Naungana na CHADEMA kwenye suala la kuitafuta Katiba Mpya, wakati wa Katiba Mpya ni sasa

Naungana na CHADEMA kwenye suala la kuitafuta Katiba Mpya, wakati wa Katiba Mpya ni sasa

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Hata kama CHADEMA wanaitaka Katiba mpya ili waweze kushiriki uchaguzi wenye ushindani halali bado katiba mpya ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu.

Katiba ya sasa ina mapungufu mengi sana. Kwanza swala la elimu halikuzingatiwa kabisa katika kuwapata viongozi mbalimbali.

Dunia ya sasa inaongozwa na sayansi na teknolojia. Huwezi kushindana katika ulimwengu unaotumia sayansi na teknolojia bila kutumia watu walioelimika kwa kukaa darasani. Hata kama watanzania wengi waliopata elimu hawaleti matokeo mazuri kwenye taifa hilo limetokana na kuwatumia viongozi wasio na elimu kwenye Taifa letu.

Wakati wa mabadiriko ndio huu hakuna wakati mwingine tutakaoweza kupata katiba mpya zaidi ya wakati huu.

Watanzania tuunganeni katika swala la katiba mpya ni muhimu sana. Taifa letu linapata maendeleo ya ndani tu lakini haliwezi kushindana, na mataifa mengine.

Katika hili lazima tuwe na utayali taifa ni letu sote. Bila katiba mpya mambo mazuri hayawezi kuja kiurahisi.
 
... halafu kwenye mchakato wabunge wa Bunge lililopo nao wanakuwa sehemu ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba; this is funny! Halafu Musukuma na Kibajaji wataielewaje ibara ya inayozungumzia elimu kama sifa ya mtu kuchaguliwa kuwa mbunge?

Ibara zenye kugusa maslahi yao zitapigwa chini fasta! Ni kosa kubwa wabunge kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba au kuingiza uchama! Mnakumbuka walikwamisha mchakato last time kosa kama hilo lisirudiwe.
 
Mzururaji na kibaraka wa wazungu asitubabaishe, watanzania tunataka maendeleo na tunaona yakifanyika, wanafuta unafuu wa kupata uongozi kupitia uchochoro wa katiba mpya wakati iliyopo haina shida imetumika miaka mingi na ilikuwa ikifanyiwa marekebisha mbalimbali ili kuendane na mabadiliko mbalimbali, semeni ni kipengele gani kwenye katiba hakipo sawa kifanyiwe marekebisho.
 
Kizazi cha sasa kuongozwa na katiba mfu ni utopolo mtupu.

Tunataka katiba inayowafunga viongozi baada ya uongozi waishie jela.

Itasaidia kukomesha upotevu wa kodi na matumizi mabaya ya madaraka.

Sio mtu anajiamulia tu kujenga airport kijijini kwao,au kujenga ikulu mpya huku watoto wanakaa chini.

Ni afrika pekee ndipo watawala awaozei jela thus hatuna maendeleo
 
Mama alipaswa sema neno la matumaini katika siku za 100 za awali, bado Nina Imani na Mama ataweka sawa.
 
Mzururaji na kibaraka wa wazungu asitubabaishe, watanzania tunataka maendeleo na tunaona yakifanyika, wanafuta unafuu wa kupata uongozi kupitia uchochoro wa katiba mpya wakati iliyopo haina shida imetumika miaka mingi na ilikuwa ikifanyiwa marekebisha mbalimbali ili kuendane na mabadiliko mbalimbali, semeni ni kipengele gani kwenye katiba hakipo sawa kifanyiwe marekebisho.
Katiba hii ya kidikteta inafaa maiti kama nyie,
 
Kwani uongozi ni kusoma sana?

Wataalamu mbona wanaajiriwa kwa vigezo vya elimu?

Mbona nigeria inaongoza kwa viwango vya juu vya elimu hususani viongozi wao na bado nchi yao imetopea katika rushwa na vitendo vya vurugu na ugaidi?

Kuitaka katiba mpya ili tupate viongozi wasomi hakuna mashiko hayo.

Ikumbukwe pia waliopata kufanya vitendo vya ubadhirifu na ufisadi hapa nchini ni wasomi tu, tena wasomi kwelikweli.

