Naungana na jamii ya kimataifa kutompa ushirikiano mheshimiwa Uhuru Kenyatta

Naungana na jamii ya kimataifa kutompa ushirikiano mheshimiwa Uhuru Kenyatta

Wild fauna

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
461
Reaction score
189
Heshima mbele,

Nimeshangazwa sana na maamuzi Wakenya waliyochukua, Naomba kuungana na jamii za kimataifa hususani Marekani ambayo tayari imetanabaisha kutoiunga mkono serikali ambayo Kenyatta atachukua nafasi kuiongoza.

Nawaza huyu bwana atainua vp uchumi,atafanya biashara na nani angali wamagharibi wameshaanza kumwekea ngumu.Sina uhakika asilimia mia moja kama haya maamuzi kweli yametoka mioyoni mwa Wakenya.

Hata kama siasa ya Kenya ni ya ukabila lakini ukabila gani unaoamini udhaifu wa mtu katika kupewa nafasi nzito kama hiyo?

Je ikitokea tuhuma zinazowakabili zikawafunga je nchi itaongozwa na nani?

Wakenya mtashangilia leo ila kazi mnayo,time will tell.
 
Hongera Mtukufu Rais Uhuru Jomo Kenyata kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Usitishwe na viji maneno vya jumuia ya Kimataifa.Jiran zako Uganda na Tz zinapendwa sana na Hizo jumuia but mpaka leo wanazungumzia ' kuhakikisha hakuna ataekufa na njaa' badala ya Maendeleo!
 
We ndiyo wale wanao amin kila asemacho mzungu ndiyo hicho cha kufuata kisa eti ana akili nyingi kushinda wewe.
Ukolon ushaisha na wanao chagua Rais si hao wa ulaya ni wananch wa Kenya na wao wamemuona anafaa ndiyo maana wakamchagua.
We endelea na umagharibi wako.
 
Nafurahi sana "manuu" unapata kiburi cha kubwabwaja humu kwa nguvu za wazungu. Bila mzungu haya matapishi yako uliyoweka hapo juu nisingeyaona. Siamini kila anachosema mzungu ila i acknowledge that they are the best,they step ahead than us
 
Heshima mbele,
nimeshangazwa sana na maamuzi wakenya waliyochukua. Naomba kuungana na jamii za kimataifa hususani marekani ambayo tayari imetanabaisha kutoiunga mkono serikali ambayo kenyata atachukua nafasi kuiongoza.
Nawaza huyu bwana atainua vp uchumi,atafanya biashara na nani angali wamangaribi wameshaanza kumwekea ngumu.
Sina uhakika asilimia mia moja kama haya maamuzi kweli yametoka mioyoni mwa wakenya. Hata kama siasa ya kenya ni ya ukabila lakini ukabila gani unaoamini udhaifu wa mtu katika kupewa nafasi nzito kama hiyo?
Je ikitokea tuhuma zinazowakabili zikawafunga je nchi itaongozwa na nani?
Wakenya mtashangilia leo ila kazi mnayo,time will tell.

Usamehewe kwa kuwa hujui usemalo. Ukipata nafasi ya kuzungumza na Wakikuyu ambao walikuwa wanachinjwa kama kuku kwenye zile vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007, watakwambia kuwa Uhuru ni Mungu wao wa pili kwani bila kuingilia kati, wangeendelea kuchinjwa zaidi. Kwa wakikuyu Uhuru ni kama Musa aliyetumwa na Mungu kuwakomboa kutoka kwenye upanga wa Wajaluo. Siasa za Kenya ni ngumu kidogo.

Tiba
 
Wild fauna umeongea point..uchakachuzi umefanywa kwa utaalam wa hali ya juu
 
"Tiba" ndo jamaa aliamua kuwa ajiri mungiki sio? Na huko ICC anatuhumiwa kwa kuwa alikuwa musa wa wakikuyu? Dah!
 
kwahiyo hoja hapa ni ipi???kama hayajatoka mioyoni mwa wakenya yametoka wapi??fikiria mbali...wakenya washaamua...waacheni
 
Usamehewe kwa kuwa hujui usemalo. Ukipata nafasi ya kuzungumza na Wakikuyu ambao walikuwa wanachinjwa kama kuku kwenye zile vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007, watakwambia kuwa Uhuru ni Mungu wao wa pili kwani bila kuingilia kati, wangeendelea kuchinjwa zaidi. Kwa wakikuyu Uhuru ni kama Musa aliyetumwa na Mungu kuwakomboa kutoka kwenye upanga wa Wajaluo. Siasa za Kenya ni ngumu kidogo.

Tiba

well said
 
We ndiyo wale wanao amin kila asemacho mzungu ndiyo hicho cha kufuata kisa eti ana akili nyingi kushinda wewe.
Ukolon ushaisha na wanao chagua Rais si hao wa ulaya ni wananch wa Kenya na wao wamemuona anafaa ndiyo maana wakamchagua.
We endelea na umagharibi wako.

haaaahaaaa HIVI UJUI UNAISHI NA DEN LA MANGHARIBI NDUGU LOH UNAFIKIR RAIS WAKO ANGEACHA SAFARI ZA KILA SIKU VIWALO UNGEVIJUA LINI
 
Vifurambwete wengine hata mpambe wa mpambe wa Uhuru hawamjui, lakini kujitutumua ushuzi tu.

