Naunga mkono Chipukizi katika siasa na kada zingine

Nashangaa wanaopinga chipukizi wa CCM ila wanaunga mkono
1. Madrasa
2. Mafundisho kanisani
3. Sunday school

Ukiangalia ideologies za hayo yote juu yanaendana 100%. Wote wanam-brainwash mtoto na kumwaminisha imani ya upande mmoja.

Hao chipukizi ndio watesi wa wapinzani baadaye.

Ni sawa tu na hao wa madrasa na sunday school huwezi waaminisha dini yao ina mapungufu wataona ina haki kuliko zingine.
 
Fafanua,

Ukiondoa WIVU na mkumbo, wanapinga chipukizi hawana HOJA.

Sisi tunaandaa Marais wajao, mawaziri, walimu wajao tangu wakiwa watoto.

Katika masuala yanayogusa USTAWI wa nchi, Rabbon Huwa nimenyooka kama rula!!
Mkuu marais au viongozi kwa ujumla hawaandaliwi kwa kuingia kwenye chipukizi. Chipukizi ilikuwa na njia ya wakomunisti kuanza kuwa-brainwash wananchi tangu wakiwa wadogo. Njia sahihi ya kuandaa viongozi ni watoto kupata makuzi na elimu bora, kuwa na mfumo mzuri wa uongozi wa nchi na viongozi kuwa na maadili mazuri.
 
Upuuzi mtupu tuonyeshe faida zinazoonekana,
badala tutengenezee watoto mitaala mizuri Ili 2040 tuwe na wataalamu wa kurusha satellite
We Unawaza uchipkizi - ujinga ttu
 
Upuuzi mtupu tuonyeshe faida zinazoonekana,
badala tutengenezee watoto mitaala mizuri Ili 2040 tuwe na wataalamu wa kurusha satellite
We Unawaza uchipkizi - ujinga ttu
Kwahiyo watoto wote watarusha satellite?
 
Ndomana sisi walimu wa Imani lazima tutoke mbele kupongeza,

Sababu imeandikwa, Mlee mtoto katika njia impasayo, maana hatoiacha kamwe.

Cha muhimu, itungwe SHERIA Bora kuhakikisha hao chipukizi wanapata mafunzo Bora ,wasifundishwe uhalifu, Bali Uzalendo nk nk.
 
Una uelewa finyi soma Tena nilichokuandikia
Hakuna Mahali nimepinga watoto wasipewe Elimu Bora,

Muhimu ni kuwa, wakiwa katika mfumo huo wa kielimu, wanapata pia fursa ya kuendelea vipaji vyao nk nk.
 
Uko sahihi,

Yote ni muhimu, kinachotakiwa ni Nia na dhamira njema katika kuyatekeleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…