N.B: Katiba hii tuliyonayo ni nzuri wala haina mapungufu.Muhimu ni kuendelea kuifuata vyema tu

#Kaziiendelee
#Jmtkwanza
 
Ninapatwa na Hofu kubwa pale taasisi nyeti zinaponyamaza kimya Badala ya kujali na kuidai katiba mpya.

1. Taasisi za kiimani
- wakristo na makanisa yao wapo kimya, ningetarajia Maaskofu, mapadri, wachungaji, wainjiristi, nk kuwaelimisha wafuasi wao umuhimu wa katiba mpya

- waislam na misikiti yao wapo kimya, ningetarajia mashekh, maustadhi nk kuwaelimisha wafuasi wao umuhimu wa katiba mpya.

Hii ni aibu kubwa kwa taifa. Sababu watu wa imani miskitini na makanisani kufumbia macho haki stahiki kwa waumini wao juu ya madai ya katiba mpya.
 
Pole mjane,kama refa anateuliwa na timu shindan kisha ukaona hakuna tatizo basi utakuwa kubwa la mazumbukuku
Mzururaji na kibaraka wa wazungu asitubabaishe, watanzania tunataka maendeleo na tunaona yakifanyika, wanafuta unafuu wa kupata uongozi kupitia uchochoro wa katiba mpya wakati iliyopo haina shida imetumika miaka mingi na ilikuwa ikifanyiwa marekebisha mbalimbali ili kuendane na mabadiliko mbalimbali, semeni ni kipengele gani kwenye katiba hakipo sawa kifanyiwe marekebisho.
 
Kwani uongozi ni kusoma sana?

Wataalamu mbona wanaajiriwa kwa vigezo vya elimu?

Mbona nigeria inaongoza kwa viwango vya juu vya elimu hususani viongozi wao na bado nchi yao imetopea katika rushwa na vitendo vya vurugu na ugaidi?

Kuitaka katiba mpya ili tupate viongozi wasomi hakuna mashiko hayo.

Ikumbukwe pia waliopata kufanya vitendo vya ubadhirifu na ufisadi hapa nchini ni wasomi tu, tena wasomi kwelikweli.

N.B: Katiba hii tuliyonayo ni nzuri wala haina mapungufu.Muhimu ni kuendelea kuifuata vyema tu

#Kaziiendelee
#Jmtkwanza

Katiba mpya itakuwa nafaida kubwa kwa viongozi na raia

1. Tutatenganisha madaraka ya Rais kufanya uteuzi kwa maslahi yake na utashi wake bila kujali sifa na mahitaji ya wananchi

Hasara za uteuzi wa rais kwa viongozi

A) wateuliwa watafanya kwa kumfurahisha rais ........ Elimu zitawekwa mifukoni.
Mfano.
- Kabudi, alimuabudu mteuzi wake nakuacha utendaji kwa mujibu wa taaluma take.

- Wizara ya Afya walinyamaza kimya nakujificha, ili tu wasimuuzi mteule wao

- Air Tanzania tuliambiwa tunapiga faida sana na gawio lakutosha kwa serikali..... kumbe ilikuwa tofauti, wasimamizi ni wasomi lakini usomi uliwekwa mifukoni wasimuuzi mteuzi wao.

- Bashiru msomi mbobezi, alijisahau mpaka kusema nafuu yao nikutumie Dola kubaki madarakani, nawakatumia wakafanikiwa, akasahau suala ni uongozi unaotokana na umma kwa uchaguzi huru sio utawala wa nguvu za Dola..... kwanini tupige kura kama hoja nikutumie Dola?

Mifano ni mingi sana, elimu zinawekwa mfukoni ilikumfurahisha mfalme, ukitenda kinyume unatumbukiwa AMA kutenguliwa
 
Baadhi ya faida za katiba mpya

1. Uchaguzi uwe na tume huru ya uchaguzi,
- kura iwe na maamuzi, mtu anapotoka kuenda kupiga kura, Tuione thamani ya hiyo kura katika maamuzi.

