina shida kidogo inanikabili ndugu zangu, tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15 kuna hali ndani yangu ambayo sio ya kawaida, iliyonipelekea kuwa na kama ugonjwa wa kudhoofika mwili wangu na akili.

Nina umri wa miaka 38, nina elimu nzuri tu ya degree ya kwanza katika mambo ya utawala. Kwa sasa napitia katika hali ngumu sana ya kiuchumi, tangu nimalize chuo sijawai kupata kazi katika maisha yangu.

Tangu nikiwa na umri wa miaka 15 ikitokea mwenzangu akifanikiwa roho inaniuma sana. Yaani roho inaniuma mpaka kuna muda nashindwa kula kabisa, ile hali inapelekea kuona kwanini nisifanikiwe mimi kwanini awe huyo mtu?

Ndugu zangu tangu miaka 15 mpaka sasaivi 38 iyo hali inaniumiza sana, nimepoteza marafiki wengi sana. Nikiona amefanikiwa tu halafu mimi bado nipo hapa hapa nilipo leo basi na namba yake ya simu nafuta na sitaki tena urafiki maana roho inakuwa inanifukuta na kuona mbona mimi nafaa kukaa katika hiyo nafasi, kwanini huyo ndio akae hapo?

Mfano rafiki yangu anaweza kuja kunieleza jambo lake ambalo lipo katika njia ya kufanikiwa, najikuta naumia ndani kwa ndani huku nikimuomba mungu jambo ilo lifeli (lisifanikiwe) kabisa kwa huyo mtu, na ikitokea amefanikiwa basi nakuwa sipo katika hali nzuri.

Rafiki yangu akija kunieleza jambo lake ambalo ni la shida au amepata matatizo fulani kazini au sehemu nyingine, basi roho yangu huwa kama na furaha na ahueni tena nikimuona mtu huyo nimemzidi hata mavazi nakuwa na furaha sana.

Juzi tulienda kufanya mitihani ya utumishi pale DUCE mimi na rafiki yangu mmoja hivi, sasa kwa bahati mbaya mimi sikufanikiwa na yule rafiki yangu akapata nafasi ya ile kazi. Akaja kuniambia malengo yake baada ya hiyo kazi, akasema anataka kwanza avute usafiri wa kutembelea nikajikuta naishiwa nguvu kabisa huku mapigo ya moyo yakienda kasi na kuhisi napoteza fahamu kabisa. Roho iliniuma sana sana sana, nikatamani niende ofisini kwake nikawaambie huyo mtu mliyemchagua hafai kabisa, mfukuzeni.

Kuna rafiki yangu fulani aliniambia kuwa ana mpango wa kuacha kazi afanye biashara, akaniomba nimpe wazo la biashara, nikamuambia anipe muda kidogo. Nikaanza kufanya utafiti kuhusu biashara ambayo ni mbaya sana ambayo mtu akiingia tu huko basi afilisike kabisaaa na achakae vibaya mnooo. Nikapata wazo la biashara ya network marketing basi nikamuunganisha uko, akaingia akaanza izo biashara pamoja na forex, akaanza uza vitu vyake ili awekeze uko, akaanza kufilisika kidogokidogo, mpaka akaja kufukuzwa kwenye nyumba aliyekuwa anakaa, hali ilikuwa mbaya sana kwake, mimi moyo wangu ulikuwa na amani tele.

Kwa kifupi nikiona mtu wangu wa karibu kafanikiwa iwe ni ndugu, jamaa au rafiki basi roho yangu huwa kama inataka kutoka hivi kwa maumivu makali sana.

Ndio hali inayo nikabili ndugu zangu, sijui nafanyaje niache, ushauri wenu wakuu.
Hiyo ni mentality mbaya sana,sasa nakushauri,anza kuangalia,video clips za babu mmoja mhindi anaitwa sadhguru,utajifunza vitu vingi ambavyo vitauondoa huo ugonjwa
 
Jitahidi kuomba kwa imani yako ili hiyo roho ikukimbie..la sivyo utaendelea kuwa na tatizo la kutofanikiwa maisha yako yote.
 
Back
Top Bottom