Naunga mkono Chipukizi katika siasa na kada zingine

Naunga mkono Chipukizi katika siasa na kada zingine

Nashangaa wanaopinga chipukizi wa CCM ila wanaunga mkono
1. Madrasa
2. Mafundisho kanisani
3. Sunday school

Ukiangalia ideologies za hayo yote juu yanaendana 100%. Wote wanam-brainwash mtoto na kumwaminisha imani ya upande mmoja.

Hao chipukizi ndio watesi wa wapinzani baadaye.

Ni sawa tu na hao wa madrasa na sunday school huwezi waaminisha dini yao ina mapungufu wataona ina haki kuliko zingine.
 
Fafanua,

Ukiondoa WIVU na mkumbo, wanapinga chipukizi hawana HOJA.

Sisi tunaandaa Marais wajao, mawaziri, walimu wajao tangu wakiwa watoto.

Katika masuala yanayogusa USTAWI wa nchi, Rabbon Huwa nimenyooka kama rula!!
Mkuu marais au viongozi kwa ujumla hawaandaliwi kwa kuingia kwenye chipukizi. Chipukizi ilikuwa na njia ya wakomunisti kuanza kuwa-brainwash wananchi tangu wakiwa wadogo. Njia sahihi ya kuandaa viongozi ni watoto kupata makuzi na elimu bora, kuwa na mfumo mzuri wa uongozi wa nchi na viongozi kuwa na maadili mazuri.
 
Salaam, Shalom!!!

I declare interest, Rabbon ni mdau wa watoto, nimekuwa katika kitengo hicho Kwa miaka mingi sasa katika Imani.

Viongozi wapo wa Kuzaliwa Toka tumboni, na wapo wa kufundishwa. Likewise wanasiasa wa Kuzaliwa wasizuiwe.

Katika umri wa kuanzia miaka 4 Hadi mitano, tayari unaweza jua mtoto uliyenaye darasani au nyumbani ana kipaji Gani. KAZI inayobaki ni kukipalilia kipaji na kukiwekea mbolea kikue na kuleta matunda.

Footbollers wanapatikana wakiwa katika umri mdogo kabisa kuanzia miaka 4 na kuendelea, waimbaji,waombaji, engineers, drivers, wachoraji nk nk wanajulikana katika umri mdogo.

Kwakuwa Tanzania kama nchi Ina miaka mingi ijayo, ni muhimu viongozi waandaliwe wakiwa WADOGO kabisa.

Nimefurahi kuona ujasiri wa kujieleza wa mtoto wa Msanii Shetta, hicho ni kipaji, alelewe na atatufaa sana baadaye.

Wakubwa pia Huwa wanakosea, haikuwa sahihi kuzuia chipukizi katika vyama, makazini, katika kwaya, na sekta mbalimbali Kwa kigezo Cha shule.

Watoto wasome, lakini vipaji vyao viendelezwe na kupewa nafasi mapema kuanza kuongoza.

Rabbon tayari ninao walimu watakaokuja kushika nafasi zetu tutakapopumzika, na ni watoto. Wahubiri wazuri tayari wanakuzwa, wapo mashuleni lakini wanajitambua ni akina nani, wapo mashemasi wa watoto kuanzia miaka 8 na kuendelea, wanasoma, lakini siku ya IBADA wanashika zamu zao.

Utaratibu mzuri uwekwe kuwapokea Chipukizi katika kada mbalimbali.

Vyama vingine pia vichangamkie fursa mapema.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen
Upuuzi mtupu tuonyeshe faida zinazoonekana,
badala tutengenezee watoto mitaala mizuri Ili 2040 tuwe na wataalamu wa kurusha satellite
We Unawaza uchipkizi - ujinga ttu
 
Upuuzi mtupu tuonyeshe faida zinazoonekana,
badala tutengenezee watoto mitaala mizuri Ili 2040 tuwe na wataalamu wa kurusha satellite
We Unawaza uchipkizi - ujinga ttu
Kwahiyo watoto wote watarusha satellite?
 
Nashangaa wanaopinga chipukizi wa CCM ila wanaunga mkono
1. Madrasa
2. Mafundisho kanisani
3. Sunday school

Ukiangalia ideologies za hayo yote juu yanaendana 100%. Wote wanam-brainwash mtoto na kumwaminisha imani ya upande mmoja.

Hao chipukizi ndio watesi wa wapinzani baadaye.

Ni sawa tu na hao wa madrasa na sunday school huwezi waaminisha dini yao ina mapungufu wataona ina haki kuliko zingine.
Ndomana sisi walimu wa Imani lazima tutoke mbele kupongeza,

Sababu imeandikwa, Mlee mtoto katika njia impasayo, maana hatoiacha kamwe.

Cha muhimu, itungwe SHERIA Bora kuhakikisha hao chipukizi wanapata mafunzo Bora ,wasifundishwe uhalifu, Bali Uzalendo nk nk.
 
Una uelewa finyi soma Tena nilichokuandikia
Hakuna Mahali nimepinga watoto wasipewe Elimu Bora,

Muhimu ni kuwa, wakiwa katika mfumo huo wa kielimu, wanapata pia fursa ya kuendelea vipaji vyao nk nk.
 
Mkuu marais au viongozi kwa ujumla hawaandaliwi kwa kuingia kwenye chipukizi. Chipukizi ilikuwa na njia ya wakomunisti kuanza kuwa-brainwash wananchi tangu wakiwa wadogo. Njia sahihi ya kuandaa viongozi ni watoto kupata makuzi na elimu bora, kuwa na mfumo mzuri wa uongozi wa nchi na viongozi kuwa na maadili mazuri.
Uko sahihi,

Yote ni muhimu, kinachotakiwa ni Nia na dhamira njema katika kuyatekeleza.
 
Back
Top Bottom