Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
NAUNGANA NA SPIKA NDUGAI, VIJANA WENGI SIO WAAMINIFU, TENA WAVIVU
Na, Robert Heriel
Kauli ya SPIKA NDUGAI ni kauli thabiti yenye ukweli kwa 100% ndio maana naungana nayo.
Ndugai anamadhaifu yake mengi tuu lakini kwenye hii kauli yake yupo sahihi. Vijana wengi watampinga, watamtukana, watamsema kwa kila lililobaya lakini haiondoi ukweli wa kauli hiyo.
Ukitaka ujue ukweli wa jambo hili basi usiajiriwe jiajiri wewe mwenyewe alafu tafuta Vijana wa kuwaajiri ndio utajua ukweli wa kauli hiyo
Huwezi Muelewa Ndugai kama umeajiriwa na utampinga kwa nguvu zote lakini siku ukiwa umejiajiri na kuajiri watu wengine ndio utaelewa
Kwa upande wangu nilithibitisha kauli hiyo miaka mitatu iliyopita. Niliwekeza kwenye biashara ya usafiri wa Bodaboda, nilinunua Bodaboda tatu, Boxer zilikuwa mbili, na Haujue moja. Niliwapa Vijana, wa Boxer niliwaambia waniletee 10,000 kila siku wakati wa Haujue aniletee 8,000 kila kila siku kulingana na nature ya soko la Dsm lilivyo Boxer ndio hupendelewa na wengi
Vijana wale walijitahidi mwezi wa kwanza tuu baada ya hapo wakaanza sababu, Mara hivi mara vile.
Mmoja Akitoa Side Mirror na akawa anafanya biashara usiku mnene hali iliyopelekea akakamatwa na polisi, kesho yake ananijia bila Bike ananambia ipo kituo cha polisi. Nikaenda nikaitoa.
Mwingine akauza betri akaweka betri Ingine, kwa bahati nzuri kila jumapili niliwaambia wazipeleke kwa Fundi Omary(anayenisaidia habari za mambo haya) akazifanyie ukarabati ikiwemo Kumwaga oil. Omary akanipigia simu kuwa mbona Boxer moja imebadilishwa Betri.
Nampigia dereva ananikana na kunishutumu, nikamwambia mimi sio mtu wa kuchezewa akaona ni maneno matupu hivyo nilikuwa natakiwa kuonyesha vitendo. Nikaongea na Polisi, wakamtia ndani mpaka akasema alipoiuza, aliiuzia Mwenge, akaitwa aliyemuuzia akabanwa akaitoa.
Nikamuachisha kazi. Akaanza kulia lia na kuniomba msamaha kwani anafamilia. Alafu mtu mwenyewe ni mkubwa kwangu kiumri kwani alikuwa na miaka 32 mimi nilikuwa na 24. Nilimpa kazi kwa kudhani atakuwa na akili kutokana na majukumu yake ya kifamilia lakini wapo.
Nikanyang’anya wale wengine wawili mmoja wao akishikwa akiwa na mzigo wa Mirungi akitokea njia ya Bagamoyo. Polisi hawakunielewa kwa urahisi mpaka nilipojitambulisha vyema kuwa sihusiki na biashara za namna hizo. Zikanitoka pesa kidogo nikaitoa pikipiki nikimuacha bodaboda kwenye Kesi yake. Hata hivyo ilichukua siku nyingi.
Haya kwenye biashara ya vipodozi napo niliajiri Msichana lakini nao kila mara huiba, nimebadilisha wasichana sio chini ya 10
Kwenye hilo Duka pia nimeweka mitungi ya Gesi.
Msichana anauza hata mitatu ile mikubwa kwa siku ambayo faida hapo ni 15,000 alafu lile gari likipita anaijaza, nikija anasema hajauza.
Wakati mimi nilishaweka mawasiliano na wale watu wa magari yenye mitungi ya Gesi kuwa kila wakija kubadilisha wanijuze. Hivyo Msichana akisema hajauza wakati mawakala wa Gesi wameniambia wamembadilishia ni ukosefu wa uaminifu.
Kwenye Kilimo napo nimejionea wala sijajadithiwa.
Vijana wengi sio waamnifu. Hupenda kufanya kazi pale Boss awapo karibu, yaani bila usimamizi kwa Hawa Vijana lazima uibiwe.
Vijana wasiowaamnifu ndio huhitaji usimamizi yaani kuwachunga kama watumwa bila hivyo umeumia.
Sijazungumzia mambo ya Saluni za kike na kiume jinsi Vijana wasivyowaaminifu.
Sijazungumzia mafundi Washi ambao bila kuwasimamia basi mpaka nyumba yako inaisha na yake imepanda mpaka kwenye Lenta kwa wizi anaokufanyia.
Sijazungumzia mambo ya Fundi nguo jinsi wasivyowaamifu. Nguo inaweza kaa hata miezi sita mpaka mwaka ipo kwa Fundi unazungushwa kama mpira utadhani unashonewa bure.
Kwa bahati mimi pia ni Fundi nguo kwani nilikofunza wakati nasoma Chuo hivyo naelewa nachokizungumza.
Pia ninajishughulisha Na Recruitment agency hivyo watu wengi hunitumia kuwatafutia wafanyakazi wa aina mbalimbali, hivyo naelewa jinsi Vijana wengi wanavyonitia Aibu huko ninapowapeleka kufanya kazi.
Vijana wengi wanapenda mishahara mikubwa wakati ufanisi wao upo chini.
Sio rahisi mtu akupe mshahara mkubwa wakati ufanisi wako upo chini.
Kingine, Kijana hatujuani zaidi ya huku mtandaoni, anakuambia anataka kazi. Unamuambia kazi ipo ila ya 200,000 njoo ujishikize kwa muda ili zikitokea za mshahara mkubwa nikuunganishe. Kijana hataki anataka nimpe kazi ya 600,000 wakati bado simuamini na wala sijaona utendaji kazi wake ili zitokapo kazi za maana kulingana na connection zangu nim-recommend yeye halijui hilo.
Ndugai hajasema Vijana wote wa kitanzania sio waaminifu bali amesema wengi wetu. Hilo naungana naye.
Nawe ukitaka kuungana naye, basi anzisha biashara unayoilewa nje ndani, kisha Ajiri Kijana utajionea mwenyewe.
Hata hivyo niwapongeze Vijana wachache ambao mmekuwa wema na waaminifu. Endeleeni na moyo huo huo.
Na wale wasiowaaminifu mbadilike acheni wizi wizi.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro