Asante Kwa maoni yako, Altezza, GX110 na Verossa zipo za bei chini zaidi ya hiyo uliyotaja, mimi si mgeni wa kumiliki magari, nina umri wa miaka 43 sasa hivi, nilianza kumiliki magari nikiwa na miaka 26. Nilianza na Cresta Balooni, niliuza Dodoma miaka hiyo, Suzuki Escudo, nikauza hapa hapa Dar, Subaru Legacy tena toleo la kwanza, 1990 nikauza Arusha, nikanunua Cresta kama hilo hapo juu, rafiki yangu akanivua morogoro, nikanunua Mark ii GR kutoka Las Vegas Casino, gari ya kampuni na ilikuwa imesimama balaa, hilo nilikuwa nasimamishwa na watu wakitaka niwauzie. Niliuza kwa jamaa mmoja anaduka la matairi Temeke, baadaye nikabahatisha hili kwa jamaa mmoja Arusha, yeye aliuza baada ya kununua Harrier. Ukisoma hayo maelezo utagundua mimi si njegeka. Najua magari na najua engines, transmissions, spare parts, nina wauza spare ambao ni marafiki kutoka tandika/urafiki kwa wakataji hadi ilala shaurimoyo. Kama unataka kupunguziwa unaweza kupiga simu, ila Udalali hapana, mnaumiza wanunuzi