LGE2024 Naunga Mkono Serikali kuongeza majina (Kama kweli hilo limefanyika) kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Bado wewe ni mbuluchamba akili za darasa la pili subiri kidogo ukue utaweza kujua nini unachoandika.
Kati ya mimi na wewe unayegoma kujiandikisha nani anatakiwa kusubiri kukua? Nafikiri wanaoshindwa kujiandikisha ndo wanapaswa zaidi kusubiri kukua mana huo ni utoto na ujinga.
 
Haijaongeza
Mimi ninakoishi wana CCM wote na familia na ndugu wansishi nao wote waliofikisha miaka 18 wamejiandikisha
Saaafi sana, kunyweni beer creti bill talipa, kama walokole kunyweni soda creti 2 talipa, mnajitqmbua sana
 
Tuna safari ndefu ya kwenda kama taifa kama mawazo/fikra zenyewe ndo hizi.
Wanaosusia uchaguzi ndo wanarefusha safari Mkuu, tukijiandikisha kwa wingi wagombea watatuheshimu. Mfano mgombea anakuja kupiga kura wakati anajua waliojiandikisha ni 10 na majina feki ni 500 unafikiri atawehishimu hicho kijiji au Kata au Mtaa?
 
Kwa hiyo usipojiandikisha ndo haki itapatikana?
Watu hawajiandikishi Kwa sababu ya kukosekana haki kwenye kura.mgombea anashinda mwingine anayetangazwa kushindwa ni mwingine Sasa kunahaja Gani Sasa ya kujiandikisha kupiga kula?
 
Kwa hiyo usipojiandikisha ndo unakua umewakomoa? Ujumbe gani sasa unatuma hapo wakati unaweza kuta mtaa unaokaa tayari una majina mengi kuliko hata idadi yenu ya wakazi wa mtaa kwa sababu ham hamkujiandikisha, na mtachaguliwa viongozi na ghost
 
Kuna umhimu upi kama kura za kwenye sanduku hazihesabiwi kumtambua mshindi halali?

Jibu swali halafu nikujibu sawali lako sasa
Kura hazihesabiwi kutokana na uchache wa mawakala wa vyama vingine ndo mana tunabaki tu kulalamika bila hata ushahidi wa kutosha, mfano kipindi hiki zaidi ya vituo asilimia 70% havikuwa na mawakala wa vyama vingine zaidi ya CCM
 
Kwa hiyo usipojiandikisha ndo unakua umewakomoa? Ujumbe gani sasa unatuma hapo wakati unaweza kuta mtaa unaokaa tayari una majina mengi kuliko hata idadi yenu ya wakazi wa mtaa kwa sababu ham hamkujiandikisha, na mtachaguliwa viongozi na ghost
Yaani sina matatizo na idadi ya majina, wakitaka wachukue hata watoto wanaonyonya wapige kura, lakini ujumbe kuwa hatuwataki umefika. Na hatua itakayofuata ni machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ili heshima ya box irejee. Lakini hizi chaguzi ambazo ccm ni refarii na mchezaji hapo hapo hatuna muda huo.
 
Bu........shit
 
Wanaosusia uchaguzi ndo wanarefusha safari Mkuu, tukijiandikisha kwa wingi wagombea watatuheshimu. Mfano mgombea anakuja kupiga kura wakati anajua waliojiandikisha ni 10 na majina feki ni 500 unafikiri atawehishimu hicho kijiji au Kata au Mtaa?
Sio kweli mkuu.

Kuongeza majina feki ni ishara tosha kuwa uongozi unaotawala unameshindwa kutimiza matakwa ya wananchi. Wananchi wamekata tamaa.

Viongozi hawawaeshimu wananchi kwasababu wananchi hawana nguvu ya kikatiba ya kuwawajibisha na si kwasababu ya uchache wa kura wanazopata kipindi cha uchaguzi.

Kwahiyo ata kama wangekuwa wamejiandikisha watu kumi tu kwenye mtaa na hao ndo wakampigia kura, ataendelea kuwatumikia/kuwaheshimu wananchi wote wa mtaa kwa sababu wanayo nguvu kikatiba kumwajibisha.

Katiba yetu haimpi mamlaka mwananchi juu ya viongozi wao. Kwahiyo hakuna kiongozi anayehofu wananchi wake.
 
Mambo yanabadilika sana, zama zile ni tofauti sana na nyakati za leo. Tafakari kuhusu chaguzi za 2019 na 2020, jibu sahihi atakalopata ndiyo chanzo cha mdororo katika uandikishaji.... "Maumivu ya mtu aliyekunywa sumu hapaswi kulia ilhali sumu alikunywa kwa hiari yake".
 
Unakielewa ulichokiandika au bado upo mtungi tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…