Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Rais Samia jana alisema hapo katikati tulitetereka kidogo tukaanza kubaguana kwa itikadi, ukanda na ukabila, hakutaja ni kipindi cha Magufuli, lakini wafuasi wengi wa Magufuli wakasema anamlenga Magufuli
Hili linaashiria kuwa ni kweli Magufuli alikuwa mbaguzi hadi ubaguzi unapokemewa tayari inaonekana Magufuli ndio kaguswa.
Na kama trukitaka kusonga mbele kama taifa lenye umoja na mshikamano ni lazima tuongee kwa uwazi matatizo yetu ili yasije kujitokeza tena, hata kama yamefanywa na kiongozi gani, lazima tuyasema hapa tulikosea na tunatakiwa kujirekebisha
Magufuli alisikika mara nyingi akisema kipindi cha Kikwete na Mkapa taifa hili lilikuwa likinyonywa sana na mafisadi, lengo ni kujua tulikosea wapi ili tujue tunarekebisha vipi, sikuona watu wakimlalamikia Magufuli kuwasema marais hawa wastaafu
Magufuli alisikika mara nyingi tu akisema hawezi kutatua shida za wananchi maeneo ambayo wamechagua upinzani, alisikika pia mara nyingi akiwatishia wananchi waziwazi wakichagua diwani ama mbunge wa upinzani basi serikali yake haitotatua shida zao kabisa..hizi sio kauli za kiungwana na zinafaa kukemewa kama tunataka kujenga taifa pasipo unafiki
Magufuli pia alisikika akiwaambia Tanroads wasiwabomolee watu wa Mwanza kwa kuwa walimpa kura nyingi huku bomoa bomoa ikiwa imefanyika kwa wakazi wa Kimara Dar huku kukiwa na zuio la mahakama, hii haikuwa uungwana hata kidogo kufanywa na kiongozi wa nchi na inafaa ikemewe
Rais pia alisikika akitoa hotuba kwa kilugha cha kwao mara nyingi wakati wa kampeni za uchaguzi hata wakati wa hotuba za kawaida, hii haikuleta picha nzuri, na kama tunataka kujenga taifa lisilo na wanafiki yafaa kukemea mambo haya
Namuunga mkono Rais Samia, amekuwa akirekebisha mabaya ya Magufuli na kuendeleza yale mazuri, na asiogope kusema kuwa sehemu fulani tul;ikosea kwani uwazi na nuaminifu ndio hujenga taifa imara