Wewe ni nani mpaka Uhuru ahitaji ushirikiano wako? Wamarekani, Waingereza na wenzao wanajipanga waanzaje kumtongoza upya awape ushirikiano katika efforts zao za usalama horn of Africa na katika biashara, wewe nani mpaka ahitaji ushirikiano wako?

Granted, the game is rigged. Kenya is all but a fiefdom. But what is the significant difference between Raila and Uhuru? They are both oligarchs. Politicians by pedigree, plagued by Plutarchian plunder and nagged by nihilistic nepotism through hedonistic harpooning for hegemony and a dual dogged determinism.

It's not like Raila angekuwa revolutionary. Tumemuona alivyokuwa PM.

I am not Kenyan so whoever Kenyans choose I am fine. Even as I would like to see what Shaggy call "some lickle ghetto youth with some bright ideas" in "It Burn Me" to ascend to the helm (notice, not the throne).

Don't blame the player, fix the game.
 
Mkubwa sana masikitiko yangu ni kuwa hata ukiungana nao hao haitazuia chochote wala kuwapunguzia chochote wakenya wakenya wameamua na tuwaige kwa kuchukua maamuzi magumu siyo hapa kwetu mtu anapiga kura kwa ushawishi wa mahindi kisado.
 
Kenyata ndiye chaguo la kidemokrasia la Wakenya! Waaumini wote wa demokrasia wanapaswa kuuheshimu uamuzi huo!
 
UHURU KENYATTA na ODINGA wote kwa pamoja hawakutakiwa kabisa kushiriki ktk uchaguzi huu wa KENYA maana wote ni wahusika wakubwa wa Ukabila nchini Kenya. Na nitasema wazi ya kwamba uchaguzi umekwisha lakini subirini mtakuja yaona yanayofuata wala sii muda mrefu, sura halisi za hawa watu zitajitokeza..
 
"Tiba" ndo jamaa aliamua kuwa ajiri mungiki sio? Na huko ICC anatuhumiwa kwa kuwa alikuwa musa wa wakikuyu? Dah!

Wild Fauna, fungua akili yako angalia mbali. Aliyepashwa kupelekwa ICC zaidi ni Raila akifuatiwa na Kibaki, hawa ndio kugombea kwao madaraka kulipeleka taifa kwenye machafuko. Uhuru alijitokeza kuzuia watu wa kabila lake wasimalizwe baada ya serikali kushindwa kuwapa protection. Jumuia ya kimaifa na hasa wazungu wanavyoliangalia hili suala la ICC ni tofauti ya Wakenya wanavyoliangalia, la sivyo Uhuru asingepigiwa kura zaidi ya millioni 6 na Wakenya.

I might be wrong, but this is my personal stand!!!

Tiba
 
Heshima mbele,
nimeshangazwa sana na maamuzi wakenya waliyochukua. Naomba kuungana na jamii za kimataifa hususani marekani ambayo tayari imetanabaisha kutoiunga mkono serikali ambayo kenyata atachukua nafasi kuiongoza.
Nawaza huyu bwana atainua vp uchumi,atafanya biashara na nani angali wamangaribi wameshaanza kumwekea ngumu.
Sina uhakika asilimia mia moja kama haya maamuzi kweli yametoka mioyoni mwa wakenya. Hata kama siasa ya kenya ni ya ukabila lakini ukabila gani unaoamini udhaifu wa mtu katika kupewa nafasi nzito kama hiyo?
Je ikitokea tuhuma zinazowakabili zikawafunga je nchi itaongozwa na nani?
Wakenya mtashangilia leo ila kazi mnayo,time will tell.

Mbona unaandika na kujikana wewe mwenyewe, unasema huamini kama kwli Wakenya ndio wamemchagua Bw.Uhuru Kenyata hapo hapo unasema Wakenya mtashangilia leo ila kazi mnayo, sasa kama hawakumchagua kwa nini tena washangilie?

Wild Fauna, fungua akili yako angalia mbali. Aliyepashwa kupelekwa ICC zaidi ni Raila akifuatiwa na Kibaki, hawa ndio kugombea kwao madaraka kulipeleka taifa kwenye machafuko. Uhuru alijitokeza kuzuia watu wa kabila lake wasimalizwe baada ya serikali kushindwa kuwapa protection. Jumuia ya kimaifa na hasa wazungu wanavyoliangalia hili suala la ICC ni tofauti ya Wakenya wanavyoliangalia, la sivyo Uhuru asingepigiwa kura zaidi ya millioni 6 na Wakenya.

I might be wrong, but this is my personal stand!!!

Tiba

A million percent right analysis
 
Back
Top Bottom