Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi sijaelewa ulichotaka kuwakilisha,ingawaje ninaona kama umewakilisha kitu cha muhimu sana....Ningefurahi kama ungeweza kutoa tafsiri ya terms ulizotumia ambazo wewe unazijua kabisa kwamba wengine wengi humu hatujui nini maana yake...hegemony,nihilist na neno zingine zote hizo.Asante sana kwa kunielewa
Kwann wakenya wapangiwe rais ? Chaguo Lao ni Uhuru sasa vikwazo via nn ? Mm mwenyewe nilimkubali Odinga lkn kura hazikutosha naheshimu maamuzi yao .
Japokua mimi ni si Mkenya ila niungane na Wakenya kwa kuamua kutumia haki yao ya msingi kumchagua mtu waliyempenda bila kufuata influence za Magharibi...kwa uelewa wangu mdogo wa siasa za Kenya hususan yale machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2007 uliomwingiza Kibaki madarakani,Raila na Kibaki ndio walikua key players kwa hisani ya bwana Samwel Kivuitu aliyechezesha ngoma ambayo alishindwa kuhimili mirindimo yake,Mungu ampe hukumu ya haki kwa kua amekwisha kutangulia mbele ya hadi since February..
Yumkini Raila ndiye aliyeshinda uchaguzi ule wa mwaka 2007 si jambo la msingi nalosemea hapa ila reaction yake baada ya tume kumtangaza Mr Kibaki kua mshindi kwenye uchaguzi ule ilichochea ama kuhamasisha kwa namna moja ama nyingine wafuasi wake (Raila) of whom wengi walikua Waluo (im stand to be corrected) kuinuka juu ya wenzao Wakikuyu kwa kuwapiga na kuwaua ikifatana na uharibifu wa mali na makazi!
Wakati yote haya yakitokea si Raila,wala kibaki waliokemea 'kwa kumaanisha' ilihali mamia ya Wakikuyu/Wakalenjin wakiendelea kuteketea.Hapa ndipo ushiriki wa Kibaki unapokuja..
Kosa alilolifanya Uhuru ambalo limesababisha awe victim hadi leo ni nguvu kubwa aliyotumia kulipiza/kuzuia ndugu zake 'Wakikuyu' wasiendelee kuketeketezwa. Yatosha kusema tu kua kwa Jamii ya Wakenya esp. Wakikuyu/Waluo ambao hawakua upande wowote wanamwona Uhuru km Hero kwao ilihali jamii ya kimataifa ikimwona mhalifu wa kivita.
Watu wa kupeleka ICC ni pamoja Samwel Kivuitu (japo ameshafariki) Raila, na Mwai Kibaki! Wamarekani diplomatically wako sawa na Mataifa mengine na si haki kuwaamulia wenye taifa lao kwamba ni nani anafaa kuwa kiongozi. Tumeona sehemu nyingi duniani ambazo Mmarekani hana interest nazo akiachia zijiendeshe tu shaghalabaghala wakati huo huo akiwa mstari wa mbele kuamua masuala nyeti ya nchi zenye kumnufaisha kwa namna moja ama nyingine...
Viva Kenyatta,Kenya ipo mikononi mwako,kaa chini na jopo la wataalamu wa nchi yako wakushauri namna ya kujenga taifa lako na kuondoa hii mifarakano na mipasuko ya Kikabila!
Heshima mbele,
Nimeshangazwa sana na maamuzi Wakenya waliyochukua, Naomba kuungana na jamii za kimataifa hususani Marekani ambayo tayari imetanabaisha kutoiunga mkono serikali ambayo Kenyatta atachukua nafasi kuiongoza.
Nawaza huyu bwana atainua vp uchumi,atafanya biashara na nani angali wamagharibi wameshaanza kumwekea ngumu.Sina uhakika asilimia mia moja kama haya maamuzi kweli yametoka mioyoni mwa Wakenya.
Hata kama siasa ya Kenya ni ya ukabila lakini ukabila gani unaoamini udhaifu wa mtu katika kupewa nafasi nzito kama hiyo?
Je ikitokea tuhuma zinazowakabili zikawafunga je nchi itaongozwa na nani?
Wakenya mtashangilia leo ila kazi mnayo,time will tell.
Heshima mbele,
Nimeshangazwa sana na maamuzi Wakenya waliyochukua, Naomba kuungana na jamii za kimataifa hususani Marekani ambayo tayari imetanabaisha kutoiunga mkono serikali ambayo Kenyatta atachukua nafasi kuiongoza.
Nawaza huyu bwana atainua vp uchumi,atafanya biashara na nani angali wamagharibi wameshaanza kumwekea ngumu.Sina uhakika asilimia mia moja kama haya maamuzi kweli yametoka mioyoni mwa Wakenya.
Hata kama siasa ya Kenya ni ya ukabila lakini ukabila gani unaoamini udhaifu wa mtu katika kupewa nafasi nzito kama hiyo?
Je ikitokea tuhuma zinazowakabili zikawafunga je nchi itaongozwa na nani?
Wakenya mtashangilia leo ila kazi mnayo,time will tell.
Wild Fauna, fungua akili yako angalia mbali. Aliyepashwa kupelekwa ICC zaidi ni Raila akifuatiwa na Kibaki, hawa ndio kugombea kwao madaraka kulipeleka taifa kwenye machafuko. Uhuru alijitokeza kuzuia watu wa kabila lake wasimalizwe baada ya serikali kushindwa kuwapa protection. Jumuia ya kimaifa na hasa wazungu wanavyoliangalia hili suala la ICC ni tofauti ya Wakenya wanavyoliangalia, la sivyo Uhuru asingepigiwa kura zaidi ya millioni 6 na Wakenya.
I might be wrong, but this is my personal stand!!!
Tiba
swali ambalo najiuliza
immunite ambayo wataipata kama raisi na makamu wake itawasaidia icc?na
je wakipatikana na hatia icc itakuwaje?
Kwenye press confrence ya odinga amejaribu kuainisha mapungufu ya tume
ya uchaguzi na watafanya pertition kama mahakama itakuwa huru more 2
come
Usamehewe kwa kuwa hujui usemalo. Ukipata nafasi ya kuzungumza na Wakikuyu ambao walikuwa wanachinjwa kama kuku kwenye zile vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007, watakwambia kuwa Uhuru ni Mungu wao wa pili kwani bila kuingilia kati, wangeendelea kuchinjwa zaidi. Kwa wakikuyu Uhuru ni kama Musa aliyetumwa na Mungu kuwakomboa kutoka kwenye upanga wa Wajaluo. Siasa za Kenya ni ngumu kidogo.
Tiba
UHURU KENYATTA na ODINGA wote kwa pamoja hawakutakiwa kabisa kushiriki ktk uchaguzi huu wa KENYA maana wote ni wahusika wakubwa wa Ukabila nchini Kenya. Na nitasema wazi ya kwamba uchaguzi umekwisha lakini subirini mtakuja yaona yanayofuata wala sii muda mrefu, sura halisi za hawa watu zitajitokeza..