The Icebreaker
Platinum Member
- Apr 24, 2014
- 39,582
- 123,152
Hata mimi hapa nimefurahi kuona wewe unapigika kimaisha.
😀😀
😀😀
Mkuu kaombewe, una mapepo kama saba hivi ya husda,wivu,tamaa , chuki na hasira na mengine.Habari za asubuhi hii wakuu, poleni na majukumu ya hapa na pale.
Nina shida kidogo inanikabili ndugu zangu, tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15 kuna hali ndani yangu ambayo sio ya kawaida, iliyonipelekea kuwa na kama ugonjwa wa kudhoofika mwili wangu na akili.
Nina umri wa miaka 38, nina elimu nzuri tu ya degree ya kwanza katika mambo ya utawala. Kwa sasa napitia katika hali ngumu sana ya kiuchumi, tangu nimalize chuo sijawai kupata kazi katika maisha yangu.
Tangu nikiwa na umri wa miaka 15 ikitokea mwenzangu akifanikiwa roho inaniuma sana. Yaani roho inaniuma mpaka kuna muda nashindwa kula kabisa, ile hali inapelekea kuona kwanini nisifanikiwe mimi kwanini awe huyo mtu?
Ndugu zangu tangu miaka 15 mpaka sasaivi 38 iyo hali inaniumiza sana, nimepoteza marafiki wengi sana. Nikiona amefanikiwa tu halafu mimi bado nipo hapa hapa nilipo leo basi na namba yake ya simu nafuta na sitaki tena urafiki maana roho inakuwa inanifukuta na kuona mbona mimi nafaa kukaa katika hiyo nafasi, kwanini huyo ndio akae hapo?
Mfano rafiki yangu anaweza kuja kunieleza jambo lake ambalo lipo katika njia ya kufanikiwa, najikuta naumia ndani kwa ndani huku nikimuomba mungu jambo ilo lifeli (lisifanikiwe) kabisa kwa huyo mtu, na ikitokea amefanikiwa basi nakuwa sipo katika hali nzuri.
Rafiki yangu akija kunieleza jambo lake ambalo ni la shida au amepata matatizo fulani kazini au sehemu nyingine, basi roho yangu huwa kama na furaha na ahueni tena nikimuona mtu huyo nimemzidi hata mavazi nakuwa na furaha sana.
Juzi tulienda kufanya mitihani ya utumishi pale DUCE mimi na rafiki yangu mmoja hivi, sasa kwa bahati mbaya mimi sikufanikiwa na yule rafiki yangu akapata nafasi ya ile kazi. Akaja kuniambia malengo yake baada ya hiyo kazi, akasema anataka kwanza avute usafiri wa kutembelea nikajikuta naishiwa nguvu kabisa huku mapigo ya moyo yakienda kasi na kuhisi napoteza fahamu kabisa. Roho iliniuma sana sana sana, nikatamani niende ofisini kwake nikawaambie huyo mtu mliyemchagua hafai kabisa, mfukuzeni.
Kuna rafiki yangu fulani aliniambia kuwa ana mpango wa kuacha kazi afanye biashara, akaniomba nimpe wazo la biashara, nikamuambia anipe muda kidogo. Nikaanza kufanya utafiti kuhusu biashara ambayo ni mbaya sana ambayo mtu akiingia tu huko basi afilisike kabisaaa na achakae vibaya mnooo. Nikapata wazo la biashara ya network marketing basi nikamuunganisha uko, akaingia akaanza izo biashara pamoja na forex, akaanza uza vitu vyake ili awekeze uko, akaanza kufilisika kidogokidogo, mpaka akaja kufukuzwa kwenye nyumba aliyekuwa anakaa, hali ilikuwa mbaya sana kwake, mimi moyo wangu ulikuwa na amani tele.
Kwa kifupi nikiona mtu wangu wa karibu kafanikiwa iwe ni ndugu, jamaa au rafiki basi roho yangu huwa kama inataka kutoka hivi kwa maumivu makali sana.
Ndio hali inayo nikabili ndugu zangu, sijui nafanyaje niache, ushauri wenu wakuu.
True sayingMkuu ili ufanikiwe furahia mafanikio ya wengine nenda kajifunze kwao .Ukiwachukia hautaweza kujifunza kwa walifanikiwa .
Dahh[emoji3][emoji16]Jf forever,
I say Jf forever
Jf forever for life.
Sasa unakwenda kupona maana ushaanza kulijua tatizo lako.
Pepo la uchawi ulilorithishwa na bibi yako ndilo chanzo. Kaombewe lutoke uwe huru
[emoji16]Wakati wenzako wakiwa kitaa wanafight wewe upo class una piga kitabu haya sasa kale vitabu..
IndeedRekebisha hapo kwa Kaini na Abel mkuu, ni watoto wa Adam
Watu wa dizain ya mtoa mada wanajionaga wao ndo wana akili, wao ndo wanastahili, wao ndo wanajua kila kitu. Wanadhani maisha ya shule/darasani ndo kila kitu maishani. Wanaumia sana wanapoona wenzao wanaowaona ka vikaza wakitoboa.
Wanasahau kuwa ktk maisha kuna bahati, connection, neema ya Mungu halafu ndo uwezo binafsi.
Huyu anahitaji mwanasaikolojia amuweke sawa
[emoji16]kmmkHata mimi hapa nimefurahi kuona wewe unapigika kimaisha.
😀😀