Sio mtu anapanga foreni, anashinda na njaaa, anapiga kura isionathamani..... Anaibuka mtawala anasema unatumia nafuu ya Dola kubaki madarakani. Kwanini unasumbua watu sasa kupanga mafoleni, kushinda na njaa na kupoteza muda?

maana yake, viongozi wanashindishwa kwa nguvu ya Dola na hawatawatumikia wananchi Bali watakuwa wa ndiyooooo kwa kila jambo..... ukitazama bungeni utaona, ni ndiyoooooo, ndiyoooooo,
Tuongeze kodi ...... ndiyoooooo
Tuongeze makato..... ndiyoooo
Afukuzwe mnadhim... ndiyooooo
Hakuna kuhoji, hakuna kupinga nikukubali tuuuu

Sababu wamewekwa na Dola, yaani kura haikuwaweka pale. Ingelikuwa kura ya mpiga kura inanguvu ndiyoooooo za ajabuajabu zisingekuwepo
Weledi
Elimu
Vipaji
Utashi
Hekima na busara

Tungeziona
 
Mzururaji na kibaraka wa wazungu asitubabaishe, watanzania tunataka maendeleo na tunaona yakifanyika, wanafuta unafuu wa kupata uongozi kupitia uchochoro wa katiba mpya wakati iliyopo haina shida imetumika miaka mingi na ilikuwa ikifanyiwa marekebisha mbalimbali ili kuendane na mabadiliko mbalimbali, semeni ni kipengele gani kwenye katiba hakipo sawa kifanyiwe marekebisho.
Iliyopo ndio imesababisha Jiwe amekufa kibudu.
 
Baadhi ya faida za katiba mpya

1. Uchaguzi uwe na tume huru ya uchaguzi,
- kura iwe na maamuzi, mtu anapotoka kuenda kupiga kura, Tuione thamani ya hiyo kura katika maamuzi.

Sio mtu anapanga foreni, anashinda na njaaa, anapiga kura isionathamani..... Anaibuka mtawala anasema unatumia nafuu ya Dola kubaki madarakani. Kwanini unasumbua watu sasa kupanga mafoleni, kushinda na njaa na kupoteza muda?

maana yake, viongozi wanashindishwa kwa nguvu ya Dola na hawatawatumikia wananchi Bali watakuwa wa ndiyooooo kwa kila jambo..... ukitazama bungeni utaona, ni ndiyoooooo, ndiyoooooo,
Tuongeze kodi ...... ndiyoooooo
Tuongeze makato..... ndiyoooo
Afukuzwe mnadhim... ndiyooooo
Hakuna kuhoji, hakuna kupinga nikukubali tuuuu

Sababu wamewekwa na Dola, yaani kura haikuwaweka pale. Ingelikuwa kura ya mpiga kura inanguvu ndiyoooooo za ajabuajabu zisingekuwepo
Weledi
Elimu
Vipaji
Utashi
Hekima na busara

Tungeziona
Katiba mPya ina faida Milioni moja.
 
2. Demokrasia ya kweli kiutendaji
A) vyombo vya habari viripoti kwa uhuru, viibuwe Souza, matumizi mabovu ya madaraka, Mali za umma, uzembe nk
Waanfishi wafanye investigative journalism bila mikwara kama nitawachapa viboko, kuwafungulia mikesi ya kubumba nk

Kunafaida kubwa ya kuwaacha wandishi wa habari wafanye uchunguzi kwa kuzingatia maadili na miiko yao kitaaluma serikali isiwekee vipingamizi na vitisho.

Faida itakuwa kubwa sana maana ufisadi na mafisadi watawekwa hadharani
 
3. Vyama vya siasa vishindane kwa
- Sera, chenye sera nzuri na ushawishi kishinde uchaguzi kiwajibike kwa ubora wa sera zake, kikiharibu kitaadhibiwa kwa nguvu ya sanduku la kura, sio unafuu wa nguvu za Dola kukibakisha madarakani

- Hoja, vyama vishindane kwa hoja kwa kuzingatia ukweli, haki na uwazi. Pasiwe na ukiritimba wa nafuu ya Dola kubanananisha baadhi ya vyama na kunufaisha mmoja wao hatakama hoja zake dhaifu na hazina mashiko

Ushindani wa hoja kwa uwazi, ukweli na haki utalinufaisha sana taifa kutoka Kwenye mikwamo na changamoto mbalimbali zilizoonekana kukosa njia za kutoka na kuboresha tija na ufanisi.
 
Back
Top Bottom