Nauza gari yangu, GX100 kwa member haina udalali

Nauza gari yangu, GX100 kwa member haina udalali

Picha hujaziweka sawa mkuu
weka picha namna hii
IMG_20220112_094258_267.jpg

kwa msaada zaidi wa kuwekewa picha kama hivyo njoo na buku watsap 0767-733-555
 
Anayeuza hataki dalali...ghafla dalali anatokea ah ah ah ah
Madalali acha kabisa! Hapo dalali tayari ameshanusa harufu ya mnuso. Muda si mrefu atakuja kutuuzia gari hii hii kwa milioni 5!! Na wakati mmiliki ameanzia na milioni 4 tu.
 
Sikukatishi tamaa Ila nakueleza ukweli, mil 4 Tena kwa gari hiyo tena kwa namba B Huuzi.
Hapo hamna hamna Ni mil 2.5 ikizidi sana mil 3.

Mil 4 ni bei ya Altezza, Verossa, GX 110, na jamii ya hizo tena kwa namba C.
 
Gari imetulia sana..wewe kweli ni mmiliki huna janja janja...nakupongeza na nakutakia mauzo mema
Asante Sana mkuu. Kwenye hivi vyombo utunzaji ni muhimu sababu huwa usipotunza ukataka kuuza inakuwa ngumu, lkn ukitunza mteja akija, msisitize aje na fundi aendeshe tena kwenye njia mbovu mbovu, hachomoki ! Haha haa
 
Hujasema iko mkoa gani ,si unajua wengine tuko hku mbali mpakani na tanzania
Samahani niko Dar es Salaam, Zakhiem kiwanda cha simenti siku za weekdays, na siku za weekend nakuwa Kitunda Relini, gari inakuwa maeneo hayo sababu inatumika
 
Back
Top Bottom