Car4Sale Nauza gari 2,200,000/=

Car4Sale Nauza gari 2,200,000/=

Bro hongera kwa kuweka tangazo kwa lugha nzuri ya Kitanzania pole kwa kejeri unazopewa na watu wenye akili za malezi ya kiteja.
Watu wa jamiiforum ni wa ajabu sana. Nishakumbana nao katika posti yangu moja katika harakati za kimaisha lkn nilisimamia ninachokiamini. Kaka wenye nia na hiyo gari watakutafuta maana hujaomba uchangiwe pesa humu JF maana ungeitwa tapeli na kibaka. Stand up wiz ur dream.
 
Bro hongera kwa kuweka tangazo kwa lugha nzuri ya Kitanzania pole kwa kejeri unazopewa na watu wenye akili za malezi ya kiteja.

Watu wa jamiiforum ni wa ajabu sana. Nishakumbana nao katika posti yangu moja katika harakati za kimaisha lkn nilisimamia ninachokiamini. Kaka wenye nia na hiyo gari watakutafuta maana hujaomba uchangiwe pesa humu JF maana ungeitwa tapeli na kibaka. Stand up wiz ur dream.

Nashukuru sana mpendwa, watu wa kutoa kejeli nimeishawazoea halafu kama ingekuwa ndio gari yangu ya kwanza ningeishakata tamaa ila hii ni gari yangu ya tatu kuuza humu na gari zangu mbili za mwanzo nimeuza humu humu, gari yangu ya kwanza ilikuwa nissan march nyekundu ya mwaka 1998 nilipoitangaza humu nilipata maneno ya kukatisha tamaa lakini akatokea mteja kutoka mwanza akaja kuinunua na akasafiri nayo mpaka mwanza ila kama unavyojua kwa nissan watu humu waliponda ohoo spea zake ghari mara maneno ya kejeli kibao lakini mwisho wa siku niliuza, gari yangu ya pili ni nissan march.

Pia ya mwaka 2004 ile yenye muundo wa kobe watu waliniponda lakini mwisho wa siku nikamuuzia humu humu jamaa mmoja wa uhamiaji dar es salaam. sasa kwa gari yangu hii ya tatu kuuza humu na kukutana na maneno ya kejel hakika sintokata tamaa halafu uzuri wa hii gari engine yake unaweza kuiweka karibia gari zote za Toyota ikiwemo Hiace na Noah kwa hivyo nikikosa mteja kwa bei ninayoitaka mimi nitaendelea kuitumia na nikiichoka natoa engine, gear box na control box yake natafuta body nyingine ya gari ya toyota nafunga, na body ya chasser napeleka pale mabibo nauza, sasa wanaonibeza wanafikiri mimi ni mgeni wa haya mambo.

Nashukuru sana Ng'wanapagi kwa maneno yako mazuri.
 
Watanzania tulio wengi tumekuwa watu WA kukatishana Sana tamaa, by the way hizo in baadhi ya tabia za walioshindwa. Mara zote Tangazo linapowekwa humu huwa kuna walengwa, kama unajihisi sio mmoja wao huna haja ya kuja name kejeli humu.
 
Bei inapungua mpaka ngapi mkuu..??
itategemea na wewe utakapokuja kuiona na kama utakuwa na nia ya kuinunua wewe unaniambia pungufu yako kama inawezekana tunafanya biashara kwahivyo kuwa na aman
 
WaTz wamezoea kuuziwa vitu bei gali ukimuuzia rahis anahs unamwibia hahahahahaha
Mtu unaweza kuuza kitu kwa changamoto ulizo nazo ili uzisolve fasta kwahyo nikawaida bei hiyo tu mteja atapatikana tu mkuu
 
Watu wengine hawana akili kabisa eti siwezi kua mteja kwani umeambiwa uwe mteja? Km huwezi nunua wapo watakao nunua utakuja kuolewa mume si wako
 
mimi sio mteja, ila nakupongeza kwa kuweka tangazo lako vizuri sana, nimekuwa nikigombana na watu mara zote hapa jf kuweka matangazo kama wanachuki na hy biashara. kila kheri
 
Back
Top Bottom