Naungana na wasioamini uwepo wa Mungu

NIMESIKITIKA na KUUMIA kwa ajili ya mtoa maada. Pamoja na kwamba siendi kanisani wala msikitini na wala sio muumini wa dini yeyote ile. Ila Naamini kuwa Mungu yupo. Na uwepo wake una athari wa moja kwa moja katika maisha yetu.

Sikulaumu sana hata mimi kuna kipindi cha ujana nilishawishika kuwaza hivyo lakini pia nilikuwa najiuliza maswali mengi kumhusu Mungu, asili yake, jinsi ulimwengu ulivyoumbwa na chanzo chake, je Mungu ni mmoja au ni muunganiko wa miungu miungu mingi inayojenga taasisi moja ya Umungu, je sisi wanadamu tuliumbwaje kwa material gani, kama inavyosemwa katika biblia kuwa hapo mwanzo lakini kabla ya mwanzo kilikuwa na nini, je kuna viumbe wengine kama sisi.

Maswali ni mengi sana mengine nimepata majibu ila mengi sana bado.

Ukihusianisha miendenendo mibovu ya viongozi wa dini unaweza kushawishika kuwa hakuna Mungu kwa kuwaza kuwa kama kuna Mungu kwanini asiwaadhibu hao watu.

Pamoja na vyote hivyo Mzee nakushauri sana amini kwamba Mungu yupo na kama mimi na wengine tulivyoumia kuhusu hii makala yako basi hata yeye anaumia hata zaidi because you do not acknowledge him despite all the evidence.

Omba msamaha kwa Mungu naye atakusamehe.

Mimi nilikuwa mkristo na bado kuna mambo nayaamini katika ukristo ila ni ukweli kwamba biblia imeficha mambo mengi sana ambayo tulitakiwa kuyajua kuhusu Mungu na ulimwengu.

Huwa Naamini kuhusu neno "Mtaujua ukweli nao ukweli utawaweka huru" lakini pia "wingi wa maarifa huleta huzuni." Ni sahihi kuwa na maswali na kuchunguza ila usiende mbali zaidi na kusema hakuna Mungu. Unakosea sana.

Kuna mchangiaji mmoja alishwahi kusema kuwa Wanadamu ni matokeo ya biological Engineering iliyofanyika katika gallaxy ya Alpha Centauri. Yale mawazo yake yalinifikirisha sana na kuona nadharia ile unaweza kuwa na ukweli ndani yake.

Mungu yupo Ndugu. Hata kama huamini kuwa Mungu basi amini kuwa ni form fulani ya Supreme Power running the whole universe.
 
MKUU MUNGU YUPO ILA DINI ACHANA NAZO UTAKUJA NISHUKURU
 
Uzuri Mungu ameweka maisha ya binadamu siyo mengi ni kati ya 60, 70 au 80 utajua bada ya kufa kama Mungu yupo au hayupo
Mungu asiyeonekana wakati uko hai ati usubiri mpaka ufe huyo hayupo. Kwenye biblia kumejaa simulizi nyingi za Mungu kujionyesha kwa wanadamu kwa namna mbalimbali. Sasa miungu iko mingi tu na mingi ni ya kufikirika tu ndio hiyo mtu anaiamini haoni matokeo yoyote. Yapo hata makanisa yanahubiri miungu ambayo si Mungu halisi. Yaani kama wale manabii wa mungu Baali na siku hizi kuna manabii na mitume wanaohubiri miungu isiyo Mungu. Ndio utawasikia usiku kucha wakipiga makelele mpaka na kwenye redio. The same scenario kama wale manabii wa Baali!
 
Umekosea KIDOGO sana NAMNA ulivyoanza sentensi yako.

Ulitakiwa uanze hivi: NAUNGANA NA WAJINGA.......

HAWA WATU PAMOJA NA wewe ni WAJINGA kwa sababu hawajui
 
Umekosea KIDOGO sana NAMNA ulivyoanza sentensi yako.

Ulitakiwa uanze hivi: NAUNGANA NA WAJINGA.......

HAWA WATU PAMOJA NA wewe ni WAJINGA kwa sababu hawajui
Sawa mjanja unae amini kitu hukioni...!
 
K
Leo hii mtu akijiita NGOSHA anaonekana mjinga na mlugaluga...ila Michael au John ndio wanaonekana wajanja na wanao enda na wakati...
Kwanini unajiita X_INTELLIGENCE? Heri ungejiita hata Masalakulangwa

Huna tofauti yoyote na wanaojiita Michael au John.

Tuliza komwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…