Pre GE2025 Naunga mkono hoja ya Ally Keissy kuwa Rais Samia anamalizia Kipindi cha Magufuli, yeye Vipindi vyake ataanza Oktoba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mpeni miaka 20 Tena! Mmelala siku mkiamka mtaelewa,mlikofikishwa
 
Mtu ulikuwa mbunge wa muda mrefu halafu hujui Katibaya nchi inasemaje? Zee pumbavu kabusa hili! Samia kama atashinda uchaguzi atakuwa amemaliza muda wake anapewa kupisha mwingine hiyo 2030 full stop! Kama angeingia madarakani kukiwa kumebaki mwaka mmoja hapo ingekuwa sawa lakini sasa hivi kaingia kipindi cha zaidi ya miaka mitatu hivyo kinahesabika ni kipindi kizima hicho!
 
Mkuu mazezeta kwenye lile jengo Dodoma tupo wengi mno.
 
Safi sana akitoka apewe zuchu kila mtu anayo haki hiyo.
 
Japo Bimkubwa ni Rais namba 2 kwa ubora Africa yenye nchi zaidi ya 50 na kazi ameiweza kuliko matarajio ya wengi hasa ktk miradi ya SGR japo inabidi ifike Mwanza na Kigoma na ibebe mizigo ya nchi jirani ili kuleta tija na kukamilisha Bwawa la Nyerere, ila katiba inasema wazi uraisi wa tz ni mihula miwili, japo mimi nadhani kuna mkanganyiko kwenye katiba sababu inatakiwa ikamilike mihula 2 ya miaka 10, hivyo binafsi naona inapaswa Maza akimaliza 2030 aongezwe ule muda aliotumia Rais Magufuli ili ifike miaka kumi kamili.

Binafsi naamini ni kinyume cha katiba Maza kuongoza mihula mitatu na tumeona vurugu za Burundi baada ya Nkurunzinza kujipa muhula wa 3, we cannot guarantee amani iwapo hilo litatokea, itakuwa big scandal na labda mwanzo wa vurugu zisizoisha tz na moto wake huwa hauzimiki milele.
 
Rais Samia aliapishwa kuwa Rais baada kifo cha Rais Magufuli kwa mujibu wa Ibara ya 37 (5) ya Katiba ya JMT kwa masharti yalivyoelekezwa katika Ibara ya 40 ya Katiba hiyo. Sasa kama tunakubaliana kuwa Samia aliapishwa kuwa Rais kwa mujibu wa Katiba ya JMT kwa nini Katiba hiyo ivunjwe ili kumuongezea kindi cha tatu?Au ni kwa vile Samia mwenyewe haiheshimu Katiba hiyo ambayo alidiriki kuiita kijitabu tu?
 
Huyu dingi namfahamu anavuta bangi sana nilishamuona maeneo ya Mbezi Makonde analipuliza nafikiri ana nyumba maeneo hayo.
 
Hilo lizee limekaa miaka na miaka Bungeni, kanogewa na pesa za bure. Hapo anafanya uchawa na ni mzee mzima ili tu, ateuliwe tena Ubunge. Naomba asiteuliwe akalee wajukuu huko, huwa anaropoka tu, hachuji maneno yake.
 
Kuna wakati unajiuliza huyu aliwezaje kuwa mbunge kwa mashudu haya anayozungumza mbele ya umma?

Katiba ipo wazi kwamba endapo Makamu wa Rais atashika madaraka ya Rais kwasababu ya Rais aliyekuwa madarakani aidha kujiuzulu, kufariki dunia ama sababu nyingine yoyote katika kipindi kinachozidi miaka mitatu basi ana haki ya kugombea kipindi kimoja pekee cha miaka mitano.

Ikiwa Makamu wa Rais atashika kiti cha Urais kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu basi atakuwa na haki ya kugombea nafasi ya Urais kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Sasa ukiangalia Rais Samia ameshika madaraka ya Urais kwa kipindi kinachozidi miaka mitatu (2021-2025) hivyo basi ana haki ya kugombea kiti cha Urais kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano.
 
Hivi Wabunge si huwa wanaapa kuilinda Katiba ya JMT.?

Na vipi Mbunge akipendekeza jambo ambalo ni uvunjifu wa katiba.?

Si anakuwa amekiuka kiapo chake.?
 
Na hiyo miandishi ya habari haina uelewa ndiyo maana hayajambana na maswali ya maana! Yanamhoji kama mapumbavu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…