Heshima mbele,
Nimeshangazwa sana na maamuzi Wakenya waliyochukua, Naomba kuungana na jamii za kimataifa hususani Marekani ambayo tayari imetanabaisha kutoiunga mkono serikali ambayo Kenyatta atachukua nafasi kuiongoza.
Nawaza huyu bwana atainua vp uchumi,atafanya biashara na nani angali wamagharibi wameshaanza kumwekea ngumu.Sina uhakika asilimia mia moja kama haya maamuzi kweli yametoka mioyoni mwa Wakenya.
Hata kama siasa ya Kenya ni ya ukabila lakini ukabila gani unaoamini udhaifu wa mtu katika kupewa nafasi nzito kama hiyo?
Je ikitokea tuhuma zinazowakabili zikawafunga je nchi itaongozwa na nani?
Wakenya mtashangilia leo ila kazi mnayo,time will tell.
Waziri ambaye anahusika na mambo ya kigeni bw Kerry wa Marekani ni mmoja aliye tuma risala za
pongezi kwa wale walio changuliwa.
Wingereza hata wao wakatuma pamoja na afrika kusini ambao walihakikisha kufanya kazi na serikali
mpya ya Kenya.
Ndugu Kikwete na Yoweri bado wakasema wako nasi.
Lakini swali ni hili,,,,,ni biashara ngani tunayoifanya na hawa mabepari kama marekani na uingereza??????
Tangu lini pakawa na biashara baina ya mwanadamu na mbu (mosquito) ambaye kazi ni kumnyemelea na
kufyonza damu yake???????
Iko wengi wakufanya biashara na na silazima awe ni hawa mabepari ambao economies
zao zinalegea legea na wakati wowote zinaelekea kuboromoka???????
Kama walifikiri wata impose leadership in Kenya kama vile walivyozoe kwingine duniani,,
ng'oooo,,,si Kenya,,,kwani Kenya ina wenyewe.
Kama walimpendelea huyu bwana Oginga,,kwanini wasitenge sehemu moja ya Marekani
ama uingereza na kumfanya rais huko??????
Kwanini watuuzie vifaa ghali vya kufanyia kura kisha kutushawishi ati ninani twafaa
kumchagua?????????
Hizo njama zao za kiutoto tumezikataa wazi wazi hapa Kenya na tafadhali wasitulee
tee.
Chaguo la walio wengi Kenya sharti lita heshimika na hakuna choice yeyote
ingine.
Kwanini wasianze kutangaza vikwazo walio tishia??????????
Hata ninashangaa ni vikwazo ngani wanaweza kutuwekea,,,,,kupiga
marufuku wana Jubelee kuto zuru Marekani na Uingereza?????
Mmmmmmmmmmm,,,,kwani hakuna mtu wakuwaeleza yakua Uingereza
na Marekani ati si binguni?????
Hata tukiwekewa marufuku ya kwenda mbinguni juu ya sababu tumemchagua
ambaye tulimpendelea kama kiongozi wetu,,,tutasema hata hiyo mbinguni
ikae.
Sisi si wajinga,,,tumekuja kugundua yakwamba hawa mabeberu hawawezi kuishi
bila sisi,,,in the third world na hasa Afrika.
Hebu tuone ni nani anaehitaji mwingine,,hebu wajaribu hiyo,,ati marufuku,,,
na tuone ninani atae kua na kicheko cha mwisho.
Kweli,,,heshima mbele,,,,afadhali nikae na njaa lakini heshima kwangu,,,,,,,
iko.
Mwafrika lazima achukue responsibility yake mikononi mwake,,na si
kuegemea kwa hawa mbu kwajina,,,, jina ati,,the west.
Mpaka lini tutakubali kuendelea kubakwa na hawa walowezi??????
Hatuhitaji misaada ya biscuits na sweets na manguo ya ma jeans yalio na uchafu,,,
hiyo,,,,,wapee wengine.